JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAHAFALI UDOM: RAIS MAGUFULI ATUNUKIWA SHAHADA YA UDAKTARI WA FALSAFA

> Rais Magufuli ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa katika Sayansi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

> Shahada hiyo imetolewa kutokana na uongozi wake katika ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwa kuwekeza ktk Sekta za Maendeleo

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliPhdFalsafa
MDHAMINI WA LISSU: LISSU AMESHAPONA, ANASHINDWA KUREJEA NCHINI AKIHOFIA USALAMA WAKE

- Ibrahim Ahmed, aliyasema hayo leo Novemba 21, alipokuwa akiieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juu ya maendeleo ya afya ya Mwanasheria huyo wa CHADEMA

Soma https://jamii.app/MdhaminiAsemaLissuKapona
#JFLeo
SHINYANGA: ASHAMBULIWA NA FISI USIKU AKIWA AMELALA

- Mkazi wa Kijiji cha Chela, Buluba Jilasa(70) amejeruhiwa na fisi kwa kung’atwa sehemu mbalimbali za mwili

- Asema alishtuka mlango ukivunjwa na fisi huyo aliingia hadi chumbani na kumjeruhi

Zaidi, soma https://jamii.app/FisiAjeruhiMzee
SOMALI: MWANAHARAKATI ALMAAS ELMAN AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

- Ameuawa jana akiwa njiani kuelekea Uwanja wa ndege wa Mogadishu akiwa safarini kurudi Nairobi

- Ni mtoto wa Mwanaharakati wa amani wa Somalia, Elman Ahmed aliyeuawa mwaka 1996

Zaidi, soma https://jamii.app/AlmaasElmanAuawaSML
ATHARI ZA MVUA, DAR: AFARIKI AKIJARIBU KUTOKA NDANI YA NYUMBA ILIYOJAA MAJI

- Mwenga Agustino(78) amefariki akijiokoa kwenye nyumba iliyojaa maji

- Alizidiwa nguvu na maji, Wananchi walimuokoa lakini alifariki njiani akipelekwa hospitali

Zaidi oma https://jamii.app/MvuaYaua1Dar-Nov19
Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa JamiiForums tunakupongeza Maxence Melo kwa tuzo hii ambayo inasimama kama kilelezo kizuri cha kazi nzuri inayofanywa na timu nzima ya JamiiForums chini ya uongozi wako
DRC: TAKRIBAN WATOTO 5000 WAFARIKI KUTOKANA NA UGONJWA WA SURUA

> Ugonjwa wa Surua umewaua takriban watoto 5000 kwa mwaka 2019 na takriban watoto 250,000 wameambukizwa ugonjwa huo kwa mwaka huu pekee

> Watoto milioni 4 tayari wamepewa chanjo, lakini wataalam wameonya kwamba idadi hiyo ni chini ya nusu ya jumla ya watoto wote na chanjo zilizopo hazitoshi

Soma - https://jamii.app/VifoWatotoSurua5K
KAGERA: RC AAGIZA MKUU WA SHULE NA MKANDARASI KUKAMATWA

- Brig. Marco Gaguti ameagiza kukamatwa Mkandarasi wa Manispaa ya Bukoba na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kahororo kutokana na kutokukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya shule kwa wakati

Zaidi, soma https://jamii.app/RC-KGRKukamatwaMkandarasi
DAR: TAPELI AKAMATWA AKIWA NA KADI 23 ZA BENKI

- Polisi inamshikilia Halima Juma (23) akidaiwa kukutwa na kadi 23 za ATM alizokuwa akitumia kutapeli

- Inadaiwa alikuwa anawabadilishia watu kadi zao katika ATM wakati akijifanya kuwapa msaada

Zaidi, soma https://jamii.app/TapeliKadiATM23
NDEGE NYINGINE YA TANZANIA YAKAMATWA CANADA

- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ndege aina ya Bombardier Q400 imekamatwa

- Ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa na kesi ipo Mahakamani

Zaidi, soma https://jamii.app/BombardierTZYakamatwaCND
HIFADHI MPYA 3 ZATANGAZWA NCHINI

