JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KISUTU, DAR: WATUHUMIWA 3 WALIOSHTAKIWA KWA KUIBA TAUSI WA IKULU, WAHUKUMIWA KULIPA FIDIA YA MILIONI 6.8

- David Graha, Mohamed Hatibu na Mohamed Ally walikamatwa kwa tuhuma za kukutwa na Ndege 3 aina ya Tausi, wa Ikulu Jijini Dar

Zaidi, soma > https://jamii.app/WashtakiwaTausiFidia
UGANDA: GODFREY WAMALA AHUKUMIWA MIAKA 14 KWA HATIA YA KUHUSIKA NA KIFO CHA MWANAMUZIKI RADIO

- Godfrey Wamala ‘Troy’ amekutwa na hatia ya kumuua bila ya kukusudia Moses Ssekibogo(Mowzey Radio)

- Alimpiga Radio hadi akapoteza fahamu na kulazwa Hospitali ya Case alikofariki

Zaidi, soma > https://jamii.app/TroyKifoRadio
KENYA: MWAI KIBAKI ADAIWA KULAZWA HOSPITALINI. MSAIDIZI WAKE AKANUSHA

- Rais wa zamani, Mwai Kibaki (88) anadaiwa kulazwa kutokana na maumivu ya goti

- Msaidizi wake amesema, Kibaki hajalazwa ila alienda hospitalini kwa uchunguzi wa kiafya

Zaidi, soma https://jamii.app/KibakiAdaiwaKulazwa
TWITTER KUSITISHA KUTANGAZA `POSTS’ ZA KISIASA, WASEMA ZINAPASWA KUSAMBAA KWA KUPENDWA NA SI KULIPIWA

- Mtendaji Mkuu wa Twitter, Jack Dorsey amesema kuwa kuna biashara kubwa ya matangazo lakini wao kuanzia Novemba 22, 2019 hawataruhusu matangazo ya kisiasa

Soma > https://jamii.app/TwitterPoliticalAds
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
CHUO KIKUU DODOMA: Tembo aonekana katika pori lililopo ndani ya Chuo hicho

> Hii ni mara ya pili kwa Mnyama aina ya Tembo kuonekana ndani ya chuo hicho na hakuna madhara yoyote kwa Wanafunzi yaliyoripotiwa

#JFLeo
BURUNDI: MWANAFUNZI AFARIKI BAADA YA KUCHAPWA VIBOKO NA MWALIMU

- Chadia Nishimwe(14) amefariki baada ya Mwalimu wake kumpiga viboko shingoni na miguuni

- Baba yake amesema kipigo kilimpelekea mtoto wake kutokwa damu puani na masikioni

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuAmuuaMwanafunzi-BRND
INDIA: MWANAMKE ADAIWA KUJIUA BAADA YA KUDHALILISHWA NA MUMEWE JUU YA NGOZI YAKE

- Ni baada ya kudhalilishwa kwasababu ya rangi nyeusi ya ngozi yake

- Inadaiwa, Wahindi wengi wana mtazamo kuwa rangi nyeupe ni watu wa tabaka la juu kuliko weusi

Zaidi, soma https://jamii.app/MumeAmdhihakiAjiua-IND
DAR: Msanii Idris Sultan amefika Kituo cha Kikuu cha Polisi (Central) muda wa saa 5 asubuhi kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda

> Anaendelea kushikiliwa kituoni kwa mahojiano

> Inadaiwa anahojiwa kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 15 na 16

Zaidi, soma https://jamii.app/IdrisAhojiwaPolisi
KENYA: Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewapongeza Wakenya kwa Kuonesha Mubashara Vikao vya Kamati vya Bunge

- Amesema “Nawapongeza kwa uzinduzi, kwamba sasa vikao vya Kamati mbalimbali vitapeperushwa mubashara (Live)”

