JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RWANDA YAPIGA HATUA KUBWA KATIKA KUPAMBANA NA UKIMWI

> 84% ya watu wote wanaoishi na VVU wanafahamu hali zao, 98% ya waliokutwa na maambukizi wanapata dawa, 90% ya wanaotumia dawa hizo hawapati magonjwa yanayotokana na mfumo wa hewa, hivyo kufikia 84-98-90 kati ya 90-90-90 ya lengo lililowekwa na UNAIDS

Soma - https://jamii.app/HIVPrevalenceReduced
WB: KWA MUONGO 1 UCHUMI WA TANZANIA UMEKUWA UKIIMARIKA NA PATO LA TAIFA LIKIKUA

> Takwimu za Benki ya Dunia zinaonesha kuwa Tanzania imekuwa na uchumi imara na ukuaji mkubwa wa pato la Taifa kwa wastani wa 8%

> Pia, imehakikisha ukuaji wa ajira rasmi na zisizo rasmi unabaki katika kiwango kizuri kikiwa kwenye wastani wa 1.9%

Soma - https://jamii.app/KukuaUchumiPatoTZ
ISRAELI: WAZIRI MKUU, BENJAMIN NETANYAHU AKWAMA KUUNDA BARAZA LA MAWAZIRI

> Ameshindwa kumshawishi kiongozi wa Chama cha Blue and White, Benny Gantz ili waweze kuunda Serikali ya Mseto

>Amerudisha mamlaka hayo kwa Rais wa nchi hiyo

Soma > https://jamii.app/NetanyahuBaraza
TANZIA: MWANASIASA MKONGWE NA MWANZILISHI WA CHAMA CHA CUF AFARIKI DUNIA

> Mzee James Mapalala amefariki dunia leo katika hospitali ya Kairuki

> Alilazwa wiki 2 zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi katika mfumo wa upumuaji

Zaidi, soma > https://jamii.app/RIPMapalala
MAADHIMISHO YA JAMHURI: RAIA WA KENYA KUPITIA 'YOUTUBE' WAKERWA NA UCHAKAVU WA NDEGE ZAO ZA JESHI

- Wananchi wa taifa hilo kupitia mtandao wa 'YouTube' wameitupia lawama Serikali yao kwa kushindwa kununua ndege mpya na za kisasa licha ya fedha kuwepo

Soma > https://jamii.app/KenyaNdege
NI KWELI KUNA WATU UKIWA NAO KIMAPENZI HULETA MIKOSI/NUKSI?

> Kumekua na kasumba au dhana fulani ambayo imejengeka katika jamii kuwa kuna watu ukiwa nao kwenye mahusiano basi wanaweza kukusababishia mikosi au nuksi

> Mfano, mwanaume unaweza ukawa upo vizuri kiuchumi ikatokea ukaingia kwenye mahusiano na mwanamke fulani baada ya muda unajikuta unaanza kufilisika na kuhisi labda mtu ulienae ndio kisababishi. Na kwa wanawake pia kinyume chake

> Yawezekana umewahi kusikia hii kitu au wengine imewahi kuwatokea. Tupeni uzoefu katika hili. Je, hii hali ipo kweli au porojo?

Kujadili zaidi - https://jamii.app/MikosiNuksiMapenzi
#JFMahusiano
KWANINI VIONGOZI WASTAAFU BADO WANAPEWA KAZI BADALA YA KUACHWA WAPUMZIKE?

> Mdau aliyeleta hoja hii ndani ya JamiiForums anasema, kuna Watanzania wengi wenye kiu ya kuitumikia Serikali

> Anasema, tujenge utaratibu wa kuwapa nafasi watu wapya

Soma > https://jamii.app/HojaWastaafu
#JFLeo
KOREA KASKAZINI KUVUNJA HOTELI ILIYOJENGWA NA KOREA KUSINI

> Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameamuru kuvunjwa kwa hoteli na miundombinu ya utalii iliyojengwa na Korea Kusini eneo la Kaskazini ya nchi hiyo

> Asema imekosa mvuto na haiakisi taswira ya Korea Kaskazini

Soma - https://jamii.app/KimOrdersDemolitionHotelsSK
MAREKANI KUIONDOLEA VIKWAZO UTURUKI BAADA YA KUSITISHA MAPIGANO

> Rais Donald Trump amesema kutokana na Uturuki kukubali kusitisha vita Kaskazini mwa Syria, Marekani itaondoa vikwazo dhidi ya nchi hiyo vilivyoanza kutekelezwa siku 10 zilizopita

> Jeshi la Uturuki lilianzisha operesheni dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi Oktoba 9, 2019

Soma - https://jamii.app/TrumpLiftsSanctionsTurkey
JE, WAJUA SHERIA YA NDOA INARUHUSU KUDAI ZAWADI ULIZOTOA UCHUMBA UNAPOVUNJIKA

- Kifungu cha 69 (1) kinatoa haki ya kufungua shauri na kudai fidia baada ya uchumba kuvunjwa

