JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZIMBABWE WAANDAMANA KUPINGA VIKWAZO VYA MAREKANI NA UMOJA WA ULAYA

> Marekani na Ulaya imewawekea vikwazo maafisa wengi waandamizi wa Zimbabwe pamoja na Rais Mnangagwa kwa madai ya kukiuka haki za binadamu na udanganyifu katika Uchaguzi Mkuu, miaka iliyopita

> Rais Mnangagwa amesema vikwazo hivyo vimeathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa Zimbabwe

Soma - https://jamii.app/ZBWProtestSASanctions
MVUA MKOANI TANGA: TAKRIBAN WATU 8 WAFARIKI

> Takriban Watu nane (8) wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya gari aina ya Noah kutumbukia kwenye daraja ktk eneo la Sindeni barabara kuu ya Handeni - Korogwe, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Tanga
ABIRIA WANAOSAFIRI DAR, ARUSHA NA KILIMANJARO WAKWAMA NJIANI KWA SAA 20

> Abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Arusha, Kilimanjaro na nchi jirani na waliotoka Dar es Salaam kuelekea mikoa mbalimbali wamekwama tangu jana, saa 5 asubuhi Wilayani Korogwe na Handeni kutokana na maji yaliyotokana na mvua kupita juu ya daraja la Mandera na kulisomba daraja la Handeni

Soma - https://jamii.app/AbiriaWakwamaMvua
HOJA: FANI YA UFUNDI WA MAGARI IMEJAA WATU WASIO NA ELIMU HIYO, WASOMI TUNAKWAMA WAPI?

> Mdau wa JamiiForums amesema yeye ni Mhitimu wa Mechanical Engineering na amejikita katika Ufundi wa Magari

> Anasema, watu mahiri katika fani hiyo ni wale ambao hawakwenda shule

Kwa mjadala, fungua > https://jamii.app/UfundiMagariElimu
WATU 10 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA MAFURIKO YA MVUA JAPAN

> Mito 15 imefurika kwasababu ya mvua hiyo, watu 800 wameokolewa kutoka katika nyumba zao, wanafunzi elfu 2 wamenasa katika shule

> Safari nyingi za ndege zimeahirishwa na Hospitali kadhaa zimefurika maj

Soma - https://jamii.app/MadharaVifoMafuriko
BREAKING NEWS: Reports suggest leader of Islamic State (IS), Abu Bakr al Baghdadi has been killed in a raid conducted by the U.S. military in northwest Syria

> The final confirmation is pending while DNA and biometric testing is conducted
JamiiForums
Photo
DEVELOPING: The raid was carried out by special operations forces after they received "actionable intelligence"

> The defense official said it appears that Baghdadi detonated a suicide vest during the raid

> The CIA assisted in locating the ISIS leader
MGOGORO CATALONIA: MAELFU WAENDELEA KUHIMIZA KUJITENGA

- Wameandamana Barcelona wakipinga kuhukumiwa kwa Viongozi wa kujitenga huku wakisisitiza kujitenga

- Viongozi 9 wa Mpango huo walihukumiwa Oktoba 14 na Mahakama Kuu kwa kosa la uasi

Zaidi, soma https://jamii.app/SeparatistsProtestCatalonia
MAREKANI YAFUTA SAFARI ZA NDEGE KWENDA CUBA

> Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema uamuzi huo umechukuliwa kama muendelezo wa vikwazo dhidi ya utawala huo kukandamiza raia wake na kuunga mkono utawala wa Rais Nicolas Maduro, nchini Venezuela

Soma - https://jamii.app/USBanFlightsCuba
MUDA MREFU WA KUJAMIIANA NI DAKIKA 13, USIJIUE KWA KUTUMIA MADAWA

> Ujumbe huu ni mahususi kwa Wanandoa, utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka nchini Marekani na Canada umeeleza kuwa dakika 13 ni sawa kwa tendo hilo

Kwa ufafanuzi zaidi, fungua > https://jamii.app/SaxRange
RAIS WA ZANZIBAR AITAKA JUMUIYA YA MAJAJI EAC KUANDIKA SHERIA KWA KISWAHILI

> Rais Dkt. Ali Mohamed Shein amesema hatua hiyo itawasaidia na kuwarahisishia wananchi kupata haki zao sambamba na kuzifahamu vyema sheria za nchi zao kwani jambo hilo lina umuhimu mkubwa katika kutafuta haki kwa wananchi hali itakayowafanya kuwa Raia Bora na wenye kutii Sheria za Nchi

Soma - https://jamii.app/LughaSheriaKiswahili
KATAVI: MKUU WA MKOA AWAPA WAGANGA KAZI YA KUWALOGA WANANCHI WA MKOA HUO ILI WAPIGE KURA

- RC Juma Homera, amewataka Waganga wa Jadi utumia ujuzi wao kuwaloga watu ili wakapige kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba 24, 2019

Soma > https://jamii.app/RCKataviWaganga
SHIRIKA LA RELI LASITISHA SAFARI KWA UKANDA WA KASKAZINI

- Limeomba radhi kwa safari za mikoa ya Kilimanjaro na Tanga kusitishwa kuanzia Oktoba 26, 2019

- Ni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na zilizosababisha uharibifu wa miundombinu

Zaidi, soma https://jamii.app/TRCSafariKaskZasitishwa
MWANARIADHA WA TANZANIA ANYAKUA MEDALI YA FEDHA

- Mwanariadha Alphonce Simbu ameshinda medali hiyo katika Mashindano ya Majeshi ya Dunia yanayoendelea China

- Mwanariadha huyo ambaye ni Mwanajeshi wa JWTZ, alikimbia Marathon kwa saa 2:11:16

Zaidi, soma https://jamii.app/TanzaniaMedaliSilver
1