Zaidi, soma https://jamii.app/NdugaiApongezaBungeKE
MTWARA: WATOTO 11 WA KIUME HAWAJULIKANI WALIPO

- Wametoweka kwa zaidi ya siku 10 ktk Kijiji cha Mtimbwilimbwi Halmashauri ya Nanyamba, na bado haijulikani walipo

- Mkuu wa Wilaya asema, Serikali ina taarifa na juhudi za kuwatafuta zinaendelea

Zaidi, aoma https://jamii.app/Watoto10WapoteaMtwara
BASHE: KAMA SIO MKULIMA ASIONGOZE CHAMA CHA USHIRIKA

- Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amepiga marufuku watu wasiokuwa Wakulima kuongoza Vyama vya Ushirika kwa maelezo kuwa hawana msaada wowote zaidi ya kugeuka madalali

Zaidi, soma https://jamii.app/MkulimaKiongoziAMCOS
FACEBOOK YAFUNGA AKAUNTI ZILIZOKUWA ZIKIINGILIA NCHI ZA AFRIKA

- Imeondoa akaunti kubwa tatu za Urusi, kurasa na makundi bandia yanayowahadaa Watumiaji

- Baadhi ya nchi zilizolengwa ni Madagascar, Afrika ya Kati, Msumbiji, Congo na Libya

Zaidi, soma https://jamii.app/AkauntiFBZilizoingiliaAfrika
RPC MTWARA: WATOTO WALIOPOTEA WALISHAWAHI KUKAMATWA KWA UHALIFU

- Amesema, jumla ya watoto 11 waliotoweka huenda wakawa wameenda nchini Msumbiji

- Amesema, waliwahi kukamatwa na Maafisa wa Usalama Msumbiji kwa uhalifu na kurejeshwa Nchini

Zaidi, soma https://jamii.app/Watoto10WapoteaMtwara
MARA: AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO

Maiga Maginga (18), amehukumiwa kifungo cha maisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Wilaya ya Serengeti baada ya kukiri kumlawiti mtoto wa miaka minne

Zaidi, soma https://jamii.app/KifungoMaishaUlawiti
JE, UNAFAHAMU NINI MAANA YA KATIBA NA UMUHIMU WAKE?

> Katiba ni mpangilio wa sheria zilizoandikwa au zisizoandikwa zinazotumika kuongoza nchi, taasisi au kikundi

> Nchi zote zinahitaji katiba ili ziweze kujiendesha vizuri. Nchi isiyo na katiba inaweza kuingia kwenye machafuko

Zaidi, soma > https://jamii.app/UmuhimuKatiba

#UmuhimuKatiba
MAHUSIANO: NJIA SAHIHI ZA KUACHANA NA MPENZI WAKO KWA AMANI

- Mdau kutoka JamiiForums anasema moja ya njia sahihi ya kuvunja uhusiano ni kuwa na uhakika na unachotaka kufanya

- Kitu kingine ni kumsikiliza mweza wako hata kama umeshaamua kuvunja uhusiano wenu

Kushiriki mjadala | Tembelea > https://jamii.app/WapenziKuchanaAmani
KOREA KASKAZINI YAFANYA MAJARIBIO MENGINE YA MAKOMBORA

- Imesema jaribio lingine la kurusha makombora makubwa lililofanyika jana limefanikiwa

- Jaribio hilo limepingwa na Japan na Korea Kusini wakidai ni kinyume na Kanuni za Umoja wa Mataifa

Zaidi, soma https://jamii.app/NKoreaRocketTest
BOLIVIA: UCHUNGUZI WA KIMATAIFA KUHUSU UCHAGUZI WA URAIS WAANZA

- Waangalizi wa Kimataifa kutoka Jumuiya ya Nchi za Amerika wameanza tangu Oktoba 31, 2019 kuchunguza uhesabuji wa matokeo ya Uchaguzi wa Urais wa Oktoba 20, 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/UchunguziUchaguziBolivia