- Kifungu cha 71 kinatoa haki ya kufungua shauri kudai zawadi ulizotoa

Soma > https://jamii.app/ZawadiUchumba
BANGLADESH: WATU 16 WAHUKUMIWA KIFO KWA MAUAJI YA MSICHANA ALIYECHOMWA MOTO

> Mahakama ya Bangladesh imewahukumu kifo watu 16 kwa mauaji ya Nusrat Jahan Rafi (19), aliyechomwa moto akiwa hai baada ya kufikisha malalamiko yake Mahakamani kuwa alibakwa na Mkuu wa Shule ya Kidini (Madrasa)

Soma - https://jamii.app/16JailedMurderStudent
TRA: ATAKAYEFICHUA WAKWEPA KODI KULIPWA 3% YA KODI ITAKAYOKOMBOLEWA

> Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Diana Masalla amesema mwananchi yeyote atakayefichua wakwepa kodi atalipwa asimilia 3 ya kodi iliyokusanywa kutoka kwa mdaiwa lakini haitazidi Tsh. milioni 20

Soma - https://jamii.app/MalipoWafichuziKodi
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: WAKANDARASI WA KAMPUNI ZA NYANZA NA CHICCO WAKAMATWA KWA AMRI YA MKUU WA MKOA

- Katibu Tawala Mkoa, Abubakar Kunenge amesema Kampuni hizo zimekwishalipwa Bilioni 4.8 lakini bado zinafanya kazi chini ya kiwango na kusababisha maafa

Soma > https://jamii.app/ChiccoNyanzaDar
JE, WANAUME WENGI SIKU HIZI WANAKABILIWA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME?

> Kumekuwa na mijadala mingi inayopelekea tatizo hili kuzungumzwa sana kwa miaka ya hivi karibuni kuliko zamani hadi kusababisha woga mkubwa kwa baadhi ya wanaume

> Baadhi yao hulazimika kula vipande vya Nazi, Maranga na Muhogo mbichi na kunywa supu ya Pweza kama tiba mbadala

> Ni kweli tatizo hili ni kubwa kwa kizazi cha sasa? Nini kifanyike?

Tembelea - https://jamii.app/TatizoNguvuKiume
#JFAfya
WANANCHI WATAKIWA KUEPUKA KUTUMIA DAWA ZINAZOTANGAZWA MTANDAONI

> Serikali imewataka wananchi kuepuka matumizi ya dawa hizo kwa kuwa hazijadhibitishwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)

> Aidha, aliyedai Waziri Ummy alifungua duka la dawa za kuongeza viungo vya wanaume akamatwa kwa kuwa taarifa hizo hazikuwa za kweli

Soma - https://jamii.app/ZuioDawaMitandaoni
UINGEREZA: MIILI 39 ILIYOKUTWA NDANI YA LORI KUSINI MWA NCHI HIYO, ILIKUWA NI YA RAIA WA CHINA

> Idara za Polisi England, Ireland ya Kaskazini na Ubelgiji zinaendelea na juhudi za kuitambua miili hiyo na jinsi gani imeweza kufika Uingereza

Soma > https://jamii.app/MiiliEssexChina
WAZIRI KAMWELWE AAGIZA KUKAMATWA KWA ANAYEENDESHA MTANDAO WA ATCL 'AVIATION TV'

> Ameagiza kukamatwa kwa mtu huyo kwa kutangaza kuwa ndege mpya aina ya Dreamliner inakuja nchini wakati si kweli

> Asema, kila jambo lina mamlaka zake za kutangaza na kama ni suala la ndege, Wizara yake ndio ina dhamana ya kutangaza

Soma - https://jamii.app/KukamatwaMwendeshajiAviationTv
BURUDANI: MWANAMUZIKI HARMONIZE ASEMA ALIPASWA KUILIPA KAMPUNI YA WASAFI MILIONI 500 ILI AWE HURU

> Amelazimika kuuza nyumba zake 3 na baadhi ya mali zake ili aweze kulipa kiasi hicho kwasababu hakuwa na fedha

> Kuhusu Rais Magufuli kuwa na kiu ya kumuona anakuwa Mbunge wa Tandahimba amesema hilo ni agizo hivyo lazima atekeleze

Soma > https://jamii.app/HarmonizeVsWCB
IRINGA: JESHI LA POLISI LAMZUIA MBUNGE PETER MSIGWA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA, LASEMA HAKUNA ASKARI WA KUTOSHA KUTOA ULINZI

> Mbunge huyo ameelezwa, ktk barua yake ya kulitaarifu Jeshi la Polisi hakuainisha dhumuni la kufanya mkutano huo

Soma > https://jamii.app/MsigwaPolisi
RAIA WA NIGERIA WANAOTUHUMIWA KWA KESI YA #DAWAZAKULEVYA NAO WAMUANDIKIA BARUA DPP KUKIRI MAKOSA YAO

- Washtakiwa hao ni Henry Ozoemana Ogwuanyi(Mchungaji), Onyebuchi Ogbu na Lucy Oding waliokutwa na Kilo 15.8 za Heroin

Zaidi, soma > https://jamii.app/NigeriansDPP