JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MUUGUZI ADAIWA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 16 ALIYEKUWA AKIMUUGUZA MAMA YAKE

- Ni katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora

- Mganga Mkuu wa Wilaya, Dr. Ruta Deus amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Oktoba 10, 2019

Soma https://jamii.app/MuuguziAbakaBintiMiaka16
WANAFUNZI 30,675 KUNUFAIKA NA MKOPO KWA AWAMU YA KWANZA 2019/20

- Mkopo wenye thamani ya Tsh. Bilioni 113.5 umetolewa kwa Wanafunzi wa mwaka wa kwanza

- Wanafunzi waliopata mkopo wanatakiwa kuingia katika akaunti zao walizoombea mkopo

Zaidi, soma https://jamii.app/MkopoAwamu1-2019-20
SERIKALI YASEMA HAIHUSIKI NA HUKUMU ILIYOTOLEWA NA BARAZA LA ICSID

> Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, amesema Serikali haihusiki na hukumu iliyotolewa na Baraza la Kimataifa la Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICSID), ambayo imetaka Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) Ltd ilipwe dola milioni 185

> Amesema Msingi wa kesi zote mdaiwa si Serikali wala TANESCO ila ni deni la benki dhidi ya IPTL

Soma - https://jamii.app/SerikaliHaidaiwiIPTL
NDAYIRAGIJE: TANZANIA ‘TUTAPINDUA MEZA’ KWA SUDAN

- Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Etienne Ndayiragije amewatoa wasiwasi mashabiki wa Stars kwa kusema wana kila sababu ya kupindua matokeo kutokana na maandalizi

Zaidi, soma https://jamii.app/StarsKuifungaSudan
KENYA: RAIS KENYATTA AVUNJA BODI YA HUDUMA ZA FERI

- Rais Uhuru Kenyatta ametengua uteuzi wa Wanabodi watano wa Bodi hiyo hapo jana Oktoba 17, ikiwa ni takriban wiki tatu zimepita baada ya ajali ya mama na mtoto kuzama katika Feri ya Likoni

Zaidi, soma https://jamii.app/KFSBoardMembersSacked
WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI: RUFAA KUKATWA MAHAKAMA YA AFRIKA

- Baada ya Mahakama ya Rufaa kutengua zuio la Wakurugenzi wa Halmashauri na Majiji kusimamia uchaguzi, Bob Wangwe amesema atakata rufaa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu

Zaidi, soma https://jamii.app/Ma-DEDKesiRufaaAfrika
UINGEREZA: MAKUBALIANO MAPYA YA BREXIT KUJADILIWA KESHO BUNGENI

- Uingereza na Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano mapya yatakayofungua njia kwa nchi hiyo kujitoa katika Umoja huo Oktoba 31, lakini makubaliano hayo tayari yameanza kukosolewa na Wabunge wa nchi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/MajadilianoMapyaBrexit
LINDI: MBARONI KWA KUPANDISHA BENDERA YA CHAMA PINZANI BARABARANI

- Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Ruangwa, Erasmus Libaba amehojiwa kwa kupandisha bendera ya chama hicho katika barabara ambayo viongozi wa Serikali wanapita katika msafara

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniBenderaUpinzani
Radi imewajeruhi wanafunzi 39 wa Darasa la Nne katika Shule ya Msingi Ihumilo iliyopo Wilayani Geita, wakati wakiwa Darasani

> Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Soma > https://jamii.app/WanafunziWajeruhiwaNaRadi
CHALAMILA ATAKA KUWACHAPA VIBOKO WASIOOA AU KUOLEWA

- RC wa Mbeya, Albert Chalamila amesema atakuja na mpango wa kuwacharaza bakora Wanawake na Wanaume mkoani kwake ambao hawajaoa au kuolewa na kisha wakatafute wapenzi wa kufunga nao ndoa

Zaidi, soma https://jamii.app/BakoraWasiooaWasioolewa-MBY
AFGHANISTAN: MLIPUKO WATOKEA MSIKITINI. TAKRIBANI WATU 31 WAUAWA

