JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Kocha Mkuu wa timu ya Taifa 'TaifaStars', Ettiene Ndairagije ametaja Kikosi cha Wachezaji 27 kitakachojiandaa na michezo kufuzu AFCON 2021

- Taifa Stars inakabiliwa na michezo miwili dhidi ya Equatorial Guinea na Libya katika michuano hiyo ya Mataifa ya Afrika
MBATIA: WAGOMBEA WOTE WA NCCR KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA JIMBONI VUNJO WAMEENGULIWA

- Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema mchezo uliofanywa ni hatari kwa nchi na tayari ameiandikia Serikali barua ya malalamiko

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziMitaaNCCR-Vunjo
BASHE: SERIKALI HAITAINGILIA KUPANGA BEI ZA PAMBA MSIMU UJAO

- Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuelekea msimu ujao wa Pamba, Serikali itajitahidi kupunguza gharama, kutopanga bei na kujitajitahidi kumlinda mkulima asipate hasara

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliKutopangaBeiPamba
ZAHERA: NIMEONDOLEWA YANGA KWA KUKATAA KUFANYA KAZI NA CHARLES MKWASA

- Mwinyi Zahera amedai viongozi wa Yanga walimuhakikishia kuendelea kuwa Kocha hata kama angefungwa Misri

- Amedai, ameondolewa baada ya kumkataa Mkwasa kama Msaidizi wake

Zaidi, soma https://jamii.app/ZaheraSababuKuondoka
UTURUKI YADAI KUMKAMATA DADA WA KIONGOZI WA ISLAMIC STATE ALIYEUAWA

- Rasmiya Awad (65) anadaiwa kukamatwa huko Aleppo karibu na mji uliodhibitiwa na Uturuki, Azaz

- Ni dada wa aliyekuwa Kiongozi wa Islamic State (IS), Abu Bakr al-Baghdadi

Zaidi, soma https://jamii.app/DadaKiongoziISMbaroni
MAREKANI: ALIYEFUKUZWA KAZI KWA KUMUONESHA 'KIDOLE CHA KATI' TRUMP APEWA OFISI YA UMMA

- Juli Briskman aliyemuonesha 'Kidole cha Kati' Rais Trump Oktoba 2017, amechaguliwa kuwa Mwakilishi wa Wilaya ya Algonkian katika Kaunti ya Loudoun, Virginia

Zaidi, soma https://jamii.app/BriskmanAwaMwakilishiWilaya
MBUNGE WA HONK KONG ACHOMWA KISU WAKATI WA KAMPENI

> Mmoja wa waandamanaji anayeipinga Serikali amemchoma kisu na kumjeruhi Mbunge wa Hong Kong, Junius Ho wakati akifanya kampeni ya uchaguzi hii leo

> Hata hivyo, Mbunge huyo anadaiwa kupanga tukio hilo kwa maslahi ya kisiasa

Soma https://jamii.app/BeijingLawmakerStabbed
BUNGENI: Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson ameagiza Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Peter Msigwa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuthibitisha kauli aliyoitoa leo kuwa kura ziliibiwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015

Zaidi, soma https://jamii.app/Tulia-MsigwaKamatiMaadili
WAFANYAKAZI WA ZAMANI WA TWITTER WASHTAKIWA KWA KUICHUNGUZA MAREKANI

- Wafanyakazi wawili wanaodaiwa kutumiwa na Saudi Arabia kuichunguza Marekani, wameshtakiwa wakishutumiwa kuwasaidia Maafisa wa Saudi Arabia kupata taarifa binafsi za watumiaji wa Mtandao huo wakiwemo wakosoaji

Zaidi, soma https://jamii.app/USAvsSaudi-Twitter
WALIOTUMIA JINA LA MAMA JANETH MAGUFULI KUTAPELI WAHUKUMIWA KULIPA FAINI

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu watu wanne kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5 kila mmoja baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kutumia jina la mke wa Rais Magufuli kutapeli Tsh. Milioni 4.4

> Mbali na faini hiyo, Mahakama imetaifisha gari aina ya Toyota Raum pamoja na simu 8 vilivyotumika katika utapeli huo

Soma - https://jamii.app/UtapeliJinaMkeRais
UJERUMANI: SHIRIKA LA NDEGE LA LUFTHANSA LAFUTA SAFARI TAKRIBAN 1,300

- Limefuta baadhi ya safari za leo na kesho kutokana na mgomo wa Chama cha Wahudumu wa Ndege

