JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
HARMONIZE AWAKERA WANAHABARI KENYA, WASEMA ANA DHARAU ILIYOKOMAA

- Wamekasirika baada ya Mwanamuziki huyo kutoka Tanzania, kuwapa dakika 3 za mahojiano

- Afika kwenye mahojiano akiwa ameongozana na walinzi waliowasukuma Wanahabari

Soma > https://jamii.app/HarmonizeKenya
RIPOTI: HALI YA HOFU, UDHIBITI WA VYOMBO VYA HABARI NA UKANDAMIZAJI #TANZANIA

- Taasisi za Amnesty International na Human Right Watch zimesema Ukandamizaji wa vyombo vya habari, Watetezi wa #HakiZaBinadamu na vyama vya upinzani umeongezeka tangu mwaka 2015

- Sera na hatua za kupinga mabadiliko ya Serikali zimezuia vyombo vya habari, zimepandikiza hofu kati ya Asasi za Kiraia na kuminya shughuli za vyama vya siasa

Zaidi, tembelea https://jamii.app/RipotiAmnestyUkandamizajiTZ
URUSI: MWANAJESHI AWAUAWA KWA RISASI WENZAKE 8 NA KUWAJERUHI WENGINE WAWILI

- Ramil Shamsutdinov amekamatwa na taarifa za awali zinaeleza kuwa huenda Askari huyo anaugua magonjwa ya akili

- Alifyatua risasi wakati wa kubadilishana zamu

Soma > https://jamii.app/MwanajeshiAuaUrusi
VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WANAOWAHUJUMU WAKULIMA WATAKIWA KUKAMATWA

- Agizo limetolewa na Waziri Lugola kwenda kwa Polisi Nchini

- Ni baada ya DC wa Bunda kuwakamata viongozi walioshindwa kurejesha Serikalini zaidi ya Tsh. Bilioni 1.8

Zaidi, soma https://jamii.app/ViongoziUshirikaKukamatwa
UMOJA WA ULAYA (EU) WAKUBALI KUIONGEZEA MUDA UINGEREZA KUJADILI BREXIT

- Wamekubaliana na ombi la Uingereza la kuongeza muda wa miezi 3 wa kupitisha mpango wake wa kujitoa kwenye Umoja huo (Brexit) ikiwa awali mwisho ilikuwa Oktoba 31, 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/EUAgreesBrexitExtension
AFYA: WAZIJUA ATHARI ZA KUNYWA MAJI MENGI KUPITA KIASI?

> Kunywa maji kupitia kiasi husababisha kutokwa na jasho jingi, usumbufu wakati wa kulala, kumewahi sababisha kifo

> Je, wajua kiasi kinachoshauriwa na Wataalamu?

Kwa makala hii, soma > https://jamii.app/KiasiMajiMwili
#JFAfya
RC CHALAMILA: WANAOKOSOA MAENDELEO YA SERIKALI WENGI HAWAJAOLEWA, HAWAJAOA AU WAMEACHIKA

- RC wa Mbeya, Albert Chalamila amedai kwa utafiti alioufanya, amegundua hayo na pia amedai Wakosoajia hao hudhani Serikali ndiyo imeharibu mahusiano yao

Zaidi, soma https://jamii.app/ChalamilaUhusianoSerikali
AFYA: JE, WAJUA CHANZO, DALILI NA TIBA YA TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO?

- Tatizo hili huletwa na kudhoofika au kuumia kwa neva za pembezoni mwa mwili. Moja ya dalili ni mtu kuhisi ganzi

- Kitaalamu tatizo hili hujulikana kwa jina la 'Peripheral Neuropathy'.

Kupata Ushauri, Kinga na Tiba, Soma => https://jamii.app/MiguuKuwakaMoto
MARUBANI WA NDEGE YA SHIRIKA LA SOUTHWEST WATUHUMIWA KWA KUTEGA KAMERA KATIKA VYOO VYA NDEGE

- Mfanyakazi wa kampuni hiyo anasema lengo la Marubani hao ni kuwapiga picha abiria wanapoenda ktk vyoo vya ndege hiyo wakienda kujisadia

Zaidi, soma > https://jamii.app/CameraVyooSouthwest
UGANDA: WAHALIFU WAKOSEA NA KULIWEKEA MTEGO GARI LA POLISI, MMOJA AUWA

> Waliweka kizuizi barabarani ktk eneo la Kaliro, walitegemea kuteka gari la raia wa kawaida lakini wakakumbana na gari la Polisi

