JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MACHAFUKO CHILE: ABIRIA WAZUILIWA UWANJA WA NDEGE WA SANTIAGO NA SAFARI ZAFUTWA

> Safari hizo zimesitishwa kutokana na vurugu zinazoendelea kwa siku 3 mfululizo na kusababisha vifo vya watu 7 mpaka sasa

> Serikali imetangaza hali ya dharura katika Majimbo matano, ikiwa ni pamoja na Mji Mkuu wenye wakaazi milioni 7

Soma - https://jamii.app/SantiagoFlightsSuspended
AJALI YA NYUMBA KUUNGUA: WATOTO WAWILI WAPOTEZA MAISHA

> Jaksoni Kebini (4) na Deograta Kebini (1) wakazi wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera wameteketea kwa moto baada ya kibatari kusababisha nyumba yao kuungua wakati wakiwa wamelala

> Wazazi wao walikuwa kwenye biashara wakati ajali hiyo ikitokea

Soma - https://jamii.app/VifoNyumbaMoto
USHAURI KWA TRA: WANAOAGIZA MIZIGO NJE WAPEWE UNAFUU KATIKA KULIPA KODI
-
Mdau wa JamiiForums.com anasema TRA iwape nafuu wafanyabiashara wanaoagiza mizigo nje, baada ya makadirio ya kodi wapewe nafasi ya kulipa kwa awamu au muda hata miezi sita katika kumaliza kulipa hiyo kodi
-
Anaongeza kuwa, kama wanavyofanya kwenye makadirio ya Kodi ya mwaka kwamba unalipa kwa awamu nne basi ifanye na hapa pia kwani itawasaidia wafanyabiashara na wananchi wa kawaida kuweza kufikia malengo yao na kukuza uchumi
-
Anasema, baadhi ya bidhaa kutoka nje huuzwa kwa bei ndogo lakini kodi inakuwa kubwa zaidi hata ya mara mbili ya bei ulionunulia. Serikali iangalie hili ili kuwapa unafuu wa maisha wananchi wake

Tembelea - https://jamii.app/HojaMalipoKodiMizigo
#JFHoja
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MOROGORO: MKUU WA MKOA AAGIZA KUKAMATWA WATUMISHI 5

> RC Loata Ole Sanare, ametaka watumishi hao wahojiwe kwa tuhuma za matumizi mabaya ya edha za ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Mkuyuni na hospitali ya Wilaya ya Mvomero

Zaidi, soma => https://jamii.app/RCMoroWatumishi
TAARIFA KUHUSU KUKATIKA KWA UMEME
-
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kukatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Ilala na Temeke, jijini Dar es Salaam kesho, Oktoba 22 kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi 10:30 jioni
-
Maeneo yatakayokumbwa na usumbufu huo ni pamoja na Buguruni, Vingunguti, Tazara, Gongo la Mboto, Ukonga, Mombasa, Mzambarauni, Pugu, Yombo, Kitunda, Machimbo, Mwanagati, Mbondole pamoja na baadhi ya maeneo ya Tabata
KALIIRO, UGANDA: WANAFAMILIA 3 WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI

> Waliouawa ni Francis Rwabagabo(60), Mkewe Kellen Nakato(38) na Mkwe wao Leokadia Kizza

> Mtoto wa Kiume wa Rwabagabo aitwaye Mwebaze anatuhumiwa kuhusika

Zaidi, soma => https://jamii.app/MauajiLyantondeUG
KISUTU, DAR: MAHAKAMA YATAKA HAKI ITENDEKE KATIKA KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU

> Godfrey Gugal pamoja na wenzake wanatuhumiwa kwa kumiliki mali zeye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 3.6 kinyume na kipato chake halali

Zaidi, soma => https://jamii.app/KesiMhasibuPCCB
RUVUMA: BINTI WA MIAKA 26 AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA 'BOYFRIEND' WAKE

> Aliyeuawa ni Beata Kafuru aliyepigwa risasi 3 za kichwani na James Paul (27), anayeelezwa kuwa ni mpenzi wake

> Chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi

Soma > https://jamii.app/RIPBeataKafuru
AFYA: FAIDA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO YENYE LIMAO ASUBUHI

> Maji hayo huongeza Kinga ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo, husafisha mfumo wa chakula, na kuondoa sumu mwilini

> Pia, huleta hewa/harufu safi kinywani

Kwa faida zaidi, soma => https://jamii.app/MajiLimao
#JFAfya
Treni imeacha njia maeneo ya Buguruni Chama na kusababisha msongamano mkubwa.

