JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
IKULU: RAIS MAGUFULI AFANYA TEUZI MBALIMBALI

- Miongoni mwao, Mathias Kabunduguru ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania

- Pia, amemteua Hashim Abdallah Komba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea akichukua nafasi ya Rukia Muwango

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliTeuziMbalimbali
VIONGOZI 99 WA AMCOS MBARONI KWA KUWADHULUMU WAKULIMA

- Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inawashikilia viongozi 99 wa Vyama 31 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) wanaodaiwa kuwadhulumu Wakulima wa ufuta Tsh. Bilioni 1.2

Zaidi, soma https://jamii.app/Viongozi99AMCOSMbaroni
LIGI KUU ENGLAND: CHELSEA YASHINDA, TOTTENHAM YABANWA

- Michezo kadhaa za Ligi Kuu za mzunguko wa 9 zimemaliza huku klabu ya Tottenham ikiwa nyumbani ikitoka sare ya goli 1-1 na klabu ya Watford

- Klabu ya Chelsea ikiwa nyumbani imepata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Newcastle United huku Leicester City nayo ikipata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Burnley
UINGEREZA: WABUNGE WAPIGA KURA KUCHELEWESHA MPANGO WA BREXIT

> Wabunge wamepiga kura 322 dhidi ya 306 za kuchelewesha mpango wa Waziri Mkuu, Boris Johnson wa kujiondoa Umoja wa Ulaya

> Wametaka muda zaidi kusoma na kuyaelewa vizuri yaliyomo ndani ya mpango huo kabla ya tarehe ya mwisho, Oktoba 31

Soma - https://jamii.app/UKMPsDelayBrexit
LEBANON: WANANCHI WAANDAMANA KUIPINGA SERIKALI

- Maelfu ya Waandamanaji wameingia katika mitaa ya Lebanon jana, ikiwa ni siku ya tatu ya maandamano ya kuipinga Serikali, wakiwalenga vingozi wao juu ya kuporomosha Uchumi

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamanoLebanon
MDAU: MKE WANGU NI LAZIMA AMPENDE MAMA YANGU

- Mdau wa JamiiForums anaeleza kuwa sababu zinazoweza kumfanya akamfukuza mke wake bila hata kuwaza mara mbili ni pale atakapogundua mama yake anateswa na Mkewe

- Anadai mkewe hawezi kumchezea Mwanamke ambaye bila yeye asingekuwepo alipo sasa na pengine hata huyo mke asingemfahamu kama isingekuwa kuzaliwa na kulelewa na huyo Mwanamke

Kujadili, tembelea https://jamii.app/MkeVsMamaMkwe
BARRICK NA TANZANIA ZAUNDA KAMPUNI YA UBIA

- Waziri Prof. Palamagamba Kabudi amesema Serikali na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni inayoitwa Twiga Minerals Corporation

- Katika kampuni hiyo Serikali ina hisa 16% na Barrick 84%

Zaidi, soma https://jamii.app/Kampuni-SerikaliBarrick
IKULU: RAIS MAGUFULI KUWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA

- Majira ya saa tisa na nusu, Rais Magufuli anatarajiwa kuwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua jana

- Miongoni mwa viongozi atakaowaapisha ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama

Fuatilia https://jamii.app/UapishoViongozi-Okt20
IKULU: RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI

- Amemwapisha Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania

- Aidha, amemwapisha Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na Ali Sakila kuwa Balozi

Zaidi, soma https://jamii.app/UapishoViongozi-Okt20
KASHMIR: WATU 7 WAUAWA KWENYE MAPIGANO YA INDIA NA PAKISTAN

> Makabiliano kati ya wanajeshi wa Pakistan na India ktk eneo la Kashmir yamesababisha mauaji ya watu 7 kutoka pande zote mbili

> India imeyaita mashambulizi hayo kama hujuma isiyozuilika inayokiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwaka 2003 kati ya India na Pakistan

Soma - https://jamii.app/DeathKashmirAttack
MAREKANI: Baadhi ya Washindi wa tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA), zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Jumapili ya Oktoba 20, 2019 nchini Marekani

- Tuzo hizo zinazotolewa kila mwaka zilianza kutolewa Mwaka 2015 zikiheshimu ubora katika nyanja mbalimbali hususan Burundani, Uongozi wa Kijamii na Ujasiriamali ndani ya bara la Afrika
UN: ZAIDI YA WATOTO NA VIJANA MILIONI 1.3 DUNIANI KOTE NI WAFUNGWA

> Ripoti iliyotolewa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa imesema kiasi cha watoto na vijana milioni 1.3 wako kizuizini ambapo kati yao 410,000 wapo chini ya umri wa miaka 18

> Vijana 330,000 wako kizuizini ulimwenguni kote wakihusishwa na uhamiaji haramu

Soma - https://jamii.app/RipotiWatotoWafungwa
MAREKANI: DAKTARI AKIRI KUUA KWA UZEMBE MTU ALIYETAKA KUONGEZA MAKALIO

> Donna Francis amekiri mashtaka ya mauaji yaliyotokana na uzembe wakati wa kumfanyia upasuaji mwanamke (34) ambaye alienda kwake kwa ajili ya kuongeza makalio

> Tukio hilo lilitokea Mei 2015, ambapo mgonjwa alipatwa na mshtuko wa moyo baada ya kuchomwa dawa husika

Soma - https://jamii.app/DeathBotchedButt
TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA MAWAZIRI SEKTA ZA MAZINGIRA, MALIASILI NA UTALII SADC

> Mkutano huo unafanyika jijini Arusha na utajadili mwenendo wa hali ya mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na hali ya utalii na misitu katika nchi za SADC

> Pia, utajadili juu ya utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira

Soma - https://jamii.app/MkutanoSADCMazingira
MWILI WA KIJANA WAKUTWA VICHAKANI BAADA YA KUPOTEA KWA SIKU 8

> Mwili wa Noel Jengeni Mlilo (27) umepatikana kichakani ukiwa na jeraha mgongoni ambalo linaonesha kusababishwa na kitu chenye ncha kali

> Pia, mwili wake ulionesha hali ya kukosa hewa na kuachana kwa mifupa ambayo ilisababishwa na mkabo uliokusudiwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili

Soma - https://jamii.app/MwiliWaokotwaKichakani
TBS YAONDOA VIPODOZI AINA 16 VYENYE SUMU SOKONI

> Vipodozi vilivyoondolewa vinaelezwa kuwa na viambata vyenye sumu hivyo kuhatarisha afya kwa watumiaji.

> Baadhi ni Carolight, Movate, Diproson,Viva White, Bronz na Eclair, Citrolight, Tent Clear, Light up, Dermotyl na Top Lemon

Soma - https://jamii.app/TBSVipondoziSumu