JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TANZIA: ALIYEKUWA BALOZI WA TANZANIA URUSI AFARIKI

> Aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi katika Serikali ya Awamu ya Nne, Balozi Jaka Mwambi amefariki leo Desemba 8, 2019

> Pia, marehemu aliwahi kuwa Mkuu wa Mikoa ya Tanga, Rukwa na Iringa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara

Soma - https://jamii.app/RIPBaloziMwambi
SHINYANGA: WANAUME WADAIWA KUWAOZESHA WATOTO WAO WADOGO KWA POMBE

- Wanawake katika Kijiji cha Penzi wamewashutumu Wanaume kwa kuwaozesha watoto wao bila kuwajulisha kwa kubadilishana na jagi la pombe wawapo vilabuni au mifugo aina ya ng’ombe

Zaidi, soma https://jamii.app/WanaumeKuozaBinti-SHY
Bodi, Uongozi na Wafanyakazi wote wa Jamii Forums tunaungana na Watanzania wote kusheherekea Kumbukumbu ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika
MLIMBWENDE WA AFRIKA KUSINI ATWAA TAJI LA MISS UNIVERSE

- Zozibini Tunzi (26) ameshinda taji hilo katika mashindano yaliyofanyika Atlanta, Georgia

- Madison Anderson (Puerto Rico) amekuwa mshindi wa pili huku Sofía Aragó (Mexico) akiwa mshindi wa tatu

Zaidi, soma https://jamii.app/MissUniverse2019-SA
MBEYA: AUAWA AKITUHUMIWA KUWATESA WANANCHI KWA UCHAWI

- Polisi inawashikilia Watu watatu wakidaiwa kumuua John Mwakarundwa(62), Mkazi wa Kijiji cha Nkunga, Rungwe

- Wananchi walikuwa wakimtuhumu Marehemu kununua uchawi Malawi na kuwatesa nao

Zaidi, soma https://jamii.app/AdaiwaMchawiAuawa
NEW ZEALAND: MMOJA AFARIKI NA TAKRIBAN 27 HAWAJULIKANI WALIPO KUTOKANA NA MLIPUKO WA VOLKANO

- Watu 23 wameokolewa katika Mlipuko huo uliotokea kwenye Mlima uliopo Kisiwa cha 'White Island'

- Polisi imesema kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka

Zaidi, soma https://jamii.app/MlipukoVolkanoNewZealand
MIAKA 58 YA UHURU: RAIS MAGUFULI ASAMEHE WAFUNGWA 5,533

- Amesema, ameshuhudia mrundikano wa wafungwa ambapo hadi leo kuna Wafungwa 17,547 na Mahabusu 18,256

- Amesema, baadhi yao wamefungwa kutokana na makosa madogo yakiwemo ya kuiba kuku

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAhameheWafungwa5533
TIMU YA TAIFA YA URUSI YAFUNGIWA KUSHIRIKI MICHEZO MIKUBWA

- Wakala wa Kupambana na Dawa za Kuongeza Nguvu (WADA) wameifungia Timu ya Soka ya Urusi

- Haitashiriki michuano ya Olimpiki ya mwaka 2020 na Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar

Zaidi, soma https://jamii.app/TimuUrusiYafungiwa
MBINU ZA KUKUWEZESHA KUFANYA BIASHARA KWA MTAJI MDOGO

> Chagua wazo la biashara unalolipenda na kuliweza vyema

> Anza na unachokijua pasipo kuhusisha mambo mengi mageni kwa kuwa huna pesa za kuyagharamia

> Waambie watu unachokifanya ili kupata wateja na kufahamika na usiogope kueleza kuwa unafanya biashara ya aina fulani

Soma - https://jamii.app/BiasharaMtajiMdogo
#JFBiashara
CHILE: NDEGE YA KIJESHI ILIYOKUWA NA WATU 38 YAPOTEZA MAWASILIANO ANGANI

- Ilikuwa na Wafanyakazi 17 na Abiria 21 ikielekea katika Kambi ya Jeshi huko Antarctica

- Shughuli za kuitafuta ndege hiyo zimeanza kwa kutumia ndege na meli za Jeshi

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeJeshiYapotea-CHL
👍1
SIKU YA HAKI ZA BINADAMU: VIJANA WANASIMAMIA HAKI ZA BINADAMU

