JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Msanii Idris Sultan amefika Kituo cha Kikuu cha Polisi (Central) muda wa saa 5 asubuhi kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda

> Anaendelea kushikiliwa kituoni kwa mahojiano

> Inadaiwa anahojiwa kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 15 na 16

Zaidi, soma https://jamii.app/IdrisAhojiwaPolisi
KENYA: Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewapongeza Wakenya kwa Kuonesha Mubashara Vikao vya Kamati vya Bunge

- Amesema “Nawapongeza kwa uzinduzi, kwamba sasa vikao vya Kamati mbalimbali vitapeperushwa mubashara (Live)”

Zaidi, soma https://jamii.app/NdugaiApongezaBungeKE
MTWARA: WATOTO 11 WA KIUME HAWAJULIKANI WALIPO

- Wametoweka kwa zaidi ya siku 10 ktk Kijiji cha Mtimbwilimbwi Halmashauri ya Nanyamba, na bado haijulikani walipo

- Mkuu wa Wilaya asema, Serikali ina taarifa na juhudi za kuwatafuta zinaendelea

Zaidi, aoma https://jamii.app/Watoto10WapoteaMtwara
BASHE: KAMA SIO MKULIMA ASIONGOZE CHAMA CHA USHIRIKA

- Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amepiga marufuku watu wasiokuwa Wakulima kuongoza Vyama vya Ushirika kwa maelezo kuwa hawana msaada wowote zaidi ya kugeuka madalali

Zaidi, soma https://jamii.app/MkulimaKiongoziAMCOS
FACEBOOK YAFUNGA AKAUNTI ZILIZOKUWA ZIKIINGILIA NCHI ZA AFRIKA

- Imeondoa akaunti kubwa tatu za Urusi, kurasa na makundi bandia yanayowahadaa Watumiaji

- Baadhi ya nchi zilizolengwa ni Madagascar, Afrika ya Kati, Msumbiji, Congo na Libya

Zaidi, soma https://jamii.app/AkauntiFBZilizoingiliaAfrika
RPC MTWARA: WATOTO WALIOPOTEA WALISHAWAHI KUKAMATWA KWA UHALIFU

- Amesema, jumla ya watoto 11 waliotoweka huenda wakawa wameenda nchini Msumbiji

- Amesema, waliwahi kukamatwa na Maafisa wa Usalama Msumbiji kwa uhalifu na kurejeshwa Nchini

Zaidi, soma https://jamii.app/Watoto10WapoteaMtwara
MARA: AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO

Maiga Maginga (18), amehukumiwa kifungo cha maisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Wilaya ya Serengeti baada ya kukiri kumlawiti mtoto wa miaka minne

Zaidi, soma https://jamii.app/KifungoMaishaUlawiti
JE, UNAFAHAMU NINI MAANA YA KATIBA NA UMUHIMU WAKE?

> Katiba ni mpangilio wa sheria zilizoandikwa au zisizoandikwa zinazotumika kuongoza nchi, taasisi au kikundi

> Nchi zote zinahitaji katiba ili ziweze kujiendesha vizuri. Nchi isiyo na katiba inaweza kuingia kwenye machafuko

Zaidi, soma > https://jamii.app/UmuhimuKatiba

#UmuhimuKatiba
MAHUSIANO: NJIA SAHIHI ZA KUACHANA NA MPENZI WAKO KWA AMANI

- Mdau kutoka JamiiForums anasema moja ya njia sahihi ya kuvunja uhusiano ni kuwa na uhakika na unachotaka kufanya

- Kitu kingine ni kumsikiliza mweza wako hata kama umeshaamua kuvunja uhusiano wenu

Kushiriki mjadala | Tembelea > https://jamii.app/WapenziKuchanaAmani
KOREA KASKAZINI YAFANYA MAJARIBIO MENGINE YA MAKOMBORA

- Imesema jaribio lingine la kurusha makombora makubwa lililofanyika jana limefanikiwa

- Jaribio hilo limepingwa na Japan na Korea Kusini wakidai ni kinyume na Kanuni za Umoja wa Mataifa

Zaidi, soma https://jamii.app/NKoreaRocketTest
BOLIVIA: UCHUNGUZI WA KIMATAIFA KUHUSU UCHAGUZI WA URAIS WAANZA

- Waangalizi wa Kimataifa kutoka Jumuiya ya Nchi za Amerika wameanza tangu Oktoba 31, 2019 kuchunguza uhesabuji wa matokeo ya Uchaguzi wa Urais wa Oktoba 20, 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/UchunguziUchaguziBolivia
UHISPANIA: WALIOBAKA WAACHIWA HURU KWA KUWA HAWAKUTUMIA NGUVU KUBAKA

- Mahakama imewaachia huru Wanaume 5 waliohukumiwa kifungo kwa kumbaka msichana wa miaka 14

- Nchini humo shtaka linaweza kuwa ubakaji iwapo nguvu ama vitisho vitatumika

Zaidi, soma https://jamii.app/WabakajiHuruUhispania
KATAVI: AFUNGWA MAISHA KWA KUMPA UJAUZITO MTOTO WAKE

- Lazaro Charles(35) amehukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kumpa ujauzito mtoto wake (14)

- Mshtakiwa alikuwa akimbaka kwa nguvu wakiwa nyumbani wakati mama yake alipokuwa amesafiri

Zaidi, soma https://jamii.app/KifungoMimbaMwanaye
IGP SIRRO AMTAKA ALIYEMTISHIA MWENZAKE BASTOLA KUFIKA POLISI

- Amemtaka kijana aitwaye Shaban anayeonekana kwenye video iliyosambaa mtandaoni akimtishia bastola mwenzake kuripoti Kituo cha Polisi mara moja na kusalimisha silaha yake

Zaidi, soma https://jamii.app/AliyetishiaBastola-Polisi
ACT WAZALENDO: UCHUKUAJI WA FOMU KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA UMEJAA HUJUMA

- Kimesema wanachama wake wanaochukua fomu wanakumbana na vikwazo mbalimbali ikiwemo kunyimwa fomu, ofisi kufungwa, kutishwa na kupewa fomu zisizo kamili

Zaidi, soma https://jamii.app/ACT-HujumaUchaguziS-Mitaa
ALIYEKUWA 'MISS GAMBIA' AMTUHUMU ALIYEKUWA RAIS WA NCHI HIYO YAHYA JAMMEH KWA KUMBAKA

> Akiwa mbele ya Kamisheni ya Maridhiano baada ya utawala wa Jammeh kuanguka amesema pia alilazimishwa kumkataa mchumba wake na ahadi ya kuolewa

Zaidi, soma => https://jamii.app/FatouVsJammeh
BILIONI 40 KUTUMIKA KULIPA MADENI YA WAKULIMA WA KOROSHO

- Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kutoa Tsh. Bilioni 40 ili kumalizia madeni yote ya Wakulima wa Korosho yaliyobaki baada ya Serikali kununua korosho msimu ulioisha

Zaidi, soma https://jamii.app/Bilioni40MadeniKorosho
MKURUGENZI ALIYETAKA MWEKEZAJI ALIPIE VIKAO KUCHUKULIWA HATUA

- Waziri Mkuu ameagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara, Maisha Mtipa achukuliwe hatua

- Alimtaka Mwekezaji alipe Tsh. Milioni 31.6 ya vikao ili kumpatia eneo

Zaidi, soma https://jamii.app/MkurugenziMwekezajiVikao-MTR