JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: RAIS MSTAAFU JIMMY CARTER AANGUKA NA KUVUNJIKA NYONGA, AKIMBIZWA HOSPITALI

> Jimmy Carter(95) sasa amelazwa katika Kituo cha Afya cha Phoebe Sumter baada ya kuanguka na kuvunjika nyonga

> Aliiongoza Marekani mwaka 1977 hadi 1981

Soma > https://jamii.app/JimmyCarterPelvic
CAG PROFESA ASSAD ASEMA KAMATI ZA BUNGE ZAANZA KUFANYIA KAZI RIPOTI YA OFISI YAKE

> Profesa Assad pia, amezipongeza Halmashauri zilizofanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato ya Serikali kama ilivyotangazwa na Waziri, Selemani Jaffo

Zaidi, soma > https://jamii.app/CAGPongezi
MAREKANI: MWIZI AVUNJA NYUMBA NA KUINGIA NDANI, KABLA YA KUIBA AMUOGESHA MTOTO

> Elizabeth Hixon(22) anashikiliwa na Polisi baada ya kuvamia nyumbani kwa Areica Hill

> Kabla ya kufanya wizi alinza kumuogesha Mtoto wa Kiume aliyemkuta amelala

Soma > https://jamii.app/HouseBurglary
MAHUSIANO: JE, KUNA ULAZIMA WA KUMHUDUMIA MCHUMBA WA KIKE?
-
Mdau wa JamiiForums anasema, kwa upande wake amejiwekea malengo ya kumhudumia mpenzi wake pindi atakapokuwa Mke wake halali

> Kama mwanamke anakaa kwao, basi wazazi wake ndio wana wajibu wa kutoa huduma

Soma > https://jamii.app/HudumaMpenzi
UDSM KUANZA KUTOA MITIHANI YA KIMATAIFA YA UJUZI WA KISWAHILI

> Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinatarajia kuanza kutoa Mitihani hiyo mwaka 2020, kwa lengo la kuhakikisha lugha ya Kiswahili inakua zaidi

> Itakuwa ikifanyika mara sita kwa mwaka kwa njia za kielektroniki katika vyuo na vituo mbalimbali vya Kiswahili duniani

Soma - https://jamii.app/UDSMKukuzaKiswahili
WIZARA YAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUUZA NYAMA PORI

> Wizara ya Maliasili na Utalii imesema ifikapo Desemba 2019, kanuni zitakuwa zimekamilika na watatangaza kwa umma maeneo yatakapokuwepo mabucha na Serikali itaendelea kudhibiti biashara hiyo ili mwananchi aweze kununua nyama hiyo kwa njia halali

Soma - https://jamii.app/ZuioKuuzaNyamapori
MARA: FISI WAVAMIA MSIBA NA KUJERUHI WATU WAWILI

> Watu 2 wameshambuliwa na Fisi wasiojulikana idadi yao baada ya kuvamia kwenye mji uliokuwa na msiba, Wilayani Bunda

> Majeruhi ni David Robert aliyejeruhiwa sehemu mbalimbali ikiwemo mikono yake na Elizabeth Mgeta (60) ambaye amejeruhiwa mkono mmoja

Soma - https://jamii.app/FisiUvamiziMsiba
KENYA: ASKARI POLISI ALIYEPINGA KUPELEKWA MAENEO YA KAZI AMBAYO HAWEZI KUJIPATIA FEDHA, APEWA LIKIZO YA LAZIMA

> Jane Asimizi, amepewa likizo hiyo ya lazima baada ya kuonekana kupitia video akilalamikia kupangwa maeneo yesiyo na ulaji

Soma > https://jamii.app/AsimiziLeave
HOJA: Wanafunzi wengi wanapohitimu masomo hutegemea na huamini kuwa vyeti vyao ndivyo vitakavyowakomboa lakini si kweli. Badala ya kukazana kutembea na vyeti, weka juhudi katika kutumia fursa zinazojitokeza mbele yako
-
Endapo mtu akikupa nafasi ya kufanya kitu na huna uhakika kama utaweza kukifanya, kubali kukifanya, kisha jifunze namna ya kukifanya. Wenye uwezo wa kukariri ndio wanaofanikiwa shuleni, lakini katika maisha wenye ubunifu na uwezo wa kutatua matatizo ndio wanaofanikiwa
-
Kuongoza darasani hakumaanishi utaweza kufanya vizuri kwenye maisha nje ya darasa. Duniani kuna watu wengi ambao hawakufanya vizuri darasani lakini ni matajiri kutokana na uwezo wao wa kuchangamkia fursa na kutatua matatizo
-
Tembelea > https://jamii.app/ElimuVsFursaMafanikio
MAHAKAMA YATAKA UTHIBITISHO WA MAENDELEO YA AFYA YA LISSU

> Mahakama ya Kisutu imewataka wadhamini wa Tundu Lissu kwenda na uthibitisho wa maendeleo ya afya yake kesi hiyo itakapotajwa tena baada ya kudai kuwa Lissu bado anaumwa

