JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UFARANSA: GAVANA WA KINSHASA ADAIWA KUSHAMBULIWA NA RAIA WA CONGO

- Gentiny Ngobila Mbaka anadaiwa kushambuliwa na raia wa Congo wanaoishi Ufaransa alipokwenda dukani kufanya manunuzi

- Sababu ya raia hao kufanya hivyo haijafahamika bado

Zaidi, soma https://jamii.app/GavanaKinshasaKipigo-FR
MICHEZO: Baada ya Taifa Stars kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Equtorial Guinea, leo inashuka tena dimbani kupambana na Libya kuwania kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2021

- Mchezo huo unaotarajiwa kuanza majira ya saa Nne Kamili Usiku (Saa za Afrika Mashariki) utachezwa katika dimba la Olympique Mustapha Ben Jannet Monastir nchini Tunisia
MPYA: MAURICIO POCHETTINO AFUNGASHIWA VIRAGO

- Klabu ya Tottenham Hotspurs imemfuta kazi Kocha wake huyo baada ya kuiongoza timu hiyo kwa miaka mitano

- Taarifa ya timu inasema matokeo ya mwishoni kwa ligi za ndani msimu uliopita na matokeo ya msimu huu si ya kuridhisha

Zaidi, soma https://jamii.app/PochettinoAfukuzwaSpurs
MICHEZO: Timu ya Taifa Stars imeenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa goli 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Libya

- Nahodha wa Stars, Mbwana Samatta ndiye aliyefunga goli hilo kwa mkwaju wa penati baada ya Simon Msuva kuchezewa rafu katika eneo la hatari
UPDATES: Timu ya Taifa ya Libya inapata goli la kusawazisha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 67 dhidi ya Taifa Stars na kufanya matokeo kuwa goli 1-1. Mpira unaendelea...
KUFUZU AFCON 2021: Timu ya Libya inapata goli lake la pili katika dakika ya 81 katika mchezo dhidi ya Taifa Stars na kufanya matokeo kuwa 2-1

- Taifa Stars ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli katika mchezo huo unaoendelea hivi sasa
KUFUZU AFCON 2021: TAIFA STARS YAPOTEZA DHIDI YA LIBYA

- Taifa Stars imefungwa goli 2-1 na Libya katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Kundi J uliochezwa Tunisia wa kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika 2021

- Stars ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa Nahodha Mbwana Samatta lakini Libya iliweza kusawazisha na hatimaye kupata goli la pili ambalo ni la ushindi
MICHEZO: JOSE MOURINHO AJIANDAA KUMRITHI POCHETTINO KATIKA KLABU YA TOTTENHAM

- Taarifa zinaeleza kuwa wawakilishi wa Jose Mourinho na wale wa Klabu ya Tottenham wanatarajiwa kufikia makubaliano mchana wa siku ya leo

Zaidi, soma > https://jamii.app/MourinhoSpurs
RC WA KILIMANJARO AMUONYA MBUNGE WA SIHA KUACHA UCHONGANISHI

- Dkt. Anna Mghwira amemtaka Mbunge Dkt. Godwin Mollel kuacha uchonganishi baina ya Watumishi wa Halmashauri, Madiwani na Wananchi, badala yake awe kiunganishi ili kuleta maendeleo

Zaidi, soma https://jamii.app/RCKili-MbungeSiha
RAIS ANAWEZA KUTOA MSAMAHA KWA MSHTAKIWA

> Rais wa Tanzania amepewa mamlaka ya kutoa msamaha kwa Mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya Mahakama kwa kosa lolote, hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 45.-(1) ya #Katiba ya Tanzania

#UmuhimuKatiba
MOURINHO AMRITHI POCHETTINO TOTTENHAM

- Jose Mourinho amechaguliwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham Hotspurs ya England hadi mwisho wa msimu 2023

- Kocha huyo wa zamani wa Klabu za Manchester United na Chelsea za England pia anachukua nafasi ya Mauricio Pochettino

Zaidi, soma https://jamii.app/PochettinoAfukuzwaSpurs
RAIS MAGUFULI AMTAKA MKURUGENZI WA NIDA KWENDA MOROGORO LEO

- Amemtaka kwenda kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi wakati wa kujiandikisha ili kupata Vitambulisho vya Taifa

- Pia, ametaka huduma hiyo iende kila Wilaya, kwani haiwezekani watu kutoka Wilayani kwenda Mjini la sivyo NIDA iwape Wananchi hela ya ‘guest’

Zaidi, soma https://jamii.app/MkurugenziNIDAvsMagufuli
MAGUFULI: UKIONA BEI YA MAHINDI IKO JUU, NENDA KALIME YAKO

- Amesema bei ya mahindi inapopanda na wachache kulalamika, Wakulima wanashangilia

- Amesema wakati wa kumpangia bei Mkulima umepita na katika kipindi chake hatampangia Mkulima bei

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliBeiWakulima
KAZI HUZAA UTAJIRI, KATIBA INATAKA WATU WAJITUME

- Ibara ya 25- (1): Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii, ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu

- Kila mtu anao wajibu wa kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazi halali

#UmuhimuKatiba
KIGOMA: MWALIMU WA SHULE YA MSINGI MBARONI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

- Zakaria Richard(30) anatuhumiwa kumbaka na kumlawiti Mwanafunzi(10) wa Darasa la 5

- Mwanafunzi huyo alikabidhiwa na wazazi wake kwa mwalimu huyo afundishwe Masomo ya Ziada

Zaidi, aoma https://jamii.app/MwalimuMbaroniUbakaji-KGM
CHAD: VIONGOZI WA WAASI NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI WAKAMATWA

- Jen. Abdoulaye Miskine na wenzake watatu wanadaiwa kuingia Chad kupitia Mji wa Tissi

- Maswali mengi yameibuka kutoka kwa wadau yakihoji iwapo walikuwa wanatafuta hifadhi Chad

Zaidi, soma https://jamii.app/WaasiAfrikaKatiMbaroni
SIKU YA MTOTO DUNIANI: NI MUDA WA WATOTO KUPATA HAKI ZAO

- Siku ya Watoto Duniani ilianzishwa mnamo 1954 na huadhimishwa Novemba 20 kila mwaka kukuza Umoja wa Kimataifa, Ufahamu wa masuala mbalimbali kati ya watoto Ulimwenguni kote, na kuboresha Ustawi wa Watoto
WABUNGE WA CHADEMA WALIOKIUKA MASHARTI YA DHAMANA WAONYWA NA MAHAKAMA

- Wabunge hao ni Peter Msigwa(Iringa Mjini), John Heche(Tarime Vijijini), Halima Mdee(Kawe) na Ester Bulaya(Bunda)

- Mahakama imesema kuwafutia dhamana ingekuwa hatua kali

Zaidi, soma https://jamii.app/WabungeCDMWaonywa-Kisutu
KAZI ZA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KWA MUJIBU WA KATIBA

- Atahakikisha matumizi ya fedha zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali yameidhinishwa

- Atahakikisha fedha zote zimetumiwa kama ilivyokusudiwa

#UmuhimuKatiba
MDAU: WANAOBUSU WATOTO WA WENZAO MIDOMONI WANANIKERA SANA

- Amesema, “Unakuta mtu kaja kutembelea mtoto wako au kamkuta umemshika anamchukua na kuanza kumpiga mabusu ya mdomoni. Huu ni uchafu sana, mimi sipendi kabisa tabia hiyo”

Kujadili, tembelea https://jamii.app/KissingAnothersKid