JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: GAVANA WA JIJI LA NAIROBI, MIKE SONKO AKAMATWA NA TAASISI YA KUPAMBANA NA RUSHWA

- Imeelezwa kuwa Sonko amekamatwa akituhumiwa kwa kujipatia kiasi cha zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 8 kinyume cha sheria ya manunuzi

Zaidi, soma > https://jamii.app/SonkoMbaroni
MANYARA: RC MNYETI AFUTA KIKUNDI CHA WATU WA KILIMANJARO

> Ni kikundi cha watu wa Kilimanjaro waishio Manyara

> Asema ataendelea kuvifuta vikundi vyote vya watu kutoka mikoa mingine waishio Manyara kwani havina faida mkoani humo na vinaendekeza ukabila

Soma http://jamii.app/RCMnyetiTena
GABON: MTOTO WA RAIS ATEULIWA KUWA MRATIBU WA MASUALA YA RAIS

> Mtoto wa Rais Ali Bongo wa Gabon, Noureddin Bongo Valentin ameteuliwa kuwa Mratibu wa masuala ya Rais ili kumsaidia Rais katika masuala yote ya Kitaifa

> Nafasi hiyo imetengenezwa baada ya Kikao cha Baraza la Washauri na kutolewa taarifa rasmi na Msemaji wa Serikali

Soma - https://jamii.app/NafasiMratibuRaisGabon
TABORA: MWANDISHI AOKOTWA PORINI NA KUDAI ALITEKWA. POLISI WASEMA HUENDA ALIKUWA KWENYE MAMBO YAKE BINAFSI

- RPC Barnabas Mwakalukwa amesema mtekaji hawezi kukuacha kinyeji tu anaweza akawa na mambo yake ya ajabu, pengine mambo ya Wanawake

Soma > https://jamii.app/PolisiVsBahamu
MAURITANIA: WAHAMIAJI 62 WAFARIKI BAADA YA BOTI YAO KUZAMA

> Takriban wahamiaji 62 wakiwamo watoto wamefariki baada ya boti waliyokuwa wanaitumia kusafiri kuzama katika Bahari ya Atlantiki nchini Mauritania

> Boti hiyo iliyokuwa imebeba watu 150 iliishiwa mafuta na kukwama kwa siku kadhaa kabla ya kuzama

Soma - https://jamii.app/VifoWahamiajiBotiKuzama
UGANDA: MCHUNGAJI MBARONI KWA KUWANYWESHA WAUMINI SUMU

> Mchungaji Sam Little (25) raia wa Uingereza amekamatwa kwa tuhuma za kuwanywesha waumini dawa ya kujichubua na kuwaaminisha kuwa ni tiba ya miujiza inayotibu Malaria, Saratani na UKIMWI

> Pia, walikamatwa raia wawili wa Uganda ambao walikuwa wakishirikiana naye

Soma - https://jamii.app/MchAnyweshaWauminiSumu
WAZIRI MKUCHIKA: VIONGOZI WA IDARA NI CHANZO CHA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU

> Amepiga marufuku viongozi wa Serikali kuzuia barua za watumishi kufika eneo linalohusika na hata kama inakwenda kwake

> Aidha, amewaonya viongozi wanaowafukuza kazi watu ambao hawajawateuwa na hawana mamlaka nao

Soma - https://jamii.app/ViongoziHakiBinadamu
TANZIA: SETH KANUMBA AFARIKI DUNIA

> Seth Bosco ambaye ni mdogo wa Marehemu Steven Kanumba, amefariki usiku wa kuamkia leo baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwa Mama yake Kimara, Dar

> Alifanyiwa upasuaji wa Uti wa Mgongo baada ya kupooza

Soma > https://jamii.app/RIPSethKanumba
RWANDA: KIONGOZI WA UPINZANI AZUIWA KUSAFIRI KWENDA KUPOKEA TUZO

- Kiongozi wa Upinzani nchini humo, Victoire Ingabire Umuhoza amezuiwa kusafiri kwenda Uhispania kupokea Tuzo ya Haki za Binadamu aliyoshinda

- Mwezi Mei alizuiwa kwenda Ujerumani

Soma > https://jamii.app/VictoireVsRwGvt
BRAZIL HATARINI KUPOTEZA HAKI YA KURA UN KUTOKANA NA ADA YA UANACHAMA

> Hadi sasa nchi wanachama 54 hazijalipa michango ikiwemo Brazil ambayo inadaiwa na Umoja huo zaidi ya dola milioni 415

> Kwa mujibu wa ibara ya 19 ya sheria ili Brazil isipoteze haki hiyo inapaswa kulipa dola milioni 126 kufikia mwishoni mwa mwaka 2019