> Watatu wakimbia, msako unaendelea

Soma > https://jamii.app/ThugsKaliro
WAZIRI JAFO: MARUFUKU UCHUKUAJI FOMU ZA UGOMBEA KWA MBWEMBWE

- Amevionya Vyama vya Siasa kuacha shamrashamra wakati Wagombea wao wa Serikali za Mitaa wanapochukua fomu

- Amesema vitendo hivyo vitaashiria kampeni kuanza wakati muda wake bado

Zaidi, soma https://jamii.app/MarufukuMbwembweUchukuajiFomu
KENYA: MWALIMU ASAKWA KWA KUMNAJISI MWANAFUNZI WA KIKE ALIYEMUAHIDI KUMLIPIA ADA

> Alimuita nyumbani kwake Mwanafunzi huyo wa Darasa la 5 wa Shule ya Madaraka ili ampe vitabu kisha akamnajisi

> Mwanafunzi aliyenajisiwa ana miaka 12

Soma > https://jamii.app/MwlAnajisiMeruCounty
BUGIRI, UGANDA: MTOTO ATEKETEA KWA MOTO, BABA YAKE AKIWA ANAANGALIA MCHEZO WA ARSENAL FC

> Mtoto wa Kike wa miaka 6 amefariki kwa kuteketea kwa moto; Baba yake alimuacha na kwenda kufuatilia mchezo kati ya Arsenal na Crystal Palace

Zaidi, soma > https://jamii.app/MtotoMotoBugiriUG
KENYA: NDEGE YA SHIRIKA LA SILVERSTONE YATUA KWA DHARURA BAADA YA GURUDUMU KUNG'OKA

- Ndege hiyo imelazimika kutua katika Uwanja wa Eldoret

- KCAA imeanza kuzichunguza Ndege za Shirika hilo baada ya nyingine kupata ajali wiki 2 zilizopita

Soma > https://jamii.app/KCAAVsSilverstone
KATAVI: MKUU WA MKOA AKANUSHA KUSEMA ANATAKA WANANCHI WAROGWE ILI WAPIGE KURA

- Mkuu wa Wilaya ya Katavi, Juma Homera amedai Wapinzani wake wamemzushia kauli hiyo

- Amesema anajua wanafanya hivyo kwa kuwa amewashika pabaya na anawanyoosha kama rula

Zaidi, soma https://jamii.app/HomeraAkanushaKutakaWananchiWarogwe
LUDEWA, NJOMBE: DC ATAKA WANAOISHI BILA NDOA WAPELEKWE MAHABUSU

- Andrea Tsele amemuagiza Mtendaji wa Kata ya Mavanga kuwapeleka Mahabusu watu wanaoishi bila ndoa

- Amesema, wasiofunga ndoa wanaongeza watoto wa mtaani kwani wanazaa na kuachana

Zaidi, soma https://jamii.app/LudewaWaoishioBilaNdoaMahabusu
TANZANIA KUZIJIBU RIPOTI ZA AMNESTY NA HRW MSTARI KWA MSTARI

- Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema Serikali inachukulia ripoti hizo kwa uzito mkubwa na baadhi ya mambo walishayatolea maelezo kipindi cha nyuma

Zaidi, soma https://jamii.app/TZKujibuRipotiAmnestyHRW
JE, WAJUA CHANZO CHA UGONJWA WA SARATANI?

- Ugonjwa huu unaotokea katika viini vya mwili vinavyohusika na kurithisha tabia kutoka kizazi kimoja hadi kingine

- Moshi wa tumbaku, magari na mionzi ya jua na X-rays vyatajwa kuwa visababishi

Kufahamu zaidi, tembelea https://jamii.app/ElimuSaratani
HERI YA KUZALIWA RAIS MAGUFULI

> Leo, Oktoba 29, 2019 Rais John Pombe Joseph Magufuli anatimiza umri wa miaka 60

> Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) alizaliwa Oktoba 29, 1959
SIKU YA KIHARUSI DUNIANI: Huadhimishwa Oktoba 29, ili kusisitiza uwepo wa ugonjwa huo, kuongeza uelewa wa kuzuia na matibabu yake

- #Kiharusi kinaweza kutokea kwa mtu yeyote, wakati wowote na mahali popote

Kufahamu zaidi, soma https://jamii.app/DaliliMadharaKiharusi

#StrokeDay