JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFYA: JE, WAJUA CHANZO, DALILI NA TIBA YA TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO?

- Tatizo hili huletwa na kudhoofika au kuumia kwa neva za pembezoni mwa mwili. Moja ya dalili ni mtu kuhisi ganzi

- Kitaalamu tatizo hili hujulikana kwa jina la 'Peripheral Neuropathy'.

Kupata Ushauri, Kinga na Tiba, Soma => https://jamii.app/MiguuKuwakaMoto
MARUBANI WA NDEGE YA SHIRIKA LA SOUTHWEST WATUHUMIWA KWA KUTEGA KAMERA KATIKA VYOO VYA NDEGE

- Mfanyakazi wa kampuni hiyo anasema lengo la Marubani hao ni kuwapiga picha abiria wanapoenda ktk vyoo vya ndege hiyo wakienda kujisadia

Zaidi, soma > https://jamii.app/CameraVyooSouthwest
UGANDA: WAHALIFU WAKOSEA NA KULIWEKEA MTEGO GARI LA POLISI, MMOJA AUWA

> Waliweka kizuizi barabarani ktk eneo la Kaliro, walitegemea kuteka gari la raia wa kawaida lakini wakakumbana na gari la Polisi

> Watatu wakimbia, msako unaendelea

Soma > https://jamii.app/ThugsKaliro
WAZIRI JAFO: MARUFUKU UCHUKUAJI FOMU ZA UGOMBEA KWA MBWEMBWE

- Amevionya Vyama vya Siasa kuacha shamrashamra wakati Wagombea wao wa Serikali za Mitaa wanapochukua fomu

- Amesema vitendo hivyo vitaashiria kampeni kuanza wakati muda wake bado

Zaidi, soma https://jamii.app/MarufukuMbwembweUchukuajiFomu
KENYA: MWALIMU ASAKWA KWA KUMNAJISI MWANAFUNZI WA KIKE ALIYEMUAHIDI KUMLIPIA ADA

> Alimuita nyumbani kwake Mwanafunzi huyo wa Darasa la 5 wa Shule ya Madaraka ili ampe vitabu kisha akamnajisi

> Mwanafunzi aliyenajisiwa ana miaka 12

Soma > https://jamii.app/MwlAnajisiMeruCounty
BUGIRI, UGANDA: MTOTO ATEKETEA KWA MOTO, BABA YAKE AKIWA ANAANGALIA MCHEZO WA ARSENAL FC

> Mtoto wa Kike wa miaka 6 amefariki kwa kuteketea kwa moto; Baba yake alimuacha na kwenda kufuatilia mchezo kati ya Arsenal na Crystal Palace

Zaidi, soma > https://jamii.app/MtotoMotoBugiriUG
KENYA: NDEGE YA SHIRIKA LA SILVERSTONE YATUA KWA DHARURA BAADA YA GURUDUMU KUNG'OKA

- Ndege hiyo imelazimika kutua katika Uwanja wa Eldoret

- KCAA imeanza kuzichunguza Ndege za Shirika hilo baada ya nyingine kupata ajali wiki 2 zilizopita

Soma > https://jamii.app/KCAAVsSilverstone
KATAVI: MKUU WA MKOA AKANUSHA KUSEMA ANATAKA WANANCHI WAROGWE ILI WAPIGE KURA

- Mkuu wa Wilaya ya Katavi, Juma Homera amedai Wapinzani wake wamemzushia kauli hiyo

- Amesema anajua wanafanya hivyo kwa kuwa amewashika pabaya na anawanyoosha kama rula

Zaidi, soma https://jamii.app/HomeraAkanushaKutakaWananchiWarogwe
LUDEWA, NJOMBE: DC ATAKA WANAOISHI BILA NDOA WAPELEKWE MAHABUSU

- Andrea Tsele amemuagiza Mtendaji wa Kata ya Mavanga kuwapeleka Mahabusu watu wanaoishi bila ndoa

- Amesema, wasiofunga ndoa wanaongeza watoto wa mtaani kwani wanazaa na kuachana

Zaidi, soma https://jamii.app/LudewaWaoishioBilaNdoaMahabusu
TANZANIA KUZIJIBU RIPOTI ZA AMNESTY NA HRW MSTARI KWA MSTARI

- Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema Serikali inachukulia ripoti hizo kwa uzito mkubwa na baadhi ya mambo walishayatolea maelezo kipindi cha nyuma

Zaidi, soma https://jamii.app/TZKujibuRipotiAmnestyHRW
JE, WAJUA CHANZO CHA UGONJWA WA SARATANI?

