JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KANUNI YA KUWABANA WAMILIKI WA NYUMBA KUPELEKWA BUNGENI

- Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema Serikali inatarajia kupeleka Kanuni Bungeni ili kuwabana Wamiliki wa nyumba wanaowalazimisha Wapangaji kulipa kodi kwa muda wa miezi 6 hadi 12

Zaidi, soma https://jamii.app/KanuniKuwabanaWapangishaji
KASI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI MKOANI TANGA YAPUNGUA

> Kasi ya maambukizi mapya ya ugonjwa huo imeshuka kutoka asilimia 5 ya 2017 hadi asilimia 2.2 Julai 2019

> Kasi ya watu kujitokeza kupima kwa hiari imeongezeka kutoka watu 51,344 mwaka 2017 hadi kufikia watu 66,308 mwaka 2018

Soma - https://jamii.app/KupunguaKasiMaambukiziVVU
KESI YA KABENDERA: HAKIMU ATEULIWA KUWA JAJI. KESI YAAHIRISHWA

- Kesi inayomkabili Erick Kabendera imeahirishwa ktk Mahakama ya Kisutu hadi Novemba 20, 2019

- Hakimu aliyekuwa akiisikiliza kesi, Augustine Rwizile amekuwa Jaji wa Mahakama Kuu

Soma https://jamii.app/Hakimu-JajiKesiKabendera
MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA UHALIFU YAMUHUKUMU BOSCO NTAGANDA MIAKA 30 JELA

- Kiongozi wa zamani wa Waasi wa Congo amehukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu

- Alipatikana na hatia katika makosa 18 yakiwemo ubakaji na utumwa wa ngono

Zaidi, soma https://jamii.app/NtagandaMiaka30Jela-DRC
MAAMBUKIZI MAPYA YA TB YAPUNGUA KWA ASILIMIA 4.6 TANZANIA

> Tanzania ni miongoni mwa nchi 7 duniani ambazo zimefikia malengo ya mkakati wa kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kufikia mwaka 2020 na ambapo mwaka 2018 maambukizi mapya yalipungua kwa 4.6

> Vifo vinavyotokana na ugonjwa huo vimepungua kwa 27% kutoka vifo 55,000 kwa 2015 hadi 39,000 kwa 2018

Soma - https://jamii.app/KupunguaMaambukiziMapyaTB
Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Zaidi, soma https://jamii.app/CHADEMAYajotoaUchaguzi2019
KATIBA INAWEKA USAWA KWA WOTE

> #Katiba ya Tanzania inaeleza kuwa Raia yeyote hatakuwa na haki, hadhi au cheo maalum kwa misingi ya Nasaba, Jadi au Urithi

> #Katiba inapambanua, ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo kwa misingi ya upendeleo

#UmuhimuKatiba
BOLIVIA: WAANDAMANAJI WAMPAKA RANGI NA KUMKATA NYWELE MEYA

- Patricia Acre amepakwa rangi nyekundu, kukatwa nywele na kutembezwa bila viatu na Waandamanaji wa Upinzani

- Wanamshutumu kwa baadhi ya mambo yakiwemo kuhusika na vifo vya wenzao

Zaidi, soma https://jamii.app/MeyaAkatwaNyweleMaandamano-BLV
UINGEREZA: VYAMA VITATU VYA UPINZANI VYAUNGANA KUPIGANIA NCHI IBAKI EU

- Vyama vya Liberal Democrats, Walinzi wa Mazingira na Plaid Cymru vimekubaliana kushirikiana katika Uchaguzi wa Desemba 12 ili kuongeza idadi ya Wawakilishi Bungeni

Zaidi, soma https://jamii.app/VyamaVyaunganaBrexit
NCHI 18 BARANI AFRIKA ZAATHIRIWA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

> Kwa mujibu wa Oxfam, Zaidi ya watu milioni 52 katika nchi 18 Barani Afrika wanakabiliwa na baa kubwa la njaa, sababu ikiwa hali mbaya ya hewa, umasikini na migogoro

