JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DR CONGO: TAKRIBAN WATU 28 WAMEFARIKI BAADA YA NDEGE KUANGUKA

- Wamefariki Mashariki mwa Nchini hiyo baada ya ndege iliyokuwa na Watu 18 (Abiria 16 na Rubani 2) kuanguka katika Makazi ya Watu na kuua waliokuwemo ndani ya ndege na Wakazi 10

Zaidi, soma https://jamii.app/AjaliNdege28Wafariki-DRC
KILIMANJARO: MREMA ALIA KUCHEZEWA RAFU UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

- Mwenyekiti wa TLP, Agustino Mrema, amelalamika kufanyiwa hujuma na baadhi ya Mawakala wake kuondolewa kwenye vituo vya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ktk Kijiji cha Kiraracha

Zaidi, soma https://jamii.app/MremaRafuUchaguziSMitaa
CHADEMA YATANGAZA WAGOMBEA NGAZI YA KANDA

- Wagombea wa Uchaguzi Ndani ya chama hicho, ngazi ya Kanda wameteuliwa kwenye Kikao cha Kamati Kuu cha Novemba 23, 2019

- Chama hicho kinatarajiwa kufanya Uchaguzi wake Mkuu Desemba 18, mwaka huu

Zaidi, soma https://jamii.app/WagombeaKandaCHADEMA-2019
KENYA: WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA MOTO

- Regina Mueni (49), Bintiye Faith Mangeli (27) na Wajukuu wake Angel Masava (5) na Amelia Masava (2) walikuwa wamelala nyumba yao ilipochomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana

Zaidi, soma https://jamii.app/4FamiliaWafariki-KE
TMDA YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA DAWA ZA KIUNGULIA NA VIDONDA VYA TUMBO

> Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini imewataka watu waliokuwa wanatumia dawa za Raniplex 150mg, Rantac 500mg/mL na Aciloc 150mg, ambazo hutumika kwa Kiungulia na Vidonda vya Tumbo kuacha kutumia mara moja kwa ajili ya Usalama wa Afya

Soma - https://jamii.app/BanHeartburnMedication
RC GAMBO AJUTIA KUWAWEKA WATUMISHI NDANI BILA KUWASIKILIZA

- Amejutia alivyowaweka ndani saa 24 Watendaji wawili kwa kuchelewa kikao cha ghafla alivyokuwa DC wa Uvinza

- Baada kuwatoa, Mtendaji mmoja alimweleza anatokea umbali wa Km 422

Zaidi, soma https://jamii.app/GamboAjutiaKuwekaNdaniWatumishi
TAKWIMU ZA AJALI BARABARANI: MAGARI BINAFSI YAONGOZA KWA KUSABABISHA AJALI

> Kati ya Januari hadi Juni 2019, magari binafsi yamesababisha ajali 528, vifo 222 na majeruhi 453, kwa wastani; kila siku husababisha ajali 3, kifo cha mtu 1 mpaka 2 na majeruhi 2

> Pikipiki zimesababisha ajali 334, Mabasi ya abiria ajali 103, Malori ajali 167 wakati daladala zilipata ajali 143

Soma - https://jamii.app/AjaliMagariBinafsi
DC OLE SABAYA: WILAYA YA HAI HAITAKUWA UWANJA WA MAJARIBIO YA KISIASA

- Amewaonya ‘Wahalifu wa Kisiasa’ aliodai wamekuwa wakitumia Wilaya hiyo kujipatia umaarufu

- Amesema watamfyatua yeyote atakayeenda Wilayani humo kuitukana Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/SabayaHai-UwanjaKisiasa
MTANZANIA ATEULIWA KUWA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA SEKRETARIETI YA MKATABA UN

> Elizabeth Mrema ameteuliwa kuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Sekretarieti inayosimamia Mkataba wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa Tofauti za Kibiolojia (CBD) kuanzia Desemba 1, 2019

> Uteuzi huo umefanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) kufuatia kujiuzulu kwa Cristiana Pasca Palmer kutokana na sababu za kiafya

Soma - https://jamii.app/MtzKaimuKatibuCBD
FAHAMU CHIMBUKO LA MKATABA WA KIMATAIFA WA HAKI ZA WATOTO (UNCRC)

> Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto unasema Mtoto ni mtu yeyote mwenye umri wa chini ya 18. Katika hali na namna yoyote ile, jamii haina budi kutambua kwamba, mtoto ni mtu kamili na si sehemu ya mtu mwingine

> Mkataba unazitambua haki za watoto katika nyanja zote ambazo zimewekwa kwenye makundi matatu (3) muhimu; nayo ni: kundi la haki ya kulindwa, kundi la haki ya kupatiwa mahitaji na kundi la haki ya kushirikishwa

Zaidi, Soma - https://jamii.app/MkatabaUNHakiMtoto
KIJANA AMUUA MZAZI MWENZIE KUTOKANA NA WIVU WA MAPENZI

> Kijana aliyetambulika kwa jina la Paschal (24) anadaiwa kumuua RoseMary Gallus (34) kwa kumchoma kisu kisha na yeye kujichoma kisu kifuani na tumboni

> Wawili hao wamekutwa wamefariki (nyumbani kwa Mwanamke) Gongo la Mboto, Dar huku Mtoto wao (1) akiwa pembeni ya maiti za Wazazi wake na akiwa amejuruhiwa kidogo

Soma - https://jamii.app/MauajiWivuMapenzi
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: ASKOFU BAGONZA AHOJI FURAHA IKO WAPI?

- Amesema "Wanaodhani wana furaha, hawana furaha. Wapinzani na wapinzani wa wapinzani hawana furaha."

- "Wanaodhani hawana furaha ni kweli hawana furaha. Furaha iko wapi?"

Zaidi, soma https://jamii.app/BagonzaFurahaIpoWapi
DODOMA: Baadhi ya maneno aliyozungumza Rais Magufuli kuhusu Maaskari wanaokaa katika nyumba za Jeshi kukatwa mshahara ili kulipia nyumba hizo

- Rais ametoa kauli hizo leo alipokuwa anazindua Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa katika eneo la Kikombo

Zaidi, soma https://jamii.app/ZiaraMagufuliDodoma-Nov2019
MHADHIRI NIT AKIRI KUOMBA RUSHWA YA NGONO, AHUKUMIWA KULIPA FAINI AU KIFUNGO

> Mahakama ya Kisutu imemhukumu Mhadhiri wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (69) kulipa faini ya Tsh. Milioni 5 au kwenda jela miaka 3 baada ya kuomba msamaha na kukiri kuomba rushwa ya ngono kwa DPP

Soma - https://jamii.app/HukumuRushwaNgonoNIT
NJIA ZA ASILI ZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO

> Unahitaji walau vipande 5 vya matunda na mboga za majani. Kufanya hivi kutaweka mwili wako vizuri kwa kuwa matunda na mboga za majani vina nyuzi muhimu(valuable fibres) na vitamini muhimu

> Dhibiti kiwango cha Vinywaji vya Sukari unavyokunywa. Unywaji wa soda na juisi za viwandani huongeza utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kufanya uzito kuongezeka. Jitahidi kunywa glasi 8 za maji safi na salama

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/NjiaKupunguzaUzito
#JFAfya
KILIMANJARO QUEENS KUSHUKA DIMBANI LEO KUTETEA UBINGWA WA CECAFA

- Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara #KilimanjaroQueens inashuka dimbani saa 10:00 jioni leo, kuvaana na timu ya Taifa ya Wanawake wa Kenya kwenye fainali ya CECAFA kwa Wanawake