> Hakimu ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21, 2019

Soma - https://jamii.app/VithibitishoAfyaLissu
WAASI 14 WAUAWA KATIKA MAPIGANO MAGHARIBI MWA BURUNDI

> Vikosi vya Serikali ya Burundi vimewaua Waasi 14 na kukamata bunduki 11, baada ya kuzuka kwa mapigano makali katika Wilaya ya Musigasi

> Waasi waliouawa ni wa kikundi cha Red–Tabara kinachoupinga uongozi wa Rais Pierre Nkurunziza

Soma - https://jamii.app/RebelsKilledAttackBRN
TANZANIA YATANGAZA KUIUNGA MKONO CHINA KWENYE MGOGORO WAKE NA JIMBO HONG KONG

> Waziri wa Katiba na Sheria, Augustine Mahiga amesema kuwa mgogoro huo unachochewa zaidi ya vyombo vya habari vya mataifa makubwa ya Magharibi

Zaidi, soma > https://jamii.app/TanzaniaSupportsChina
RWANDA YAPIGA HATUA KUBWA KATIKA KUPAMBANA NA UKIMWI

> 84% ya watu wote wanaoishi na VVU wanafahamu hali zao, 98% ya waliokutwa na maambukizi wanapata dawa, 90% ya wanaotumia dawa hizo hawapati magonjwa yanayotokana na mfumo wa hewa, hivyo kufikia 84-98-90 kati ya 90-90-90 ya lengo lililowekwa na UNAIDS

Soma - https://jamii.app/HIVPrevalenceReduced
WB: KWA MUONGO 1 UCHUMI WA TANZANIA UMEKUWA UKIIMARIKA NA PATO LA TAIFA LIKIKUA

> Takwimu za Benki ya Dunia zinaonesha kuwa Tanzania imekuwa na uchumi imara na ukuaji mkubwa wa pato la Taifa kwa wastani wa 8%

> Pia, imehakikisha ukuaji wa ajira rasmi na zisizo rasmi unabaki katika kiwango kizuri kikiwa kwenye wastani wa 1.9%

Soma - https://jamii.app/KukuaUchumiPatoTZ
ISRAELI: WAZIRI MKUU, BENJAMIN NETANYAHU AKWAMA KUUNDA BARAZA LA MAWAZIRI

> Ameshindwa kumshawishi kiongozi wa Chama cha Blue and White, Benny Gantz ili waweze kuunda Serikali ya Mseto

>Amerudisha mamlaka hayo kwa Rais wa nchi hiyo

Soma > https://jamii.app/NetanyahuBaraza
TANZIA: MWANASIASA MKONGWE NA MWANZILISHI WA CHAMA CHA CUF AFARIKI DUNIA

> Mzee James Mapalala amefariki dunia leo katika hospitali ya Kairuki

> Alilazwa wiki 2 zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi katika mfumo wa upumuaji

Zaidi, soma > https://jamii.app/RIPMapalala
MAADHIMISHO YA JAMHURI: RAIA WA KENYA KUPITIA 'YOUTUBE' WAKERWA NA UCHAKAVU WA NDEGE ZAO ZA JESHI

- Wananchi wa taifa hilo kupitia mtandao wa 'YouTube' wameitupia lawama Serikali yao kwa kushindwa kununua ndege mpya na za kisasa licha ya fedha kuwepo

Soma > https://jamii.app/KenyaNdege
NI KWELI KUNA WATU UKIWA NAO KIMAPENZI HULETA MIKOSI/NUKSI?

> Kumekua na kasumba au dhana fulani ambayo imejengeka katika jamii kuwa kuna watu ukiwa nao kwenye mahusiano basi wanaweza kukusababishia mikosi au nuksi

> Mfano, mwanaume unaweza ukawa upo vizuri kiuchumi ikatokea ukaingia kwenye mahusiano na mwanamke fulani baada ya muda unajikuta unaanza kufilisika na kuhisi labda mtu ulienae ndio kisababishi. Na kwa wanawake pia kinyume chake

> Yawezekana umewahi kusikia hii kitu au wengine imewahi kuwatokea. Tupeni uzoefu katika hili. Je, hii hali ipo kweli au porojo?

Kujadili zaidi - https://jamii.app/MikosiNuksiMapenzi
#JFMahusiano
KWANINI VIONGOZI WASTAAFU BADO WANAPEWA KAZI BADALA YA KUACHWA WAPUMZIKE?

> Mdau aliyeleta hoja hii ndani ya JamiiForums anasema, kuna Watanzania wengi wenye kiu ya kuitumikia Serikali

> Anasema, tujenge utaratibu wa kuwapa nafasi watu wapya

Soma > https://jamii.app/HojaWastaafu
#JFLeo
KOREA KASKAZINI KUVUNJA HOTELI ILIYOJENGWA NA KOREA KUSINI

> Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameamuru kuvunjwa kwa hoteli na miundombinu ya utalii iliyojengwa na Korea Kusini eneo la Kaskazini ya nchi hiyo

> Asema imekosa mvuto na haiakisi taswira ya Korea Kaskazini

Soma - https://jamii.app/KimOrdersDemolitionHotelsSK