JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MATOKEO DARASA LA 7, 2019 YATANGAZWA. UFAULU WAONGEZEKA

- NECTA imetangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2019 na kusema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78

- Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 na Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kutokana na sababu mbalimbali

Zaidi, soma https://jamii.app/MatokeoSTD7-2019
KENYA: WANAFAMILIA WATATU WAFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO

- Mtoto 1 na wanafamilia wengine wawili wamefariki baada ya nyumba yao kuwaka moto huko Kariobangi, Nairobi

- Wanafamilia wengine wawili wamekimbizwa ktk hospitali ya Taifa ya Kenyatta

Zaidi, soma https://jamii.app/Wanafamilia3Wafariki-Moto
MICHEZO: Bondia wa Marekani, Patrick Day (27) yupo mahututi baada ya kupigwa akiwa ulingoni katika roundi ya 10 na mpinzani wake Charles Conwell
-
Patrick alipata majeraha makubwa katika ubongo hali iliyopelekea kupoteza fahamu mpaka sasa ambapo amelazwa katika hospitali ya Northwestern Memorial nchini Marekani, ambapo amefanyiwa operesheni ya kichwa
-
Imeripoti kuwa, Patrick mpaka sasa yupo kwenye ‘Coma’ (fahamu hazijarejea) tangu alipopigwa usiku wa Jumamosi
MASHAMBULIZI YA UTURUKI, SYRIA: MAREKANI YAIWEKEA VIKWAZO UTURUKI

> Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Wizara mbili za nchini Uturuki na Maafisa 3 wa Serikali, kutokana na Operesheni ya Kijeshi inayoendelea Kaskazini mwa Syria dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi

> Rais Donald Trump amemtaka Rais wa Uturuki asitishe operesheni hiyo mara moja

Soma - https://jamii.app/TrumpTurkishAttack
TAMISEMI: PWANI KINARA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA

- Mkoa unaoongoza uandikishaji kwenye Daftari la Mpiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Pwani

- Lakini Mikoa ya Dar, Arusha na Kilimanjaro uandikishaji wao uko chini ya 50%

Zaidi, soma https://jamii.app/PwaniKinaraUandikishajiKura
FAHAMU KUHUSU MNYAMA PANYA

> Panya hawaoni vizuri, hivyo hutumia uwezo wao mkubwa wa kusikia, kunusa harufu, kuhisi kupitia miguu kwaajili ya kutambua mazingira na hali ya eneo ambalo yupo

> Meno ya Panya huongezeka kila siku hivyo ili kupunguza kukua kwa kiasi kikubwa huwa na kawaida ya kupenda kujisugua katika vitu vigumu ili kupunguza urefu na hapa ndio utakuta ametafuna rimoti, waya, ndoo, nguo

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/UfahamuPanya
#JFMaarifa
UGANDA: HAKUNA MPANGO WA SHERIA YA KIFO KWA MASHOGA

- Imesema haina mpango wa kuweka adhabu ya kifo dhidi ya wanaoshiriki Mapenzi ya Jinsia Moja

- Ni baada ya Nchi wahisani kusema zinafuatilia nia ya Nchi hiyo kurejesha muswada huo

Soma https://jamii.app/UgandaSheriaKuuaMashoga
MATOKEO DARASA LA 7: Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2019

- Limetangaza pia Watahiniwa 10 waliofanya vizuri Kitaifa, Mikoa 10 iliyofanya vizuri na Shule 10 zilizofanya vizuri Kitaifa

Zaidi, soma https://jamii.app/MatokeoSTD7-2019
MOROGORO: MVUA YASABABISHA VIFO VYA WATU 11

> Mvua za Vuli zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha vifo vya watu 11 Mkoani Morogoro huku kati yao watoto wakiwa ni 9

> Watoto watano kati yao walifariki baada ya kuzama Mto Mvuha uliopo Kata ya Kibogwa

Soma - https://jamii.app/Vifo11MvuaMoro
JE, WANAUME WENGI HUFA MAPEMA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO UNAOSABABISHWA NA WANAWAKE?

