JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MAGUFULI: TUMEMUENZI NYERERE KWA KUFUFUA MASHIRIKA YA UMMA NA KUSIMAMIA NIDHAMU

> Amesema Serikali imefanya mambo mengi katika kumuenzi Baba wa Taifa ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu Serikalini, kuyafufua Mashirika ya Umma, kurejesha nidhamu katika Utumishi wa Umma na kulinda Rasilimali za Taifa

> Amesema jitihada zote zimelenga katika kuziishi fikra za Baba wa Taifa ambaye alilijenga Taifa katika misingi ya Ujamaa na Kujitegemea

Soma - https://jamii.app/MagufuliKumuenziNyerere
CUF: KUTOFANYIKA KWA MIKUTANO YA KISIASA NI SABABU YA WATU KUTOJIANDIKISHA KUPIGA KURA

> Chama cha Wananchi (CUF) kimesema mikutano ya kisiasa huhamasisha wananchi kujiandikisha na kujua umuhimu wa kufanya hivyo katika uchaguzi

> Sababu nyingine ni kufanyika kwa uchaguzi usio huru na haki, kupatikana kwa washindi wanaopita bila kupingwa na viongozi waliochaguliwa kuhama vyama vya upinzani na kwenda CCM

Soma - https://jamii.app/CUFUandikishajiKura
KENYA: MABAKI YA MIILI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA ETHIOPIAN AIRLINE YAWASILI

- Wakenya leo wamepokea mabaki ya miili ya wapendwa wao waliofariki katika ajali ya Ndege ya Ethiopia iliyoanguka mwezi Machi na kuwaua watu wote 157 waliokuwemo

Zaidi, soma https://jamii.app/MiiliWakenyaEthiopianAirline
MCHEZO WA KIRAFIKI: TAIFA STARS YATOKA SARE NA RWANDA

- Taifa Stars ikicheza bila ya nahodha wake, Mbwana Samatta imefanikiwa kutoka sare ya bila kufungana (0-0) na Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamirambo, Kigali

#JFLeo
MDAU: NI ‘UPUUZI’ KUTOA TSH. 300 ILI KUINGIA KITUO CHA MABASI CHA UBUNGO

- Mdau kutoka JamiiForums.com anadai haoni maana na faida ya kutoa Tsh. 300 kwa Waenda kwa miguu ili kuingia Kituoni hapo na kuhoji “Mbona Uwanja wa ndege hakuna kitu kama hicho?”

- Aidha, amedai kuwa suala hilo ni kero kubwa na linafanyika kienyeji sana na ushuru unakusanywa kiholela sana ndio maana hakuna maendeleo kwenye kituo hicho

Kushiriki mjadala, tembelea https://jamii.app/300UbungoTerminal
KUMBUKIZI: Passport-size ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1946 iliyowasilishwa pamoja na maombi yake kusoma Edinburgh, Scotland, United Kingdom

- Picha halisi imehifadhiwa The National Archives, United Kingdom
ALIYECHONGA KIFIMBO CHA MWALIMU NYERERE SASA ANACHONGA CHA MAGUFULI

- Mzee Omary Mwariko amesema lengo la kumkabidhi Rais Magufuli ni kama alama ya kumuenzi Mwalimu

- Amesema kitamsaidia Rais Magufuli dhidi ya Mafisadi na wote wasioeleweka

Zaidi, soma https://jamii.app/KifimboRaisMagufuli
UKUAJI WA UCHUMI KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA WAZIDI KUDORORA

> Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) inasema ukuaji wa uchumi umeendelea kuwa mdogo kwa mwaka 2019, kutokana na misukosuko ya uchumi wa dunia na mabadiliko machache ya kiuchumi katika nchi hizo

> Ukuaji wa uchumi ktk nchi zisizo eneo hilo unatarajiwa kuongezeka kwa 2.6% mwaka 2019, kutoka 2.5% mwaka 2018 ikiwa ni 0.2% chini ya kiwango kilichotabiriwa Aprili 2019

Soma - https://jamii.app/UkuajiUchumiAfrika
WARIOBA: KUKAA MADARAKANI MUDA MREFU HULETA MAZOEA KATIKA UTENDAJI

> Jaji Joseph Warioba amewashauri viongozi kutokaa madarakani muda mrefu kwani husababisha ufanyaji kazi kwa mazoea na kuathiri maendeleo ya nchi

> Ameongeza kuwa, ukiona kuna mabadiliko ya Katiba kuondoa ukomo wa uongozi, ujue Kiongozi wa Juu ndiye ana Uchu wa Madaraka ya kutaka kusalia madarakani

Soma - https://jamii.app/UkomoMudaUongozi
MBOWE: HATUTASUSIA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

- Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hawatasusia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24

- Amesema wanaona sio sawa Wapinzani kususia uchaguzi kwasababu wenzao wanatamani wasusie

