JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: MWANAFUNZI AJIUA BAADA YA MWALIMU KUMKEJELI ALIPOCHAFUKA KWA HEDHI

> Jackline Chepngeno (14) alichafuka nguo zake akiwa darasani ndipo Mwalimu alimuamuru kutoka darasani, asimame nje

> Kundi la wazazi waliandamana na kufunga barabara wakishinikiza Mwalimu huyo achukuliwe hatua

Soma - https://jamii.app/StdnSuicideHumiliation
SUDAN KUSINI: RAIS SALVA KIIR NA RIEK MACHAR WAKUBALIANA KUUNDA SERIKALI YA MPITO NOVEMBA 12, 2019

> Wamekubaliano ktk kikao walichokutana, Juba. Machar anayewaongoza Waasi amerejea nchini humo baada ya kukaa uhamishoni Khartoum kwa mwaka 1

Soma > https://jamii.app/KiirVsMacharJuba

#JFLeo
RAIA WA NIGERIA ZAIDI YA 600 WAANZA KUONDOLEWA AFRIKA KUSINI

> Watu 640 ndio wanatarajiwa kusafirishwa kutoka Johannesburg kwenga Nigeria ambapo inakadiriwa kuwa idadi ya raia 313 watachukuliwa katika awamu ya kwanza ambayo imefanyika leo na waliosalia watasafirishwa siku za Alhamisi na Ijumaa wiki hii

Soma - https://jamii.app/NigeriansLeavingSA
UGANDA: SERIKALI KUUNDA BARAZA LA KISWAHILI

- Baraza hilo litahakikisha lugha ya Kiswahili inakuwa lugha rasmi ya pili nchini humo baada ya lugha ya Kiingereza

- Katiba ya Uganda inahitaji kuwepo kwa lugha 2 rasmi(Kiswahili & Kiingereza)

Soma > https://jamii.app/KiswahiliUganda
MICHEZO: Kocha aliyeipeleka Tanzania kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019, Emmanuel Amuneke amelishtaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) akilalamika kutolipwa stahiki zake

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Kocha huyo ambaye ni raia wa Nigeria ameamua kupeleka shauri hilo FIFA ili waweze kulitatua

TFF walifikia uamuzi wa kuvunja mkataba na Amuneke baada ya Taifa Stars kufanya vibaya katika fainali za AFCON zilizofanyika kati ya Juni 21 hadi Julai 19.
HAKIMU WA MAHAKAMA YA MAGOMENI KIZIMBANI KWA KUOMBA RUSHWA

> Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imemfikisha Mahakamani Omary Abdalah (40), kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Tsh. 703,000

> Aliomba fedha hizo ili kumsaidia mlalamikaji kwenye kesi ya mirathi

Soma - https://jamii.app/HakimuKizimbaniRushwa
KISUTU: MWANDISHI ERICK KABENDERA AFIKA MAHAKAMANI AKIWA ANACHECHEMEA MGUU WA KUSHOTO

> Kesi inayomkabili Mwanahabari huyo imeahirishwa hadi Septemba 18

> Hakimu Agustine Rwizile amemuagiza kuja kuieleza Mahakama kuhusu afya yake

Zaidi, soma => https://jamii.app/AfyaKabendera
NAIBU WAZIRI WA AFYA ATOA WIKI 2 ZA UCHUNGUZI WA MTOTO ALIYEKATWA KIGANJA

> Ameagiza Baraza la Madaktari Tanganyika na Baraza la Wauguzi kuchunguza suala la mtoto kukatwa kiganja kilichoharibika baada ya kuchomwa sindano

> Asema, watu wamekuwa wakitibiwa kienyeji katika vituo vya kutolewa huduma

Soma - https://jamii.app/UchunguziKiganjaMtoto
MBOWE NA VIONGOZI WENZAKE WA CHADEMA WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU

> Mahakama ya Kisutu leo imewakuta na kesi ya kujibu viongozi 9 akiwemo M/kiti wa chama hicho, Freeman Mbowe

> Wanakabiliwa na kesi ya jinai yenye mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi

Soma - https://jamii.app/ChademaKesiUchochezi
#JFLeo
Kwa taarifa zaidi, soma https://jamii.app/DiwaniAthumanTISS
KILIMANJARO: MTOTO MCHANGA AOKOTWA KARIBU NA SHIMO LA CHOO