> Dereva unayetumia njia hiyo asubuhi hii, unashauriwa kutumia njia mbadala

Fuatilia zaidi > https://jamii.app/TreniImeachaNjiaBuguruni
KENYA: SERIKALI YAONDOA AMRI YA KUFUNGWA KWA TAASISI YA 'MARIE STOPES'

> Serikali ya Kenya imeondoa marufuku hiyo baada ya takwimu kuonesha kuwa Wanawake 320 wanalazwa na 7 wanafariki kila siku kwa kujaribu kutoa mimba kiholela

Zaidi, soma > https://jamii.app/MarieStopesKenya
IPTL INADAI FIDIA YA TSH. TRILIONI 6.5 BENKI YA STANDARD CHARTERED

> IPTL imeiomba Mahakama Kuu itamke rasmi kwamba Standard Chartered Bank (Hong Kong) si wadai wake na ibatilishe tuzo ilizopewa Ulaya bila kuwepo mhusika mkuu katika migogoro hiyo

> IPTL imeifungulia SCBHK kesi mbalimbali za madai ktk Mahakama Kuu, Dar

Soma - https://jamii.app/IPTLKudaiFidiaSCBHK
NDEGE YA AUSTRALIA YAFANYA MAJARIBIO YA SAFARI NDEFU BILA KUSIMAMA

- Qantas imekamilisha safari yake ya kibiashara ya maili 10,066 bila kusimama, ikifanya utafiti wa athari za safari ndefu zinazoweza kutokea kwa Marubani, Wafanyakazi na Abira

Soma https://jamii.app/NdegeAustraliaSafariNdefu
KENYA: AJISALIMISHA POLISI BAADA YA KUMUUA MWENZAKE WAKIGOMBEA KUMBIKUMBI

> Muriungi Kiyogere (35), mkazi wa Kaunti ya Tharaka-Nithi anadaiwa kumchoma kisu mara nne Daniel Mutiria Cece (36), kutokana na mzozo wa kugombea Kumbikumbi Jumapili jioni

> Alikimbilia Polisi kuwakwepa wanakijiji waliokuwa wakitaka kumuua

Soma - https://jamii.app/KifoUgomviKumbikumbi
HOJA: JE, NI AIBU KWA KIJANA MWENYE MIAKA ZAIDI YA 35 KUISHI KWA WAZAZI WAKE?

> Mdau wa JamiiForums anasema anasema wazazi wanashindwa kuishi kwa uhuru kwa sababu ya uwepo wako

> Anahoji, unawezaje kuendelea kula ugali wa shikamoo kwa umri huo?

Shiriki mjadala, hapa > https://jamii.app/JFHoja
UMUHIMU WA KUWASILIANA NA MWANAO

> Iwapo wazazi watadumisha mawasiliano ya karibu na watoto, hapatakuwa na haja ya kutumia nguvu nyingi kumjenga mtoto

> Tumia muda kuwasimulia watoto hadithi za chimbuko la familia yao. Hii itawapa nafasi ya kujivunia utu wao

> Jenga tabia ya kuandikiana jumbe za maneno kwenye karatasi. Hii inakupa fursa ya kujua kama anaweza kusoma na vilevile utapata kuuona mwandiko wake

> Kuwa na subira katika maongezi na mwanao. Mvumilie na jitahidi usiwe mwongeaji sana bali msikilizaji

Zaidi, soma - https://jamii.app/MbinuMawasilianoMtoto
#JFMalezi
MADHARA YA MVUA AFRIKA MASHARIKI: WATU 105 WAPOTEZA MAISHA

> Nchini Tanzania, takriban watu 16 wamefariki, Sudan Kusini, watu zaidi ya 200,000 wameathiriwa na Kenya, zaidi ya watu 1,000 wameyakimbia makazi yao

> Rwanda, watu 70 wamefariki na 177 kujeruhiwa. Nyumba 4,095 na hekta 6,708 zimeharibiwa huku wanyama 167 wakifa

Soma - https://jamii.app/MadharaMvuaEAC
CCM YAFUTA KURA ZA MAONI BAADHI YA SEHEMU, UCHAGUZI KURUDIWA

> Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema kumekuwa na madai ya rushwa, upendeleo na kanuni za kuchuja wagombea hazikuzingatiwa kwenye baadhi ya maeneo

> Pia, kulikuwa na rafu za kuchomoa majina kwenye masanduku ya kura na masanduku kubomolewa

Soma - https://jamii.app/MarudioKuraMaoniCCM
RUKWA: RC AAGIZA KUKAMATWA KWA WALIMU 2 WANAOTUHUMIWA KUBAKA NA KUWAPA MIMBA WANAFUNZI

> RC Joachim Wangabo ameagiza kukamatwa kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya, Dastan Mlelwa na Mwalimu mmoja wa Shule ya Sekondari Mpui

Zaidi, soma => https://jamii.app/RCRukwaVsWalimu
ZIMBABWE: TEMBO 55 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA UKAME

> Tembo 55 wamekufa njaa tangu Septemba 2019 katika Mbuga ya Taifa ya Hwange kutokana na ukame wa zaidi ya miezi 2

> Theluthi moja ya watu nchini humo wameripotiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula

Soma - https://jamii.app/UkameVifoTembo