JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZANZIBAR: 'BABY J' NA MAUZINDE WATAKIWA KUKAMATWA

- Msanii Jamillah Abdallah(Baby J) na Maulid Abdallah(Mauzinde) wanatakiwa kukamatwa kwa uvunjifu wa maadili

- Unadaiwa kufanyika kwenye sherehe ya singo iliyoandaliwa na Baby J

Zaidi, soma https://jamii.app/BabyJKukamatwa-ZNZ
KILIMANJARO: MBARONI AKIDAIWA KUMUUA MWANAYE KWA KUMKATA SHINGONI

- Makazi wa Rombo, Philipina Donath(37) anadaiwa kumuua mwanaye wa miaka mitano kwa kumkata na kisu shingoni

- Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alijisalimisha mwenyewe Polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/AdaiwaKumuuaMwanaye-KLM
MUSOMA: AHUKUMIWA MIAKA 60 JELA KWA KULAWITI NA KUWAVUTISHA WATOTO BANGI

- Nyamasheki Malima(41) amehukumiwa kwa kukutwa na hatia ya kuwavutisha bangi watoto wawili wa kiume wenye miaka 11 na 13 wa familia moja, kisha kuwalawiti

Zaidi, soma https://jamii.app/Miaka60JelaBangiKulawitiWatt
KIGOMA: MWANAFUNZI AMKANA MWALIMU MKUU ALIYEDAIWA KUMPA MIMBA

- Mahakama imemuachia huru Mwalimu Mkuu, Jason Rwekaza wa Shule ya Msingi Nyantore

- Ni baada ya Mwanafunzi mwenye mimba kueleza kuwa hamfahamu mtu aliyempa mimba hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuMimbaHuru-KG
SUDAN KUSINI: WATOTO WAZIDI KUINGIZWA KATIKA VIKOSI VYA MAPIGANO

> Maelfu ya Watoto waliachiwa kutoka katika vikosi vya mapigano baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani mwaka 2018

> Wasichana wanachukuliwa na kutumikishwa kingono

Soma > https://jamii.app/WatotoVitaSudanKusini
KOREA KUSINI: WAPINZANI WANYOA NYWELE, WAKIPINGA UTEUZI WAZIRI MPYA WA SHERIA, CHO KUK

> Kiongozi Mkuu wa Upinzani, Hwang Kyo-ahn amenyoa nywele nje ya Ikulu. Wiki iliyopita Wabunge Wanawake walifanya hivyo

> Familia ya Cho inatuhumiwa kwa rushwa

Soma > https://jamii.app/ChoKukSouthKorea
ITALIA: KITUO CHA TV CHAMFUTA KAZI MTANGAZAJI NA MCHAMBUZI ALIYEMBAGUA ROMELU LUKAKU

> Top Calcio 24 Tv yamfuta kazi Luciano Passirani aliyesema "Ukikabiliana na Lukaku atakuua, njia pekee ya kumkabili na kumzuia, labda kumpa ndizi 10 akale"

Soma > https://jamii.app/PassiraniVsLukaku
KIKOKOTOO CHA MAFAO: TUCTA INAZUNGUMZA NA SERIKALI. WATUMISHI WAOMBA KUSTAAFU

- TUCTA imesema inazungumza na Serikali kuhusu kikokotoo kipya kitakavyotumika

- Baadhi ya Watumishi wa Serikali wameomba kustaafu kabla kikokotoo kipya hakijaanza

Soma https://jamii.app/WatumishiKustaafuHiari
TANZIA: MHARIRI WA GAZETI LA JAMHURI, GODFREY DILUNGA AFARIKI DUNIA

- Alikuwa akihariri gazeti la Raia Mwema kabla ya kuanza kuhariri gazeti la Jamhuri mnamo Februari 2019

- Amefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alipokuwa akitibiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/GodfreyDilungaAfariki
AFGHANISTAN: BOMU LALIPUKA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOHUDHURIWA NA RAIS

- Watu 24 wamefariki na wengi kujeruhiwa leo baada ya bomu kulipuka kwenye gari la Polisi