> Katika utafiti uliowahi kufanywa ulibaini kwamba tabia ya kujihatarisha na kukandamiza mihemko ya kihisia kwa vijana wa kiume, inahusiana moja kwa moja na vifo vya mapema vya wanaume ukilinganisha na wanawake

> Tabia hizo ni Ugumu katika kufunguka, Ugumu wa kusamehe, Msongo wa mawazo, kutokujali afya na Tabia hatarishi. Inadaiwa Wanaume wengi wana maradhi ya kihisia kuliko wanawake

Kwa mjadala zaidi - https://jamii.app/VifoMeMsongoMawazo
#JFMahusiano
MBARONI KWA KUJIANDIKISHA MARA 2 KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

- Ni Ngeze Mwagilo (29), Mkazi wa Kasanga Manispaa ya Morogoro

- Anadaiwa kujiandikisha katika Kituo cha Kasanga na kisha kwenda kujiandikisha katika Kituo cha Kiwanja cha Ndege

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniUandikishaji2-Moro
MALAWI YAKANUSHA KUWA NA MGONJWA WA EBOLA

> Mamlaka ya Afya imekanusha ripoti ya kwamba mtu amegunduliwa kuwa na Ebola kwenye eneo la Karonga linalopakana na Tanzania

> Ofisa wa Afya amesema mtu huyo alikuwa na maambukizi ya Bakteria na si Ebola

Soma - https://jamii.app/MalawiDenouncesEbola
KAMPUNI ZA BOEING NA PORSCHE ZAUNGANA KUUNDA MAGARI YA KUSAFIRI ANGANI

> Boeing ya Marekani na Porsche ya Ujerumani zimetia saini makubaliano (MoU) kwa ajili ya uundwaji wa magari ya umeme yatakayokuwa na uwezo wa kupaa na kutua wima (Vertical Take-off and Landing (VTOL)) ili kuingia katika soko la 'Taxi'

Soma - https://jamii.app/PorscheBoeingFlyingCars
AZAKI ZATAKIWA KUENDESHA SHUGHULI ZAO KWA UWAZI ILI KUPATA UNAFUU WA KODI

> Waziri wa Fedha amezitaka Asasi za Kiraia kuendesha shughuli zao kwa Uwazi na Uwajibikaji kwa kufuata Sheria za Nchi, Matakwa na Vigezo ili kupata unafuu wa kodi

> Pia, amezitaka kuwasilisha mapendekezo juu ya Sheria za Kodi ili kilio chao cha msamaha wa kodi kifanyiwe kazi

Soma - https://jamii.app/AZAKIUwaziKodi
SHIRIKA LA NDEGE LA SWISS LASIMAMISHA SAFARI ZA AIRBUS A220

> Shirika la Ndege la SWISS International Airlines limesimamisha safari za ndege zake zote aina ya Airbus A220 kutokana na matatizo ya injini zake aina ya PW 1500G zinazotengenezwa na Kampuni ya Pratt & Whitney ya Canada

Soma - https://jamii.app/SwissGroundsA220
TMA YATOA ANGALIZO LA KUWEPO KWA MVUA KUBWA UKANDA WA PWANI KWA SIKU 2

> Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa ktk Mikoa ya Tanga, Dar, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro na Visiwa vya Unguja na Pemba

> Mvua hizo zitaanza Oktoba 16 hadi Oktoba 17, 2019

Soma - https://jamii.app/TahadhariMvuaPwani
UFAHAMU NA ELIMU YA UGONJWA WA MAFINDOFINDO (TONSILS)

> Mafindofindo hujitokeza pale viungo viwili vidogo nyuma ya koo vinapozidiwa nguvu katika kupambana na wadudu wabaya ndani ya mwili

> Dalili zake ni Maumivu ya koo, maumivu wakati wa kufungua kinywa, ugumu katika kumeza mate/chakula, homa, kuvimba kwa Lymph Nodes kwenye shingo

> Tiba unayoweza kujipatia mwenyewe ni kunywa/kusukutua maji ya uvuguvugu kila mara (angalau mara 4 kwa siku) yenye chumvi, asali pamoja na ndimu/limao. Jambo hili huleta maumivu makali lakini utapona haraka

Soma - https://jamii.app/UgonjwaTonsils
#JFAfya