- Ugonjwa huu unaotokea katika viini vya mwili vinavyohusika na kurithisha tabia kutoka kizazi kimoja hadi kingine

- Moshi wa tumbaku, magari na mionzi ya jua na X-rays vyatajwa kuwa visababishi

Kufahamu zaidi, tembelea https://jamii.app/ElimuSaratani
HERI YA KUZALIWA RAIS MAGUFULI

> Leo, Oktoba 29, 2019 Rais John Pombe Joseph Magufuli anatimiza umri wa miaka 60

> Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) alizaliwa Oktoba 29, 1959
SIKU YA KIHARUSI DUNIANI: Huadhimishwa Oktoba 29, ili kusisitiza uwepo wa ugonjwa huo, kuongeza uelewa wa kuzuia na matibabu yake

- #Kiharusi kinaweza kutokea kwa mtu yeyote, wakati wowote na mahali popote

Kufahamu zaidi, soma https://jamii.app/DaliliMadharaKiharusi

#StrokeDay
KENYA: DANIEL ARAP MOI ALAZWA TENA HOSPITALI WIKI MBILI BAADA YA KUTOKA

- Rais huyo wa Zamani wa Kenya, amelazwa katika Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) katika hospitali ya Nairobi

- Madaktari wanaomuhudumia wanasema ni kutokana na maumivu ya kifua na shida katika kupumua

Zaidi, soma https://jamii.app/MoiAdmittedAgain
USHAURI: WANAOMALIZA KIDATO CHA SITA WAPELEKWE VETA BADALA YA JKT

- Mdau kutoka JamiiForums ameiomba Serikali ibadili sera kwa Vijana wanaomaliza Kidato cha Sita kupelekwa VETA ili wakapate mafunzo ya awali ya ufundi mbalimbali

- Amedai, mabadiliko hayo yatasaidia kuwaandaa vijana wenye ujuzi mbalimbali mitaani watakaoweza kujiajiri au kuajiriwa

Kujadili, tembelea https://jamii.app/Vijana-JKTvsVETA
SERIKALI YADAIWA KUINGILIA UHURU WA MAHAKAMA KATIKA KESI YA BULAYA DHIDI YA WASIRA

- Jaji Mfawidhi mstaafu, Noel Chocha asema alipata vishawishi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali wakitaka aubebe upande mmoja

Zaidi, soma > https://jamii.app/JajiChochaHaki
RIPOTI YA CAG KWA MWAKA 2017/18: MAMLAKA YA BANDARI NCHINI YAKALIA KUTI KAVU

- Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali yataka uchunguzi wa mapungufu ktk ununuzi wa vifaa vya TEHAMA, ununuzi wa ardhi na ajira 32 kama ilivyoanishwa ktk ripoti

Soma > https://jamii.app/PACvsTPA
ENGLAND: Wachezaji na Wafanyakazi wa Klabu ya Southampton wameamua kila mmoja atatoa mshahara wake wa siku moja kwenda Taasisi ya kusaidia Watoto, Vijana na Watu wazima ya Saints Foundation

- Uamuzi huu ni baada ya kufungwa goli 9-0 na klabu ya Leicester, Oktoba 25
AMERIKA KUSINI: MAASKOFU KATOLIKI WAPITISHA PENDEKEZO LA KUWA NA MAPADRI WALIOOA

- Pendekezo limepitishwa kwa kura 128 dhidi ya 41

- Nchi zilizo kwenye pendekezo ni Bolivia, Brazil, Colombia, Ecuador, French Guiana, Guyana, Peru na Venezuela

Soma https://jamii.app/KatolikiLatinAmerica
IRAQ: MAANDAMANO YAENDELEA, WATU WAUAWA NA WENGINE WAJERUHIWA

- Watu 18 wameuawa na mamia kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa dhidi ya Waandamanaji huko Karbala

- Waandamanaji hao wanapinga rushwa Serikalini na ukosefu wa huduma muhimu

Zaidi, soma https://jamii.app/18WauawaIraqMaandamano