JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UPDATES: Timu ya Taifa ya Libya inapata goli la kusawazisha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 67 dhidi ya Taifa Stars na kufanya matokeo kuwa goli 1-1. Mpira unaendelea...
KUFUZU AFCON 2021: Timu ya Libya inapata goli lake la pili katika dakika ya 81 katika mchezo dhidi ya Taifa Stars na kufanya matokeo kuwa 2-1

- Taifa Stars ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli katika mchezo huo unaoendelea hivi sasa
KUFUZU AFCON 2021: TAIFA STARS YAPOTEZA DHIDI YA LIBYA

- Taifa Stars imefungwa goli 2-1 na Libya katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Kundi J uliochezwa Tunisia wa kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika 2021

- Stars ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa Nahodha Mbwana Samatta lakini Libya iliweza kusawazisha na hatimaye kupata goli la pili ambalo ni la ushindi
MICHEZO: JOSE MOURINHO AJIANDAA KUMRITHI POCHETTINO KATIKA KLABU YA TOTTENHAM

- Taarifa zinaeleza kuwa wawakilishi wa Jose Mourinho na wale wa Klabu ya Tottenham wanatarajiwa kufikia makubaliano mchana wa siku ya leo

Zaidi, soma > https://jamii.app/MourinhoSpurs
RC WA KILIMANJARO AMUONYA MBUNGE WA SIHA KUACHA UCHONGANISHI

- Dkt. Anna Mghwira amemtaka Mbunge Dkt. Godwin Mollel kuacha uchonganishi baina ya Watumishi wa Halmashauri, Madiwani na Wananchi, badala yake awe kiunganishi ili kuleta maendeleo

Zaidi, soma https://jamii.app/RCKili-MbungeSiha
RAIS ANAWEZA KUTOA MSAMAHA KWA MSHTAKIWA

> Rais wa Tanzania amepewa mamlaka ya kutoa msamaha kwa Mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya Mahakama kwa kosa lolote, hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 45.-(1) ya #Katiba ya Tanzania

#UmuhimuKatiba
MOURINHO AMRITHI POCHETTINO TOTTENHAM

- Jose Mourinho amechaguliwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham Hotspurs ya England hadi mwisho wa msimu 2023

- Kocha huyo wa zamani wa Klabu za Manchester United na Chelsea za England pia anachukua nafasi ya Mauricio Pochettino

Zaidi, soma https://jamii.app/PochettinoAfukuzwaSpurs
RAIS MAGUFULI AMTAKA MKURUGENZI WA NIDA KWENDA MOROGORO LEO

- Amemtaka kwenda kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi wakati wa kujiandikisha ili kupata Vitambulisho vya Taifa

- Pia, ametaka huduma hiyo iende kila Wilaya, kwani haiwezekani watu kutoka Wilayani kwenda Mjini la sivyo NIDA iwape Wananchi hela ya ‘guest’

Zaidi, soma https://jamii.app/MkurugenziNIDAvsMagufuli
MAGUFULI: UKIONA BEI YA MAHINDI IKO JUU, NENDA KALIME YAKO

- Amesema bei ya mahindi inapopanda na wachache kulalamika, Wakulima wanashangilia

- Amesema wakati wa kumpangia bei Mkulima umepita na katika kipindi chake hatampangia Mkulima bei

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliBeiWakulima
KAZI HUZAA UTAJIRI, KATIBA INATAKA WATU WAJITUME

- Ibara ya 25- (1): Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii, ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu

- Kila mtu anao wajibu wa kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazi halali

#UmuhimuKatiba
KIGOMA: MWALIMU WA SHULE YA MSINGI MBARONI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

- Zakaria Richard(30) anatuhumiwa kumbaka na kumlawiti Mwanafunzi(10) wa Darasa la 5

- Mwanafunzi huyo alikabidhiwa na wazazi wake kwa mwalimu huyo afundishwe Masomo ya Ziada

Zaidi, aoma https://jamii.app/MwalimuMbaroniUbakaji-KGM
CHAD: VIONGOZI WA WAASI NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI WAKAMATWA

- Jen. Abdoulaye Miskine na wenzake watatu wanadaiwa kuingia Chad kupitia Mji wa Tissi

- Maswali mengi yameibuka kutoka kwa wadau yakihoji iwapo walikuwa wanatafuta hifadhi Chad

Zaidi, soma https://jamii.app/WaasiAfrikaKatiMbaroni
SIKU YA MTOTO DUNIANI: NI MUDA WA WATOTO KUPATA HAKI ZAO

- Siku ya Watoto Duniani ilianzishwa mnamo 1954 na huadhimishwa Novemba 20 kila mwaka kukuza Umoja wa Kimataifa, Ufahamu wa masuala mbalimbali kati ya watoto Ulimwenguni kote, na kuboresha Ustawi wa Watoto
WABUNGE WA CHADEMA WALIOKIUKA MASHARTI YA DHAMANA WAONYWA NA MAHAKAMA

- Wabunge hao ni Peter Msigwa(Iringa Mjini), John Heche(Tarime Vijijini), Halima Mdee(Kawe) na Ester Bulaya(Bunda)

- Mahakama imesema kuwafutia dhamana ingekuwa hatua kali

Zaidi, soma https://jamii.app/WabungeCDMWaonywa-Kisutu
KAZI ZA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KWA MUJIBU WA KATIBA

- Atahakikisha matumizi ya fedha zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali yameidhinishwa

- Atahakikisha fedha zote zimetumiwa kama ilivyokusudiwa

#UmuhimuKatiba
MDAU: WANAOBUSU WATOTO WA WENZAO MIDOMONI WANANIKERA SANA

- Amesema, “Unakuta mtu kaja kutembelea mtoto wako au kamkuta umemshika anamchukua na kuanza kumpiga mabusu ya mdomoni. Huu ni uchafu sana, mimi sipendi kabisa tabia hiyo”

Kujadili, tembelea https://jamii.app/KissingAnothersKid
RUKWA: HAKIMU AVIFUNGULIA KESI VYOMBO VYA MAHAKAMA VILIVYOMFUTA KAZI

- Aliyekuwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kalambo, Jonathan Mgongoro amezipeleka Mahakamani, Tume ya Utumishi wa Mahakama na Kamati ya Maadili ya Maafisa wa Mahakama

Zaidi, soma https://jamii.app/HakimuAzishtakiKamatiMahakama
SONGWE: MVUA YAJERUHI NA KUHARIBU MAMIA YA NYUMBA

- Mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi jioni mkoani humo imesababisha uharibifu wa nyumba zaidi ya 360 katika Wilaya za Mbozi na Momba na kujeruhi watoto wawili

Zaidi, soma https://jamii.app/MvuaZaharibuNyumbaSNG
NJOMBE: MWANAMKE AKIRI KUMCHINJA NA KUMLA MTOTO WAKE

- Christina Mlelwa (38) anashikilikiwa na Polisi akituhumiwa kumchinja mwanae Joseph Gumbilo (4) mwenye ulemavu wa viungo

- Alikiri kumuua mwanae, kumla nyama na kutupa viungo vingine

Zaidi, soma https://jamii.app/AmchinjaAmlaMwanae-Njombe
KIGOMA: BABA LEVO AACHIWA HURU LEO

- Msanii na Diwani wa Mwanga Kaskazini, Clayton Chiponda ‘Baba Levo’ amemaliza kifungo cha miezi 5 na kuachiwa

- Ni baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa kifungo alichoongezewa baada ya kukata Rufaa ni Batili

Zaidi, soma https://jamii.app/BabaLevoAachiwaHuru