JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WAZIRI MKUU: VIWANDA 4,000 VIMEJENGWA NDANI YA AWAMU YA 5

> Amesema tangu Serikali ya Awamu ya 5 iingie madarakani, viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa na kufanya sekta hiyo kuchangia Pato la Taifa kwa 8.05% na kutoa ajira 306,180 mwaka 2018

> Aidha, Sekta ilichangia 18.1% ya mauzo yote ya nje, ikilinganishwa na 15% mwaka 2017

Soma - https://jamii.app/UjenziViwandaAwamu5
WAZIRI MAHIGA: KOMPYUTA ZILIZOIBWA SI ZA OFISI YA DPP

> Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Kompyuta zilizoibwa ni za Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Dar na sio Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini Tanzania, Biswalo Mganga
RUKWA: MUME AHUKUMIWA KWENDA JELA KWA UBAKAJI, MKE AJINYONGA KWA UCHUNGU

> Shija Lutoja(23) amejinyonga huku akiacha ujumbe kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na uchungu mkubwa alioupata baada ya mumewe kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la ubakaji

> Sababu nyingine ya kujinyonga ni baada ya kupimwa na kubainika kuwa na maambukizi ya VVU

Soma - https://jamii.app/MeUbakajiKeAjinyonga
MUSEVENI: BOBI WINE NI ADUI WA MAENDELEO UGANDA

- Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema anamshughulikia Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) kama adui

- Amemlaumu Bobi Wine akisema alikwenda Marekani na kuwaambia watu wasiende kuwekeza Uganda

Zaidi, soma https://jamii.app/Museveni-BobiWineAduiUG
MWANZA: MAFURIKO YACHIMBUA MAKABURI

- Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa moja jana, yamefukua zaidi ya makaburi 20 ya Waislam eneo la Mswahili katika Kata ya Mkuyuni

Zaidi, soma https://jamii.app/MafurikoYachimbuaMakaburi-MWZ
LIGI KUU ENGLAND: EVERTON YAPATA USHINDI WA 3 KATIKA LIGI

- Klabu ya Everton imefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Klabu ya West Ham katika mchezo wa Ligi Kuu, mzunguko wa 9

- Michezo mingine inayofuata kwenye Ligi hiyo siku ya leo ni kama ionekanavyo kwenye picha
WHO: MAAMBUKIZI YA EBOLA DRC YAPUNGUA, HALI BADO SIO SALAMA

> Takwimu zinaonesha idadi ya wagonjwa sasa ni 3,228 na kati ya hao 3,114 wamethibitishwa kuugua na 114 wanashukiwa kuwa na maambukizi

> Changamoto kubwa ni ukosefu wa fedha, kwani kati ya dola zaidi ya milioni 66.6 zinazohitajika kukabiliana na ugonjwa huo, ni dola milioni 4.5 zilizoahidiwa

Soma - https://jamii.app/WHOMaambukiziEbola
IKULU: RAIS MAGUFULI AFANYA TEUZI MBALIMBALI

- Miongoni mwao, Mathias Kabunduguru ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania

- Pia, amemteua Hashim Abdallah Komba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea akichukua nafasi ya Rukia Muwango

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliTeuziMbalimbali
VIONGOZI 99 WA AMCOS MBARONI KWA KUWADHULUMU WAKULIMA

- Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inawashikilia viongozi 99 wa Vyama 31 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) wanaodaiwa kuwadhulumu Wakulima wa ufuta Tsh. Bilioni 1.2

Zaidi, soma https://jamii.app/Viongozi99AMCOSMbaroni
LIGI KUU ENGLAND: CHELSEA YASHINDA, TOTTENHAM YABANWA

- Michezo kadhaa za Ligi Kuu za mzunguko wa 9 zimemaliza huku klabu ya Tottenham ikiwa nyumbani ikitoka sare ya goli 1-1 na klabu ya Watford

- Klabu ya Chelsea ikiwa nyumbani imepata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Newcastle United huku Leicester City nayo ikipata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Burnley
UINGEREZA: WABUNGE WAPIGA KURA KUCHELEWESHA MPANGO WA BREXIT

> Wabunge wamepiga kura 322 dhidi ya 306 za kuchelewesha mpango wa Waziri Mkuu, Boris Johnson wa kujiondoa Umoja wa Ulaya

> Wametaka muda zaidi kusoma na kuyaelewa vizuri yaliyomo ndani ya mpango huo kabla ya tarehe ya mwisho, Oktoba 31

Soma - https://jamii.app/UKMPsDelayBrexit
LEBANON: WANANCHI WAANDAMANA KUIPINGA SERIKALI

- Maelfu ya Waandamanaji wameingia katika mitaa ya Lebanon jana, ikiwa ni siku ya tatu ya maandamano ya kuipinga Serikali, wakiwalenga vingozi wao juu ya kuporomosha Uchumi

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamanoLebanon
MDAU: MKE WANGU NI LAZIMA AMPENDE MAMA YANGU

- Mdau wa JamiiForums anaeleza kuwa sababu zinazoweza kumfanya akamfukuza mke wake bila hata kuwaza mara mbili ni pale atakapogundua mama yake anateswa na Mkewe

- Anadai mkewe hawezi kumchezea Mwanamke ambaye bila yeye asingekuwepo alipo sasa na pengine hata huyo mke asingemfahamu kama isingekuwa kuzaliwa na kulelewa na huyo Mwanamke

Kujadili, tembelea https://jamii.app/MkeVsMamaMkwe
BARRICK NA TANZANIA ZAUNDA KAMPUNI YA UBIA

- Waziri Prof. Palamagamba Kabudi amesema Serikali na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni inayoitwa Twiga Minerals Corporation

- Katika kampuni hiyo Serikali ina hisa 16% na Barrick 84%

Zaidi, soma https://jamii.app/Kampuni-SerikaliBarrick
IKULU: RAIS MAGUFULI KUWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA

- Majira ya saa tisa na nusu, Rais Magufuli anatarajiwa kuwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua jana

- Miongoni mwa viongozi atakaowaapisha ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama

Fuatilia https://jamii.app/UapishoViongozi-Okt20
IKULU: RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI

- Amemwapisha Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania

- Aidha, amemwapisha Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na Ali Sakila kuwa Balozi

Zaidi, soma https://jamii.app/UapishoViongozi-Okt20
KASHMIR: WATU 7 WAUAWA KWENYE MAPIGANO YA INDIA NA PAKISTAN

> Makabiliano kati ya wanajeshi wa Pakistan na India ktk eneo la Kashmir yamesababisha mauaji ya watu 7 kutoka pande zote mbili

> India imeyaita mashambulizi hayo kama hujuma isiyozuilika inayokiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwaka 2003 kati ya India na Pakistan

Soma - https://jamii.app/DeathKashmirAttack
MAREKANI: Baadhi ya Washindi wa tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA), zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Jumapili ya Oktoba 20, 2019 nchini Marekani

- Tuzo hizo zinazotolewa kila mwaka zilianza kutolewa Mwaka 2015 zikiheshimu ubora katika nyanja mbalimbali hususan Burundani, Uongozi wa Kijamii na Ujasiriamali ndani ya bara la Afrika