- Limelipuka kwenye mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na Rais Ashraf Ghani

Zaidi, soma https://jamii.app/BlastNearAfghanPrsdnt
MBEYA: FAMILIA 9 ZAKOSA SEHEMU YA KUISHI BAADA YA NYUMBA WANAYOISHI KUTEKETEA KWA MOTO

> Moto huo umeteketeza mali zote zilizokuwepo ndani ya nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Isanga

> Hata hivyo Kikosi cha Zimamoto kilifika na kuzima moto huo

Zaidi, soma https://jamii.app/MotoNyumbaIsanga
TABORA: BINTI WA MIAKA 19 AJIFUNGUA WATOTO WATANO KABLA YA MUDA

> Monica Daudi(19) mkazi wa Mtaa wa Nyasa Wilayani Nzega, aliyekuwa na ujauzito wa miezi 5 amejifungua Watoto hao ndani ya siku 2

> Watoto wote walikuwa na jinsia ya kiume na hawakuweza kuishi kwasababu ya kuzaliwa kabla ya wakati

Soma https://jamii.app/BintiWatoto5Tabora
SHINYANGA: MTUMISHI WA HOSPITALI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA KWA KUOMBA RUSHWA

- Mahakama imemtia hatiani Lucia Thomas Mihayo kwa kuomba na kupokea rushwa ya Tsh. 50,000

- Ametakiwa kutumikia kifungo hicho au kulipa faini ya Tsh. 500,000

Zaidi, soma https://jamii.app/MtumishiKHMHatiaRushwa
KATAVI: ADAIWA KUMUUA MTOTO BAADA YA MTOTO KUPOTEZA NG’OMBE

- Lusambaja Bundala(7) ameuawa kwa kupigwa kichwani na kukatwa na kitu chenye ncha na anayedaiwa ni baba yake mdogo

- Inadaiwa ni baada ya mtoto huyo kupoteza ng'ombe aliokuwa akiwachunga

Zaidi, soma https://jamii.app/AuawaKupotezaMifugo-KTV
MOSHI: MUONGOZA WATALII AJIUA KWA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

> Aliyejirusha na kufariki ni Thomas Meela, mkazi wa Marangu mwenye umri wa miaka 58

> Alimwambia rafiki yake kuwa hawatomuona tena, akakimbia na kujirusha

Soma > https://jamii.app/AjiuaMtKilimanjaro
IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA BAADHI YA MIKOA

- Msemaji wa Polisi Nchini, David Misime ameeleza kuwa ni mabadiliko ya kawaida katika kuboresha utendaji kazi wa Jeshi hilo

- Kamanda Wilbroad Mutafungwa aliyekuwa Morogoro amehamishiwa Makao Makuu na Kamanda Hamis Issah aliyekuwa Kilimanjaro, amepelekwa Morogoro

Zaidi, soma https://jamii.app/MabadilikoMadogoRPC
RWANDA: RAIA WA KENYA AHUKUMIWA KWA KUWALAGHAI VIJANA WA RWANDA

Charles Kinuthia amehukumiwa kifungo cha miaka 2 kwa kuwalaghai vijana wa Rwanda walipe fedha za kujiandikisha kushiriki mkutano wa masuala ya utajiri ambao haukufanyika

Zaidi, soma https://jamii.app/MkenyaAhukumiwaRwanda
KAMPUNI YA TALA INAYOTOA MIKOPO YAFUNGWA NCHINI

- TALA inayokopesha kwa njia ya mtandao wa Simu za Kiganjani, imetangaza kufunga shughuli zake Nchini Tanzania na kueleza kuwa taarifa ya kina itatolewa siku chache zijazo

Zaidi, soma https://jamii.app/TalaYafungwaTanzania
KAGERA: WANAFUNZI WANAOTUHUMIWA KWA MAUAJI WARUHUSIWA KUJIANDAA NA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE WAKIWA GEREZANI

> Wanafunzi hao ni wa Shule ya Sekondari Katoro Islamic wanaotuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya Mwanafunzi mwenzao, Mudy Muswadiku

Soma > https://jamii.app/WanafunziKusomeaJela