JamiiForums
āœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JAJI MKUU KENYA: NAPANGIWA NJAMA ZA KUONDOLEWA MADARAKANI

- David Maraga ametishia kujiuzulu kufuatia kukatwa kwa bajeti ya Mahakama akidai inalenga kuidhibiti Mahakama

- Amedai ni njama za Serikali kumuondoa madarakani kabla ya Desemba 31

Soma https://jamii.app/MalalamikoJajiMkuu-KE
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Prof. Assad akiondoka baada ya kukabidhi ofisi kwa CAG mpya, Charles Kichere leo jijini Dar

> Prof. Assad amemaliza kipindi chake kimoja akihudumu kama CAG na ameondoka huku ukiibuka mjadala mkali juu ya kuondoka kwake
MKWASSA KUINOA YANGA

> Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amemtangaza Charles Boniface Mkwassa kuwa kocha wa muda wa Yanga akichukua nafasi ya Mwinyi Zahera kwa muda wa wiki mbili

Zaidi, soma https://jamii.app/MkwasaKochaYanga
MAHAKAMA YAIGOMEA SERIKALI

> Mahakama ya Kisutu imetupilia mbali maombi yaliyotolewa na upande wa Serikali kutaka kuwaondolea shtaka la Utakatishaji Fedha aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange

Zaidi, soma https://jamii.app/NyangeAvevaDhamana
MAREKANI YAWAWEKEA VIKWAZO WATU 9 WALIO KARIBU NA KIONGOZI WA IRAN

> Marekani imesema mali za watu hao zilizopo nchini Marekani zitazuiwa pamoja na hatua nyingine kuchukuliwa kutokana na tuhuma dhidi yao za kuhusika na mambo mabaya katika Utawala wa Iran

> Miongoni mwao, yupo Mkuu wa Mahakama ya Iran na mtoto wa kiume wa Kiongozi wa Iran

Soma - https://jamii.app/MarekaniVikwazoIran
IFAHAMU SERA YA CHINA YA WATU KUZAA MTOTO MMOJA TU

> Ili kukabiliana na ongezeko la idadi ya watu Serikali ilianza Tume madhubuti ya kusimamia upangaji wa uzazi mnamo 1971 na kupelekea sera ya kuzaa mtoto mmoja kuanzishwa mnamo 1980 na ilisababisha idadi ya watu kupungua hadi kufikia milioni 250 kutoka milioni 800 waliokuwepo mwaka 1970

> Watu wengi waliipinga Sera hii wakisema ilikuwa ikiwanyanyasa wanawake kwa kuwalazimisha kutumia njia za uzazi wa mpango au kulazimishwa kutoa mimba pale wanapopata ujauzito na pia ilisababisha watoto wengi kukosa ndugu wa kuzaliwa kutoka familia moja

> Mnamo Januari 2016 China iliamua kubadilisha Sera hiyo ya kuwa na mtoto mmoja na kuruhusu wanandoa kuzaa watoto wawili

Fahamu zaidi kupitia - https://jamii.app/China1ChildPolicy
#JFHistoria
IRAQ: HUDUMA YA INTANETI IMEZIMWA USIKU WA KUAMKIA LEO SABABU YA MACHAFUKO

> Huduma ya intaneti katika Mji wa Baghdad na sehemu kubwa ya nchi ya Iraq imekatwa kufuatia machafuko ndani ya nchi hiyo yanayotokana na maandamano ya kuipinga Serikali

> Taarifa zinasema kiwango cha kuunganishwa na intaneti kitaifa kimepungua na kufikia chini ya 19% ya viwango vya kawaida

Soma - https://jamii.app/InternetBlockageIraq
WAZIRI WA FEDHA: MATUMIZI YA SERIKALI KUONGEZEKA KWENYE BAJETI IJAYO

- Dkt. Philip Mpango amesema matumizi yanakadiriwa kuongezeka kutoka Tsh. Trilioni 33.105 hadi Tsh. Trilioni 34.360

- Matumizi ya kawaida yanakadiriwa kuongezeka kwa 4.7%

Zaidi, soma https://jamii.app/MatumiziSerikaliKuongezeka
RIPOTI INAYOHUSU MASUALA YA UHURU KATIKA MTANDAO 2019 YAZINDULIWA

- Katika Mataifa 65 yaliyohusika katika utafiti imeelezwa kuwa Serikali na Wanasiasa katika Mataifa 38 huwalipa watu ili wapotoshe na kuharibu mijadala katika mitandao

