JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MATOKEO DARASA LA 7: Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2019

- Limetangaza pia Watahiniwa 10 waliofanya vizuri Kitaifa, Mikoa 10 iliyofanya vizuri na Shule 10 zilizofanya vizuri Kitaifa

Zaidi, soma https://jamii.app/MatokeoSTD7-2019
MOROGORO: MVUA YASABABISHA VIFO VYA WATU 11

> Mvua za Vuli zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha vifo vya watu 11 Mkoani Morogoro huku kati yao watoto wakiwa ni 9

> Watoto watano kati yao walifariki baada ya kuzama Mto Mvuha uliopo Kata ya Kibogwa

Soma - https://jamii.app/Vifo11MvuaMoro
JE, WANAUME WENGI HUFA MAPEMA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO UNAOSABABISHWA NA WANAWAKE?

> Katika utafiti uliowahi kufanywa ulibaini kwamba tabia ya kujihatarisha na kukandamiza mihemko ya kihisia kwa vijana wa kiume, inahusiana moja kwa moja na vifo vya mapema vya wanaume ukilinganisha na wanawake

> Tabia hizo ni Ugumu katika kufunguka, Ugumu wa kusamehe, Msongo wa mawazo, kutokujali afya na Tabia hatarishi. Inadaiwa Wanaume wengi wana maradhi ya kihisia kuliko wanawake

Kwa mjadala zaidi - https://jamii.app/VifoMeMsongoMawazo
#JFMahusiano
MBARONI KWA KUJIANDIKISHA MARA 2 KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

- Ni Ngeze Mwagilo (29), Mkazi wa Kasanga Manispaa ya Morogoro

- Anadaiwa kujiandikisha katika Kituo cha Kasanga na kisha kwenda kujiandikisha katika Kituo cha Kiwanja cha Ndege

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniUandikishaji2-Moro
MALAWI YAKANUSHA KUWA NA MGONJWA WA EBOLA

> Mamlaka ya Afya imekanusha ripoti ya kwamba mtu amegunduliwa kuwa na Ebola kwenye eneo la Karonga linalopakana na Tanzania

> Ofisa wa Afya amesema mtu huyo alikuwa na maambukizi ya Bakteria na si Ebola

Soma - https://jamii.app/MalawiDenouncesEbola
KAMPUNI ZA BOEING NA PORSCHE ZAUNGANA KUUNDA MAGARI YA KUSAFIRI ANGANI

> Boeing ya Marekani na Porsche ya Ujerumani zimetia saini makubaliano (MoU) kwa ajili ya uundwaji wa magari ya umeme yatakayokuwa na uwezo wa kupaa na kutua wima (Vertical Take-off and Landing (VTOL)) ili kuingia katika soko la 'Taxi'

Soma - https://jamii.app/PorscheBoeingFlyingCars
AZAKI ZATAKIWA KUENDESHA SHUGHULI ZAO KWA UWAZI ILI KUPATA UNAFUU WA KODI

> Waziri wa Fedha amezitaka Asasi za Kiraia kuendesha shughuli zao kwa Uwazi na Uwajibikaji kwa kufuata Sheria za Nchi, Matakwa na Vigezo ili kupata unafuu wa kodi

> Pia, amezitaka kuwasilisha mapendekezo juu ya Sheria za Kodi ili kilio chao cha msamaha wa kodi kifanyiwe kazi

Soma - https://jamii.app/AZAKIUwaziKodi
SHIRIKA LA NDEGE LA SWISS LASIMAMISHA SAFARI ZA AIRBUS A220

> Shirika la Ndege la SWISS International Airlines limesimamisha safari za ndege zake zote aina ya Airbus A220 kutokana na matatizo ya injini zake aina ya PW 1500G zinazotengenezwa na Kampuni ya Pratt & Whitney ya Canada

Soma - https://jamii.app/SwissGroundsA220
TMA YATOA ANGALIZO LA KUWEPO KWA MVUA KUBWA UKANDA WA PWANI KWA SIKU 2

> Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa ktk Mikoa ya Tanga, Dar, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro na Visiwa vya Unguja na Pemba

> Mvua hizo zitaanza Oktoba 16 hadi Oktoba 17, 2019

Soma - https://jamii.app/TahadhariMvuaPwani
UFAHAMU NA ELIMU YA UGONJWA WA MAFINDOFINDO (TONSILS)

> Mafindofindo hujitokeza pale viungo viwili vidogo nyuma ya koo vinapozidiwa nguvu katika kupambana na wadudu wabaya ndani ya mwili

> Dalili zake ni Maumivu ya koo, maumivu wakati wa kufungua kinywa, ugumu katika kumeza mate/chakula, homa, kuvimba kwa Lymph Nodes kwenye shingo

> Tiba unayoweza kujipatia mwenyewe ni kunywa/kusukutua maji ya uvuguvugu kila mara (angalau mara 4 kwa siku) yenye chumvi, asali pamoja na ndimu/limao. Jambo hili huleta maumivu makali lakini utapona haraka

Soma - https://jamii.app/UgonjwaTonsils
#JFAfya
KENYA: BASI LA KANISA LAKAMATWA LIKISAFIRISHA MISOKOTO YA BANGI

> Polisi wamekamata basi la Kanisa la PEFA likiwa na Misokoto 230 ya bangi iliyokuwa imesundwa kama mizigo

> Bangi hiyo inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 1

Soma - https://jamii.app/KanisaKusafirishaBangi
SERIKALI YASHINDA RUFAA YA KUPINGA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI

> Mahakama ya rufaa imetoa uamuzi huo baada ya kujiridhisha na hoja za Serikali kuwa Wakurugenzi hao kabla ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi hula viapo vya kukana uanachama wao

> Kesi hiyo ilifunguliwa na Bob Wangwe

Soma - https://jamii.app/WakurugenziUsimamiziUchaguzi
#JFLeo
KIWANGO CHA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KITAIFA CHASHUKA

> Kiwango kimeshuka kutoka 7% mwaka 2003/04 hadi kufikia 4.7% 2016/17 huku maambukizi kwa wanaume ikiwa ni 3.4% na wanawake ni 6.3%

> Hatua zilichochangia ni pamoja na huduma za ushauri nasaha na upimaji, tohara kwa wanaume, huduma za kondomu

Soma https://jamii.app/KushukaMaambukiziVVU
MGOGORO TANESCO NA IPTL: TANZANIA YAAMRIWA KULIPA DOLA MILIONI 185

> Mahakama ya Migogoro ya Kimataifa (ICSID), imeamuru Serikali ya Tanzania kulipa Dola 185.4 milioni (zaidi ya Tsh. Bilioni 426) kwa kukiuka mkataba

> TANESCO liliingia makubaliano ya kuzalisha umeme na IPTL 1995 lakini 2013 kukatokea kutoelewana

Soma - https://jamii.app/TzMalipoIPTL
WADAIWA SUGU WASABABISHIA UMOJA WA MATAIFA UKATA

- Inadaiwa Umoja huo unaweza kushindwa lipa Wafanyakazi na Watoa Huduma wake iwapo wadaiwa wasipolipa kufikia Oktoba 31

- Wadaiwa hao ni US, Argentina, Mexico, Israel, Iran, Venezuela na Brazil

Soma https://jamii.app/UkataUmojaWaMataifa