- Wengine 55 wamejeruhiwa leo, ikiwa ni siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kusema vurugu nchini humo zimefikia kiwango kisichokubalika

Zaidi, soma https://jamii.app/31KilledAfghanistan
ALI MUFURUKI AJIUZULU UENYEKITI BODI YA WAKURUGENZI VODACOM

> Ametangaza kujiuzulu wadhifa huo kuanzia Desemba 1, 2019 na pia ametangaza kujiuzulu nafasi za Mkurugenzi huru na kamati ya uteuzi wa kampuni hiyo

> Imeelezwa kuwa amechukua uamuzi huo ili kupata muda zaidi wa kuendelea na biashara zake

Soma https://jamii.app/MufurukiResignsVoda
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: DAR YAVUKA LENGO UANDIKISHAJI WAPIGA KURA

Mikoa iliyoongoza ni Dar 108%, Pwani 96%, Mwanza 95%, Tanga 90% na Singida 90%

Jumla ya wapiga kura 19,681,259 wamejiandikisha nchi nzima ikiwa ni 86% ya lengo (22,916,412)

Soma https://jamii.app/UandikishajiSrklMitaa
CHAN: TAIFA STARS YAPINDUA MEZA SUDAN

> Taifa Stars imefuzu kucheza michuano ya CHAN 2020 nchini Cameroon baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Sudan na kufuzu kwa faida ya goli la ugenini

> Magoli ya Tanzania kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Nyoni 49’ na Nchimbi 78’
ANAYEDAIWA KUMBAKA ALIYEKUWA AKIMUUGUZA MAMAYE, ASIMAMISHWA KAZI

- Leseni ya Uuguzi ya Damian Mgaya (41), aliyemchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka kwa saa nne msichana mwenye umri wa miaka 16, imesimamishwa kwa miezi mitatu

Zaidi, soma https://jamii.app/MuuguziAbakaAsimamishwaKazi
RUVUMA: KAKA AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUMUUA MDOGO WAKE

> Mohamed Luambano(70) anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata na kitu chenye ncha kali kichwani na kiganjani Abeid Luambano(65)

> Ni kutokana na madai kwamba siku za hivi karibuni kumekuwapo na kutoelewana kati ya ndugu hao

Soma - https://jamii.app/KakaMauajiNdugu
WAZIRI MKUU: VIWANDA 4,000 VIMEJENGWA NDANI YA AWAMU YA 5

> Amesema tangu Serikali ya Awamu ya 5 iingie madarakani, viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa na kufanya sekta hiyo kuchangia Pato la Taifa kwa 8.05% na kutoa ajira 306,180 mwaka 2018

> Aidha, Sekta ilichangia 18.1% ya mauzo yote ya nje, ikilinganishwa na 15% mwaka 2017

Soma - https://jamii.app/UjenziViwandaAwamu5
WAZIRI MAHIGA: KOMPYUTA ZILIZOIBWA SI ZA OFISI YA DPP

> Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Kompyuta zilizoibwa ni za Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Dar na sio Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini Tanzania, Biswalo Mganga
RUKWA: MUME AHUKUMIWA KWENDA JELA KWA UBAKAJI, MKE AJINYONGA KWA UCHUNGU

> Shija Lutoja(23) amejinyonga huku akiacha ujumbe kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na uchungu mkubwa alioupata baada ya mumewe kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la ubakaji

> Sababu nyingine ya kujinyonga ni baada ya kupimwa na kubainika kuwa na maambukizi ya VVU

Soma - https://jamii.app/MeUbakajiKeAjinyonga
MUSEVENI: BOBI WINE NI ADUI WA MAENDELEO UGANDA

- Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema anamshughulikia Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) kama adui

- Amemlaumu Bobi Wine akisema alikwenda Marekani na kuwaambia watu wasiende kuwekeza Uganda

Zaidi, soma https://jamii.app/Museveni-BobiWineAduiUG