- Wahudumu hao wamegoma wakipigania mishahara na hadhi ya kisheria ya chama

Zaidi, soma https://jamii.app/LufthansaYafutaSafari-UJR
PROF. LIPUMBA AMUOMBA RAIS MAGUFULI KUINGILIA KATI MGOGORO KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

> Amesema, Kitendo cha kuwanyima fomu wagombea wa upinzani sio tu hakina tija kwenye ukuaji wa Demokrasia, pia ni matumizi mabaya ya Pesa za Umma

> Asema, huwezi ukafanya semina, kuchapisha nyaraka mbalimbali huku ukijua hakuna uchaguzi bali wagombea wanapita bila kupingwa

Soma - https://jamii.app/LipumbaUchaguziSMitaa
CHINA YAZINDUA RASMI UTAFITI NA UENDELEZAJI WA 6G

- Imeanza kuendeleza mfumo wa kusafirisha mawimbi ya mawasiliano ya simu wa 6G ikiwa ni hatua ya kuachana na 5G

- Imesema, Ulimwenguni ujuzi wa teknolojia hiyo upo katika hatua za majaribio

Zaidi, soma https://jamii.app/ChinaKutafiti6G
KUFANYA KAZI NA KUINGIZA KIPATO NI HAKI YAKO
-
Katiba inatoa haki ya kufanya kazi, ikijumuisha haki ya kupata ujira wa haki na halali. #Katiba inatoa nafasi ya Mtanzania kudai haki yake kama anafanya kazi halali lakini halipwi au hapati stahiki yake
-
Fedha za mishahara na posho za watumishi wa Serikali ni pamoja na fedha za malipo ya uzeeni na kiinua mgongo kwa wanaostahili. Malipo haya yatatolewa na Mfuko Mkuu wa Hazina
-
Je, Wastaafu wanaolalamikia kutolipwa stahiki hizi za kikatiba wachukue hatua gani?

#UmuhimuKatiba #JFLeo
SERIKALI YATAJA MIKOA INAYOONGOZA KWA WATU WAKE KUVUTA BANGI

> Serikali imesema matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi bado ni tatizo nchini, huku yakishika kasi katika Mikoa ya Mara, Tanga, Morogoro, Arusha, Kagera na Ruvuma

> Jumla ya vituo sita vilivyopo Dar, Mwanza, Mbeya na Dodoma viliendelea kutoa huduma na hadi mwaka 2018 zaidi ya watumiaji 8,000 walipatiwa huduma za Methadone

Soma - https://jamii.app/MikoaVinaraUvutajiBangi
UGANDA NA KENYA ZAKUBALIANA KUSHIRIKIANA KISIWA CHA MIGINGO

- Zimekubali kushikiriana Kisiwa cha Migingo huku Kenya ikiendelea kusema Kisiwa hicho kipo kwake

- Wamesaini Mkataba wa Makubaliano na Uganda kuruhusu Wavuvi kutumia Kisiwa hicho

Zaidi, soma https://jamii.app/KenyaUgandaShareMigingo
KITETO, MANYARA: MWENYEKITI WA MAZINGIRA AUAWA AKITATUA MGOGORO WA ARDHI

- Engerusi Mikonde (59) ameuawa katika shamba moja akiwa kwenye harakati za kutatua mgogoro wa ardhi

- Alishambuliwa kwa marungu na mapanga akiwa na Kamati ya Mazingira

Zaidi, soma https://jamii.app/AuawaAkitatuMgogoroArdhi
BURKINA FASO: WATU 37 WAANGAMIA KATIKA SHAMBULIO LA WAFANYAKAZI WA MGODI

> Shambulio la kushtukiza lililolenga msafara wa wafanyakazi wa Mgodi wa Samafo, limesababisha vifo vya watu 37 waliokuwa kwenye mabasi 5

> Watu waliokuwa na bunduki walishambulia msafara uliokuwa umewabeba wafanyakazi na Wahandisi

Zaidi, soma https://jamii.app/GunmenAmbushMiningConvoy
SERIKALI PEKEE INA MAMLAKA YA KUANZISHA JESHI

> Kwa mujibu wa #Katiba ni marufuku kwa mtu, shirika au kikundi kuunda au kuweka Jeshi lolote. Serikali pekee ndiyo yenye uwezo wa kuunda na kuweka Majeshi mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na raia

#UmuhimuKatiba