Zaidi, soma https://jamii.app/CHADEMAUchaguziSerikaliMitaa
UNICEF: MMOJA KATI YA WATOTO WATATU ANAKABILIWA NA UTAPIAMLO

> Ripoti iliyotolewa na Shirika la Watoto Duniani inasema Theluthi moja ya watoto chini ya umri wa miaka 5 wanakabiliwa na utapiamlo

> Theluthi mbili ya watoto hawana chakula cha kutosha na karibu nusu ya wale wenye miezi 6 hadi miaka 2, hawapati matunda na mbogamboga

Soma - https://jamii.app/RipotiUtapiamloWatoto
WANANCHI WA MSUMBIJI WANAPIGA KURA LEO KUCHAGUA RAIS NA WABUNGE

> Ushindani wa Urais ni kati ya Chama Tawala (FRELIMO) kinachoongozwa na Rais Filipe Nyusi ambacho kimekuwa madarakani tangu 1975 na Ossufo Momade anayewakilisha Chama cha RENAMO

> Wagombea wengine ni Daviz Simango wa Chama cha Demokrasia na Mario Albino wa Chama cha AMUSI

Soma - https://jamii.app/MozElections2019
HALMASHAURI YA LINDI VIJIJINI KUWA HALMASHAURI YA MTAMA

- Rais Magufuli ameagiza Halmashauri ya Lindi Vijijini kuitwa Halmashauri ya Mtama

- Pia, ametaka Makao Makuu ya Halmashauri hiyo yahamishiwe Mtama kutoka kwenye jengo lililopo Lindi Mjini ndani ya siku 15

Zaidi, soma https://jamii.app/HalmashauriMtamaOkt15
MATOKEO DARASA LA 7, 2019 YATANGAZWA. UFAULU WAONGEZEKA

- NECTA imetangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2019 na kusema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78

- Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 na Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kutokana na sababu mbalimbali

Zaidi, soma https://jamii.app/MatokeoSTD7-2019
KENYA: WANAFAMILIA WATATU WAFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO

- Mtoto 1 na wanafamilia wengine wawili wamefariki baada ya nyumba yao kuwaka moto huko Kariobangi, Nairobi

- Wanafamilia wengine wawili wamekimbizwa ktk hospitali ya Taifa ya Kenyatta

Zaidi, soma https://jamii.app/Wanafamilia3Wafariki-Moto
MICHEZO: Bondia wa Marekani, Patrick Day (27) yupo mahututi baada ya kupigwa akiwa ulingoni katika roundi ya 10 na mpinzani wake Charles Conwell
-
Patrick alipata majeraha makubwa katika ubongo hali iliyopelekea kupoteza fahamu mpaka sasa ambapo amelazwa katika hospitali ya Northwestern Memorial nchini Marekani, ambapo amefanyiwa operesheni ya kichwa
-
Imeripoti kuwa, Patrick mpaka sasa yupo kwenye ‘Coma’ (fahamu hazijarejea) tangu alipopigwa usiku wa Jumamosi
MASHAMBULIZI YA UTURUKI, SYRIA: MAREKANI YAIWEKEA VIKWAZO UTURUKI

> Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Wizara mbili za nchini Uturuki na Maafisa 3 wa Serikali, kutokana na Operesheni ya Kijeshi inayoendelea Kaskazini mwa Syria dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi

> Rais Donald Trump amemtaka Rais wa Uturuki asitishe operesheni hiyo mara moja

Soma - https://jamii.app/TrumpTurkishAttack
TAMISEMI: PWANI KINARA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA

- Mkoa unaoongoza uandikishaji kwenye Daftari la Mpiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Pwani

- Lakini Mikoa ya Dar, Arusha na Kilimanjaro uandikishaji wao uko chini ya 50%

Zaidi, soma https://jamii.app/PwaniKinaraUandikishajiKura
FAHAMU KUHUSU MNYAMA PANYA

> Panya hawaoni vizuri, hivyo hutumia uwezo wao mkubwa wa kusikia, kunusa harufu, kuhisi kupitia miguu kwaajili ya kutambua mazingira na hali ya eneo ambalo yupo

> Meno ya Panya huongezeka kila siku hivyo ili kupunguza kukua kwa kiasi kikubwa huwa na kawaida ya kupenda kujisugua katika vitu vigumu ili kupunguza urefu na hapa ndio utakuta ametafuna rimoti, waya, ndoo, nguo

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/UfahamuPanya
#JFMaarifa
UGANDA: HAKUNA MPANGO WA SHERIA YA KIFO KWA MASHOGA

- Imesema haina mpango wa kuweka adhabu ya kifo dhidi ya wanaoshiriki Mapenzi ya Jinsia Moja

- Ni baada ya Nchi wahisani kusema zinafuatilia nia ya Nchi hiyo kurejesha muswada huo

Soma https://jamii.app/UgandaSheriaKuuaMashoga