> Hali hii ni mbaya kwa nchi kama Angola, Malawi, Msumbiji, Madagascar, Namibia na Zimbabwe, Mashariki na eneo la Pembe ya Afrika hasa Ethiopia, Kenya na Somalia

Soma - https://jamii.app/JangaUkameAfrika
ATCL: HATUAJIRI WANAWAKE KUONESHA SURA

- Imesema haichagui Wanawake kwa ajili ya kuwapeleka kuonesha uzuri bali kuna vigezo

- Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima jana alidai Wahudumu wa Ndege za ATCL hawana mvuto kwa wateja

Zaidi, soma https://jamii.app/MbungeVsATCL-Wahudumu
MAREKANI: JAJI AMTAKA RAIS TRUMP ARUDISHE ZAIDI TSH. BILIONI 4 ALIZOTUMIA KWENYE KAMPENI

> Inadaiwa alichukua Fedha hizo kutoka katika Mfuko wa Misaada wa 'Trump Foundation' na kuzitumia katika kampeni zake kwenye uchaguzi wa mwaka 2016

> Mahakama yasema matumizi hayo yalikuwa Kinyume cha Sheria

Soma - https://jamii.app/FedhaKampeniTrump
MWITA WAITARA: UKINYIMWA HAKI YAKO NENDA MAHAKAMANI NA SIO KUSUSIA UCHAGUZI NA KUSHAWISHI FUJO

> Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara amevitaka Vyama vya Siasa vya Upinzani viache kuchukua maamuzi ya ajabu ya kususia uchaguzi badala yake vidai haki kwa njia sahihi

> Amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kujipanga vyema ili kudhibiti watakaofanya fujo

Soma - https://jamii.app/WaitaraUpinzaniUchaguzi
NJOMBE: AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi imemhukumu kifungo cha maisha Addo Aron Nziku (26) baada ya kukutwa na hatia ya kubaka mwanafunzi katika Kijiji cha Kitulila

> Mtuhumiwa anadaiwa kumwingilia mwanafunzi huyo zaidi ya mara tatu kabla ya mtoto kumweleza bibi yake juu ya maswahibu yanayompata

Soma - https://jamii.app/KifungoMaishaUbakaji
MWANZA: MKURUNGENZI ANUSURIKA KUPIGWA NA MACHINGA

- Machinga wa pembezoni mwa barabara ya Pamba na Mtaa wa Sokoni walitaka kumshambulia Mkurugenzi wa Jiji, Kiomoni Kibamba wakati akitoa maelekezo ya kuwataka kuondoka katika maeneo walipo

Zaidi, soma https://jamii.app/MkurugenziWamachinga-Mwanza
BURKINA FASO YAANZA MAOMBOLEZO YA SIKU 3 KITAIFA BAADA YA KUUAWA KWA WATU 38

> Rais wa nchi hiyo, Roch Marc Christian Kabore amesema shambulio hilo dhidi ya msafara wa magari ya wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Semafo, kama uhalifu wa hali ya juu unaolenga kuzua hofu kwa wananchi na kuhatarisha Demokrasia

Soma - https://jamii.app/3DaysNationalMourning
BURUNDI: KIONGOZI WA UPINZANI ADAI SERIKALI INAPANGA NJAMA ZA KUMUUA

- Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani cha CNL, Agathon Rwasa amelalamikia kuhusu kile alichosema ni njama za Serikali kumzushia uasi kama njia ya kumuua au kumtia mbaroni

Zaidi, soma https://jamii.app/RwasaVsSerikali-Burundi
UJERUMANI: MLIPUKO NDANI YA MGODI WAZUIA TAKRIBAN WATU 30 ARDHINI

- Mlipuko uliotokea katika machimbo ya madini huko Teutschenthal, umejeruhi pia watu wawili

- Uokoaji unaendelea huku ikielezwa waliokwama wapo salama ndani ya chumba kimoja

Zaidi, soma https://jamii.app/Explosion30TrapsMine