Sehemu ya Pori la Akiba la Selous lenye Km za mraba 30,893 imekuwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere

Hifadhi ya Taifa ya Kigosi yenye Km za mraba 7,460 na Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla yenye Km 3,865 zimeanzishwa

Zaidi, soma https://jamii.app/HifadhiTaifa3Mpya
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara imefanikiwa kutinga fainali ya Michuano ya CECAFA Senior Women’s Challenge Cup baada ya kuifunga Uganda goli 1-0
-
Timu hiyo itacheza Fainali dhidi ya Kenya siku ya Jumatatu Novemba 25, 2019 huku Mshindi wa tatu itakuwa ni kati ya Burundi na Uganda
KENYA: WATU 37 WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MAPOROMOKO YA UDONGO

- Wamefariki kutokana na matukio ya maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa eneo la Pokot Magharibi

- Maporomoko hayo yaliathiri zaidi Vijiji vya Nyarkulian na Parua

Zaidi, soma https://jamii.app/MafurikoKenya37WafarikiKenya
NOVEMBA 24, 2019: UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUFANYIKA LEO

- Kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni Wananchi watakuwa wakipiga kura

- Wale wote watakao kuwa kwenye foleni ifikapo saa kumi jioni wataruhusiwa kupiga kura

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziSMitaa2019
AFYA: Mafuta ya Mzeituni(olive oil) yamegundulika kuwa na faida nyingi kwenye mwili wa binadamu.

- Wataalamu wamegundua mafuta haya yanasaidia kuondoa maumivu ya tumbo, huduma ya kwanza kwa aliyekunywa sumu, tiba ya ugonjwa wa kusahau na pia kukojoa kitandani.

Zaidi, soma > https://jamii.app/OliveOil
DAR: UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

- Mtangazaji wa BBC Swahili, Sammy Awami: Hadi saa nne asubuhi kulikuwa hakuna vifaa vya kura katika Kituo cha Mwananyamala Mchangani

- Pia, Wasimamizi wa Uchaguzi hawakuwepo huku kukiwa na Wapiga Kura watatu ambao baadaye waliondoka kwa kuchoka kusubiri

Fuatilia https://jamii.app/UchaguziSMitaa2019
RAIS MAGUFULI: BAADA YA SIKU 60 BODI ZA MASHIRIKA YASIYOTOA GAWIO ZIJIVUNJE

- Atoa agizo hilo kwa Mashirika 187 yenye hisa za Serikali ambayo hayajatoa gawio lake Serikalini leo

- Amesema muda huo ukifika Ma-CEO nao wajihesabu hawapo kazini

Zaidi, soma https://jamii.app/MashirikaGawioSiku60
BIASHARA: Kufanya uchunguzi wa kitu unachotaka kukifanyia biashara ni moja ya misingi 4 unayotakiwa kuifahamu kabla ya kuanza biashara. Pili, ni vema kufahamu wateja wa biashara unayotaka kufanya

- Tatu, fahamu changamoto wanazopitia wafanyabishara ambao tayari wanafanya biashara unayotaka kuifanya. Nne, fahamu Misingi ya muhimu kabla ya kuanzisha biashara.

Kwa uchambuzi wa kina, soma => https://jamii.app/MisingiBiashara
UFAFANUZI: Katika kituo cha Mwananyamala Mchangani hakukuwa na Uchaguzi kwani Mgombea wa CCM alipita bila kupingwa baada ya Wagombea wa vyama vingine kujitoa

- Aidha, Wananchi waliokutwa katika kituo hicho walikuwa hawana taarifa ya kutofanyika kwa Uchaguzi

Fuatilia https://jamii.app/UchaguziSMitaa2019
ARUSHA: ALIYEKUWA MGOMBEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ADAIWA KUCHINJWA

Aliyekuwa Mgombea wa Ujumbe eneo la Mnara wa Voda, kupitia CHADEMA kabla hakijajitoa, Sirili Homary amekutwa amefariki nyumbani kwake akiwa na alama ya kukatwa shingoni

Zaidi, soma https://jamii.app/MgombeaAkutwaAmefarikiAR