Soma - https://jamii.app/BrazilDebtUNFee
KENYA: WATU 10 WAPOTEZA MAISHA KWENYE SHAMBULIO LA KIGAIDI

> Takriban watu 10 wamefariki katika kaunti ya Wajir siku ya Ijumaa baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi Al-Shabaab kushambulia basi

> Kati ya waliofariki wapo Askari Polisi 7, Daktari pamoja na raia 2

Soma https://jamii.app/WajirTerrorAttack
VICHOCHEO VINAVYOWEZA KUMUATHIRI MTOTO MWENYE PUMU

> Mabadiliko ya halijoto: Mabadiliko haya huweza kupelekea dalili za pumu na hata kusababisha kushikwa na pumu

> Kichocheo cha vumbi: Vumbi huchangia kwa kiasi kikubwa sana kushikwa na pumu. Vumbi lipo kila mahali lakini jitihada zinaweza kufanyika ili kulipunguza nyumbani

> Wanyama pia huweza kusababisha dalili za pumu hasa paka, mbwa na kuku. Viumbe hawa mara nyingi wanatumia vumbi kama njia ya kujikuna na kuondoa wadudu katika miili yao

Tembelea - https://jamii.app/VichocheoPumuMtoto
MICHEZO: Klabu ya Chelsea yanyukwa bao 3 kwa 1 na Everton

> Magoli ya Everton yamefungwa na Richarlison dakika ya 5 na Calvert-Lewin aliyefunga dakika ya 49 na 84

> Goli pekee la kufutia machozi la Chelsea FC limefungwa na Mateo Kovačić kunako dakika ya 52

#JFLeo #JFSports
RIPOTI: UMASIKINI WAPUNGUA TANZANIA KWA ASILIMIA 2

> Umaskini wa mahitaji muhimu umepungua kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007, asilimia 28.2 mwaka 2012, hadi asilimia 26.4 mwaka 2018

> Umaskini wa chakula umepungua kutoka asilimia 22 mwaka 1991/92, asilimia 19 mwaka 2000/01, asilimia 17 mwaka 2007, asilimia 10 mwaka 2011/12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017/18

Soma - https://jamii.app/TakwimuHaliUmasikini
MASUMBWI: Bondia Anthony Joshua kutoka nchini England amempiga kwa pointi bondia Andy Ruiz Jr. kutoka Mexico

- Wawili hao wamepambana usiku huu katika pambano la marudiano Uzani wa Juu lililofanyika nchini Saudi Arabia

- Anthony Joshua alipigwa na Andy Ruiz Jr. kwa TKO katika pambano lao la mwezi Juni 2019

#RuizVsJoshua2 #JFLeo
DELHI, INDIA: ZAIDI YA WATU 30 WAMEFARIKI BAADA KIWANDA KULIPUKA

> Mlipuko huo umetokea asubuhi ya leo na imeelezwa kuwa wengi wa waliofariki ni Wafanyakazi wa Kiwanda hicho waliokuwa wamelala

> Zaidi ya watu 50 wamejerujiwa

Zaidi, soma > https://jamii.app/FactoryBlazeDelhi
TANZIA: MFANYABIASHARA ALI MUFURUKI AFARIKI

- M/Kiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Infotech Investment Group, Ali Mufuruki amefariki dunia leo

- Aliwahi kuwa Mkurugenzi Huru, Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania kabla ya kujiuzulu

Soma > https://jamii.app/RIPMufuruki
TANZIA: MHUBIRI NA MWINJILISTI REINHARD BONNKE AFARIKI DUNIA

- Bonnke amefariki akiwa na umri wa miaka 79

- Atakumbukwa kwa kuweka rekodi ya wahudhuriaji wengi katika mikutano yake aliyoifanya ktk mataifa mengi ya Afrika ikiwemo Tanzania

Soma > https://jamii.app/RIPBonnke
IRAN: WATU 81 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA HOMA YA MAFUA

> Watu 81 wamepoteza maisha kwa sababu ya Homa ya Mafua nchini Iran huku wiki iliyopita, watu 8,333 wamefikishwa hospitalini wakilalamika kuandamwa na Mafua Makali

> Hali hiyo ilimepelekea msongamano wa wagonjwa na wengine kutibiwa wakiwa wamesimama

Soma - https://jamii.app/VifoHomaMafua
MASHIRIKA YA KIRAIA DRC YAIOMBA ICC KUCHUNGUZA MAUAJI YA RAIA

> Mashirika ya Kiraia na Wadau mbalimbali Duniani, yameitaka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ktk Mahakama ya Kimataifa ya ICC kuchunguza mauaji yanayoendelea Wilayani Beni

> Tangu mwezi Novemba, watu zaidi ya 100 wameuawa baada ya kushambuliwa na waasi wa ADF Nalu

Soma - https://jamii.app/ICCAssistanceBeniMassKilling