> Mtoto mchanga ameokotwa baada ya Mama yake, Rabia Yunisi (19) mkazi wa Wilayani Siha kumtupa kwa madai ya kutelekezwa na Mzazi mwenzake, ugumu wa Maisha na hofu ya kufukuzwa nyumbani

Soma - https://jamii.app/MtotoMchangaAokotwa
KENYA: WAHUDUMU WA AFYA WAGOMA WAKIDAI MISHAHARA YAO

> Mgomo huo umefanywa na wauguzi katika Kaunti ya Kisumu tangu jana ambapo wiki iliyopita waliipa Serikali siku 7 kuwalipa mishahara yao ya mwezi Julai na Agosti lakini Serikali imeshindwa kufanya hivyo

Soma - https://jamii.app/HealthWorkersStrike
URAFANSA: RAIS WA BUNGE KUCHUNGUZWA KUHUSU TUHUMA ZA UBADHIRIFU

> Majaji wanaohusika na uchunguzi wamemuweka Richard Ferrand chini ya uchunguzi rasmi katika sakata la ubadhirifu wa fedha

> Hii ni mara ya pili kwa Ferrand kuhusishwa kwenye tuhuma za ubadhirifu

Soma - https://jamii.app/FerrandCorruptionInvestigation
JF STATUS: Tunaomba radhi kwa wateja wetu walio Tanzania kutokana na baadhi kukutana na “Error” message inayotokea wanapoitembelea JF

> Kuna changamoto ya Content Delivery Network Servers nyingi za Afrika muda huu lakini tatizo linatafutiwa ufumbuzi wa haraka

Jamii Forums
DRC: TRENI YAACHA NJIA NA KUPINDUKA
-
Takribani watu 50 wameripotiwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya treni kuacha njia na kupinduka katika Jimbo la Kusini Mashariki nchini Jahmuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
-
Serikali imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya asubuhi na kutoa pole kwa wote waliopoteza wapendwa wao
SHINYANGA: BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA MSALALA LAWAFUKUZA KAZI WATUMISHI 46

> Watumishi hao walibainika katika zoezi la Uhakiki wa Watumishi hewa lililofanyika Nchi nzima kuwa wameghushi vyeti na kujipatia Ajira kinyume na sheria

Soma - https://jamii.app/WafukuzwaKughushiVyeti
HISTORIA: MFAHAMU MWAMI THERESA NTARE VI, CHIFU WA KWANZA MWANAMKE

> Alikuwa Kiongozi wa Jamii ya Heru huko Kasulu na aliweza kushika wadhifa wa kuwa Mkuu wa Machifu wote Tanganyika kutoka kwa Chifu Petro Itosi Marealle 1958

> Alikuwa mmoja ya Wabunge wachache wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika kabla ya Uhuru

> Aliendelea kuwa Mbunge mpaka miaka ya 1980, kabla ya hapo aliachia uchifu mwaka 1962 na alifariki mwaka 1999

Fahamu zaidi - https://jamii.app/TheresaChifuMwanamke
#JFHistoria
WALIMU 16 WAKAMATWA KWA KURUHUSU MWANAFUNZI FEKI AFANYE MTIHANI

> Walimu 16 wa Shule ya Msingi Kenyamanyori, Mkoani Mara wamekamatwa na Polisi kwa madai ya kumruhusu anayedaiwa kutokuwa mwanafunzi kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba

> Walimu hao walikuwa wamepangiwa kusimamia mitihani hiyo

Soma - https://jamii.app/MwfnzFekiDrs7
MICHEZO: Kiungo wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Arda Turan amehukumiwa kwenda jela miaka Mitatu, kwa kosa la kufyatua risasi katika hospitali moja nchini Uturuki na kusababisha taharuki ikiwa ni kinyume na sheria ya umiliki wa silaha

> Kifungo hicho pia kinaambatana na kosa la kugombana na Mwanamuziki mashuhuri nchini Uturuki na kumpiga mpaka kumvunja pua

#JFMichezo
ZIMBABWE: TAKRIBANI VIONGOZI 10 WA AFRIKA KUHUDHURIA MAZISHI YA MUGABE

> Wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Rais wa kwanza wa Zimbabwe ambaye mwili wake uliwasili Jumatano ukitokea Singapore

> Miongoni mwa waliothibitisha kushiriki ni Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Filipe Nyusi wa Msumbiji

Soma - https://jamii.app/LeadersMugabeFuneral