- Mataifa mbalimbali Duniani yametajwa katika ripoti hiyo kuwa yamekuwa yakitumia Mitandao ya Kijamii kuiba kura wakati wa Uchaguzi

Soma > https://jamii.app/FreedomOnTheNet
USIKU WA UEFA: Timu zimeenda mapumziko huku Liverpool iliyo katika Uwanja wa Anfield ikiwa imefungana goli 1-1 na Genk. Goli la Genk limefungwa na Mtanzania, Mbwana Samatta
-
Katika mchezo mwingine, Klabu ya Chelsea ipo nyuma kwa goli 3-1 ikiwa inapambana na Klabu ya Ajax ya Uholanzi
MATOKEO: Michezo ya Klabu Bingwa Ulaya iliyomalizika usiku huu katika Viwanja mbalimbali Barani humo
NIGERIA: MAMIA WAOKOLEWA WAKIWA WAMEFUNGWA MINYORORO

- Polisi imewaokoa watu 259 kutoka katika kituo kisichokubalika kisheria kilichopo Msikitini

- Inadaiwa Wazazi hupeleka watoto wanaowasumbua kitabia ktk vituo hivyo vya kurekebisha tabia

Zaidi, soma https://jamii.app/WaokolewaMsikitiniMinyororo-NGR
TMA: UTABIRI WA HALI YA HEWA HATARISHI WA SIKU 5

- Novemba 06, maeneo ya Pwani, Dar, Tanga na Zanzibar, yanatarajiwa kukumbwa na mvua kubwa

- Novemba 09 angalizo kama hilo limetolewa kwa Morogoro, Lindi, Mtwara, Pwani, Dar, Tanga na Zanzibar

Zaidi, soma https://jamii.app/UtabiriHaliHewaSiku5-Nov2019
DENI LA TAIFA LAONGEZEKA KWA TSH. TRILIONI 3 KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA

> Serikali imesema hadi kufikia Agosti 2019, Deni la Taifa lilifikia Tsh. Trilioni 52.303 kutoka Tsh. Trilioni 49.283 Agosti 2018 ambapo kiwango hicho ni sawa na ongezeko la Tsh. Trilioni 3

> Deni la Ndani lilikuwa Tsh. Trilioni 14.075 na Deni la Nje Tsh. Trilioni 38.227 na ongezeko hilo limechangiwa na kupokewa kwa mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo

Soma - https://jamii.app/OngezekoDeniTaifa
UTETEZI KESI CHADEMA: MBOWE AKANA KUWAPO KWENYE MAANDAMANO YALIYOMUUA AKWILINA

> M/Kiti Taifa (CHADEMA), Freeman Mbowe amedai hakushiriki na hakuwapo kwenye maandamano ya wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakielekea kwenye Ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni

> Yeye na wenzake 8 wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai

Soma https://jamii.app/UteteziKesiMbowe
NIGERIA: WANAFUNZI 13 WAPOTEZA MAISHA KUFUATIA VURUGU KATI YA WANAFUNZI

> Watu 13 wamefariki kutokana na vurugu za mapigano zilizotokea baina ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kogi

> Mapigano hayo yalitokea baina ya makundi mawili ya kiimani na uchunguzi kuhusiana na na tukio hilo umeanza

Soma - https://jamii.app/CultMembersKillings
YEMEN: SERIKALI NA WANAHARAKATI WANAOTAKA KUJITENGA WATIA SAINI MKATABA WA AMANI

> Mkataba huo uliosainiwa jana utawezesha kurudi kwa hali ya utulivu Kusini mwa Yemen na pia utawezesha kuundwa kwa Serikali mpya

> Ulitiwa saini mbele ya wakuu kutoka nchi za Saudi Arabia, Falme za Kirabu na Rais wa Yemen

Soma - https://jamii.app/YemenPeacefulDeal
KUPATA HABARI NI HAKI YAKO KAMA ZILIVYO HAKI NYINGINE
-
Kifungu cha 18 cha #Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 inampa Mtu haki na uhuru wa kujieleza, kutoa mawazo, kutafuta, kupata na kueneza habari bila kujali mipaka ya Nchi
-
Katiba inampa Mtu haki ya kuwasiliana bila kubughudhiwa. Aidha, kwa mujibu wa Katiba Mtanzania ana haki ya kuhabarishwa masuala yote muhimu yahusuyo maendeleo yake na jamii kwa ujumla

#UmuhimuKatiba