- Kila Disemba 10 ni Siku ya Haki za Binadamu na mwaka huu Kaulimbiu ni 'Vijana Wanasimamia #HakiZaBinadamu'

- Kila mtu anatakiwa kupata haki bila kujali dini, rangi wala hadhi yake

Zaidi, soma https://jamii.app/SikuHakiBinadamu
KIGAMBONI, DAR: Mwenyekiti wa Mtaa wa Changanyikeni kata ya Toangoma aliyepita bila kupingwa kwa tiketi ya CCM ametiwa mbaroni kwa kosa la “wizi” wa TZS 12,000,000/-

> Ni Suzanne(Dionisia) Kamugisha

> Yadaiwa alizitumia kwa ajili ya Kampeni za Uchaguzi wa Ndani wa chama

Zaidi, soma https://jamii.app/MwenyekitiMtaaMbaroni-KGMB
DAR: ALI MUFURUKI AAGWA KATIKA UKUMBI WA JULIUS NYERERE

- Mwili wa Mfanyabiashara huyo utazikwa leo katika Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar

- Alizaliwa Novemba 15, 1958 na amekuwa Mwenyekiti na Mjumbe wa zaidi ya bodi 30 za Kampuni mbalimbali

Zaidi, soma https://jamii.app/AliMufurukiAagwa-Dar
SUDAN KUSINI: SPIKA AJIUZULU, ASHUTUMIWA KWA KUTOWASILISHA RIPOTI YA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI

- Spika wa Bunge, Anthony Lino Makana amejiuzulu baada ya Wabunge kutishia kumuondoa madarakani kwa kuzuia juhudi za kupambana na rushwa

Soma > https://jamii.app/SpikaSudanKusini
FINLAND: WAZIRI MKUU MDOGO DUNIANI KUAPISHWA WIKI HII

- Sanna Marin (34) aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi amechaguliwa baada ya Antti Rinne kujiuzulu

- Pamoja na kuwa Waziri Mkuu mdogo Duniani, atakuwa ni wa 3 wa kike kuhudumu katika taifa hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/SannaWaziriMkuuMdogo
JE, KUNA MBINU ZA KUDHIBITI 'CHUMA ULETE' KWENYE BIASHARA?

> Mwanachama wa JamiiForums anasimulia kuwa alianza kufanya biashara maeneo ya Kimara Jijini Dar es Salaam baada ya muda aliihamishia biashara yake Mkoani Mtwara

> Anapata fedha nyingi lakini tatizo zinapotea katika mazingira ya kutatanisha 'Chuma Ulete'

Soma ~ https://jamii.app/ChumaUleteMtwara
NBS: MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.2 KWA MWEZI MMOJA

- Mfumuko wa bei kwa Novemba 2019 umeongezeka hadi 3.8% kutoka 3.6% mwezi Oktoba 2019

- Baadhi ya vyakula vilivyoongezeka bei ni mchele kwa 6.6%, nyama 2.6%, maharage 8.6%

Zaidi, soma https://jamii.app/MfumukoBeiNov2019
CECAFA Senior Challenge: Timu ya Taifa ya Tanzania Bara #KilimanjaroStars imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Timu ya Zanzibar #ZanzibarHeroes

- Ditram Nchimbi amefunga goli hilo na kuipatia timu hiyo alama tatu za kwanza baada ya kufungwa katika mchezo wa kwanza

#JFLeo
UGANDA: WATU 36 WAFARIKI KUTOKANA NA MAFURIKO

- Watu wengi bado hawajulikani walipo kutokana na mafuriko ya mvua zinazonyesha Mashariki mwa Uganda

- Aidha, maporomoko ya udongo yamewaacha maelfu ya watu bila makazi

Zaidi, soma https://jamii.app/UgandaFloods-Death36
MPYA: Milio ya risasi imerindima kati ya Al-Shabaab na Walinzi wa Hoteli ya Kifahari ya SYL katika Mji Mkuu wa Somalia, Mogadishu

- Al Shabaab wamevamia hotel hiyo karibu na Makazi ya Rais inayotumiwa zaidi na viongozi wengi wa Kisiasa

- Idadi ya Vifo bado haijajulikana

Zaidi, soma https://jamii.app/AlShabaabSYLHotel-Somalia