JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: WATU 10 WAPIGWA RISASI, WANNE WAFARIKI

- Watu 35 waliokuwa wanaangalia mpira wameshambuliwa Jumapili Usiku huko Fresno, California

- Watu hao waliokuwa wamekusanyika nyuma ya nyumba walifyatuliwa risasi na mtu ambaye hajafahamika

Zaidi, soma https://jamii.app/ShambulioRisasiFresno
IGP SIRRO: TUMEFUNGUA JALADA LA UCHUNGUZI KUHUSU AZORY

- Amesema uchunguzi juu ya kupotea kwa Mwandishi Azory Gwanda unaendelea

- Amesema ameshafungua jalada la uchunguzi na kuwataka wenye taarifa kuhusu tukio hilo kuzifikisha Polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/Sirro-LissuAzory
IGP SIRRO: ALIYEMPIGA LISSU RISASI BADO HAJAFAHAMIKA

- Amesema wanasubiri Lissu aje afungue kesi ili wajue kitu gani kimemtokea katika mazingira gani

- Amesema walipomtafuta dereva ilikuwa shida, Lissu mwenyewe wanamuona tu kwenye mtandao

Zaidi, soma https://jamii.app/Sirro-LissuAzory
TBA YATAKIWA KUTOPEWA MRADI, MTENDAJI MKUU ATAKIWA KUJITATHMINI

- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Nchini(TBA), Arch. Daud Kondoro ajitathmini utendaji wake

- Aidha, amewasimamisha kazi Wakurugenzi watatu wa Wakala hao

Zaidi, soma https://jamii.app/MtendajiTBAKujitathmini
ARUSHA: MWEKA HAZINA WA KIKUNDI ALIYEDAI FEDHA KUPOTEA KISHIRIKINA AKAMATWA

- TAKUKURU inamshikilia Mweka Hazina wa Kikundi cha Ujasiriamali cha Imani, Halima Mwidadi akituhumiwa kula Tsh. Million 39 za kikundi na kudai zimeyeyuka kishirikina

Zaidi, soma https://jamii.app/MwekaHazinaKikundiMbaroni-AR
UCHAGUZI MKUU WA CHADEMA KUFANYIKA DESEMBA 18, 2019

- Mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu umeanza leo hadi Novemba 30 mwaka huu

- Uchaguzi huo unahusisha nafasi mbalimbali ktk Uongozi ndani ya Chama ngazi ya Taifa na Mabaraza yake matatu

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziCHADEMA-2019
HAI, KILIMANJARO: KIJANA ADAIWA KUKAMATWA AKIWA NA MAMILIONI YA NOTI BANDIA

- Mdau wa JamiiForums anadai noti bandia za shilingi 10,000 na 5,000 ni nyingi kupita kiasi Wilayani humo

- Ameomba mtandao wa biashara hiyo haramu uchunguzwe

Soma > https://jamii.app/NotiBandiaMoshi
LUDEWA, NJOMBE: WASIOPANDA ZAO LA BIASHARA KWENDA RUMANDE

- DC Andrea Tsere ametangaza kumuweka rumande Mwananchi atakayeshidwa kuwa na zao la biashara kutokana na uhamasishaji mkubwa unaoendelea Wilayani humo ili kukuza uchumi wa Wananchi

Zaidi, soma https://jamii.app/WasiolimaBiasharaRumande-LDW
MWANZA: SERIKALI YALIFUNGA KANISA LA ZUMARIDI

- DC wa Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi amepiga marufuku Ibada zinazoendeshwa na Kiongozi wa Kanisa la Mfalme Zumaridi, Diana Bundala hadi watakapojiridhisha kuwa ibada hazikinzani na Sheria za Nchi

Zaidi, soma https://jamii.app/KanisaMfalmeZumaridiMarufuku
MIKOA 3 KUTOFANYA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

- Wizara ya TAMISEMI imebainisha kuwa CCM imepita bila kupingwa katika Mikoa ya Katavi, Tanga na Ruvuma

- Imesema katika Mikoa hiyo hakuna Kitongoji, Mtaa wala Kijiji kitakachokuwa na Uchaguzi

Zaidi, soma https://jamii.app/CCMMikoa3Yashinda-SMitaa
TETESI: KOCHA MAURICIO POCHETTINO MBIONI KUFUKUZWA

- Yadaiwa la kujiuliza juu ya Kocha huyo wa Tottenham Hotspurs ni 'Lini ataondoka?' sio 'Je, ataondoka?'

- Inadaiwa wanaoweza kumrithi ni Eddie Howe (Bournemouth), Julian Nagelsmann (RB Leipzig) au Carlo Ancelotti (Napoli)
MWANZA: WEZI WAMUUA MTOTO WA MIAKA 7 NA KUIBA MIFUGO ZAIDI YA 50

- Mtoto Andrea Sekei amenyongwa kwa kamba ya viatu, amekatwa koromeo na kupigwa na kitu kizito usoni na Watu ambao hawajafahamika.

- Alikuwa akichunga mifugo eneo la Mahiriga, Magu

Soma https://jamii.app/MtotoAuwawaAkichunga

#JFLeo
DAR: MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE ALAZWA HOSPITALI

- Ameshindwa kufika Mahakamani kutokana na kulazwa Hospitali ya Aga Khan tangu Novemba 17

- Ni miongoni mwa viongozi 9 wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi inayoendelea leo

Zaidi, soma https://jamii.app/MboweAlazwaNov17
RIPOTI: WANAOJIHUSISHA NA KAZI ZA USAFI VYOONI WAKO HATARINI ZAIDI KUPOTEZA MAISHA

> Siku ya Choo Duniani huadhimishwa Novemba 19 kila mwaka na Kati ya mwaka 2017 na 2018, kwa Nchini India imethibitika kuwa watu 3 wanaofanya uzoaji wa taka za chooni hufariki kila baada ya siku 5, huku kwa mwezi watu 18 na kwa mwaka ni watu 216

Zaidi, soma https://jamii.app/HatariAfyaWasafishaVyoo
MEYA WA JIJI LA ARUSHA (CHADEMA) KALISTI LAZARO AJIUNGA CCM

- Amesema ni baada ya kupitia wakati mgumu kutoka kwa uongozi wa chama chake

- Amedai, mara kwa mara amepokea barua za onyo za kumtaka kutotoa ushirikiano kwa Viongozi wa Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/MeyaArushaKalistiAjiungaCCM
LUIS ENRIQUE ATEULIWA TENA KUINOA TIMU YA TAIFA YA UHISPANIA

- Ni Miezi mitano tangu ajiengue kuifundisha timu hiyo ya Soka ya Wanaume kutokana na sababu binafsi

- Alijiuzulu wakati mtoto wake mdogo aliyefariki mwezi Agosti alipokuwa akiumwa Saratani ya Mifupa
KINONDONI, DAR: WAKANDARASI WAWILI RAIA WA CHINA WAKAMATWA KWA AMRI YA DC

- DC Daniel Chongolo amewakamata Wakandarasi hao wa Kampuni ya CRJE kwa kushindwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Taka kilichopo Mabwepande

Zaidi, soma https://jamii.app/WakandarasiCRJEMbaroni-KNDN
JE, WAJUA RAIS HAWEZI KUSHTAKIWA?

> Ibara ya 46.-(1) ya #Katiba ya Tanzania imeeleza kuwa wakati wote ambao Rais atakapokuwa madarakani, itakuwa ni marufuku kumshtaki au kuendesha mashtaka ya aina yoyote juu yake kwa kosa lolote la jinai

#UmuhimuKatiba
Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa JamiiForums tunapenda kuwatakia Wanaume wote Kheri ya Siku ya Wanaume Duniani