JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Tanzania ‘#TaifaStars’ imetoka sare ya goli 1-1 na timu ya Taifa ya Burundi ndani ya dakika 120 zilizomalizika

- Zinaenda kutafuta mshindi atakayefuzu hatua inayofuata kwa kupigiana penati baada ya kuwa zimefunga goli 2-2 katika michezo miwili
MICHEZO: Tanzania imefanikiwa kwenda hatua ya makundi kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022 baada ya kuitoa Burundi kwa penati 3-0

- Kipa Juma Kaseja ameweza kucheza penati 1 ya Burundi wakati timu hizo zikitafuta mshindi kutokana na kutoka sare ya goli 1-1
TETEMEKO LA ARDHI LATIKISA MKOA WA KATAVI

> Tetemeko lenye ukubwa wa 5.5 kipimo cha Richa usiku wa kuamkia leo limetikisa huko Mpanda mkoani Katavi na limesikika hadi mikoa jirani

> Athari zake bado hazijajulikana

> Ni tetemeko la pili ndani ya mwaka mmoja

Soma https://jamii.app/TetemekoMpanda

#earthquake
MOROCCO: MAFURIKO YAPINDUA BASI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 11

> Vifo vimetokea baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduliwa na mafuriko katika daraja lililopo El Khank

> Watu 27 wameokolewa na kupelekwa Hospitali ya Errachidia

Zaidi, soma > https://jamii.app/MafurikoMorocco
UINGEREZA: WAZIRI WA AJIRA AJIUZULU KWA KUTOKUBALIANA NA MPANGO WA BREXIT

> Waziri Mkuu, Boris Johnson amemteua Therese Coffey kujaza pengo lililoachwa wazi na Waziri wa Ajira na Pensheni, Amber Rudd aliyejiuzulu kwa kutokubaliana na namna Johnson anavyoendesha mchakato wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya-Brexit

> Johnson ameapa kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31

Soma - https://jamii.app/MinisterWorkResigns
HONG KONG: MAELFU YA WANAFUNZI WAGOMA ILI KUUNGA MKONO HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU NA DEMOKRASIA KUTOKA CHINA

- Maelfu ya Wanafunzi wameshikana mikono nje ya shule zao wakiungana na raia wengine kupigania uhuru demokrasia kamili kutoka China

Soma > https://jamii.app/MgomoWanafunziHongKong
BURKINA FASO: WATU 29 WAFARIKI KWENYE SHAMBULIO LA RISASI NA BOMU

> Watu 15 wamefariki baada ya Lori la uchukuzi kukanyaga bomu la kutegwa ardhini lililotengenezwa kienyeji

> Wengine wamefariki kwenye tukio la watu wenye silaha kushambulia msafara wa chakula ambacho kilikuwa kinasafirishwa kwa wakimbizi wa ndani katika Wilaya ya Kelbo

Soma - https://jamii.app/29DeadBurkinaFaso
MARA: MWALIMU MKUU ATUHUMIWA KUBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA 7

> Polisi Mkoa wa Mara wanamshikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi Bwai A, Lazaro Mmanga, kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wa darasa la saba(14)

> Anadaiwa kutenda kosa hilo katika ofisi za shule

Soma - https://jamii.app/MwlMkuuAbakaMwnf
MICHEZO: Bodi ya Ligi Kuu Tanzania bara imeuondoa kwenye ratiba mchezo wa ligi kuu kati ya Mbeya City na Yanga uliopangwa kuchezwa Septemba 18, 2019 na sasa mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine
-
Taarifa kutoka bodi ya ligi inaeleza kuwa sababu za kuondoa mchezo huo ni kuipa nafasi timu ya Yanga kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zesco ya nchini Zambia
UPDATE: Mwili wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe unatarajiwa kuwasili nchini humo Septemba 11, 2019 na mazishi yatafanyika Jumapili, Septemba 15 baada ya kuagwa katika Uwanja wa Taifa Mjini Harare

> Rais Mugabe alifariki Septemba 6 nchini Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu tangu Aprili, 2019

#JFLeo
HAI: ZAIDI YA WANAFUNZI 400 WA CHUO CHA UALIMU WAANDAMANA, WADAI KUTAPELIWA ADA ZAO NA UONGOZI WA CHUO

- Wanafunzi hao wanaitaka serikali iingilie kati sakata la madai yao ya kutapeliwaa milioni 75 walizolipa kama ada ya masomo

Zaidi, soma => https://jamii.app/WanafunziMoshiPolisi
AFYA: FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA U.T.I, DALILI NA TIBA

> U.T.I (Urinary Tract Infection) huathiri njia ya Mkojo na Figo na huweza kusababisha maumivu makali na Bakteria wasipotibiwa mapema huenea hadi kwenye Figo

> Dalili zake ni pamoja na mtu kusikia haja ya kukojoa kila wakati, kusikia maumivu, kutoa mkojo mchafu na hata kutoa mkojo iliyochanganyika na damu

> Tiba mbadala, unaweza kuudhibiti kwa kunywa maji mengi pamoja na Juisi ya matunda halisi, iwapo utawahi kabla tatizo halijawa sugu

Tembele - https://jamii.app/FahamuUgonjwaUTI
#JFAfya
FAHAMU BAADHI YA MAMBO AMBAYO BARA LA AFRIKA LINAJIVUNIA KUWA NAYO

> Je, unayajua mambo ambayo bara la Afrika linajivunia kuwa nayo? Moja ni Nigeria kuwa nchi yenye matajiri wengi weusi kuliko sehemu nyingine na Zanzibar ndio nchi ya kwanza kuwa na television ya rangi Afrika

> Rais wa Zimbabwe, Hayati Robert Mugabe ndiye Rais msomi zaidi duniani ambapo ana degree 7 alizosomea katika vyuo mbalimbali

> Somalia ilipata mashine yake ya kwanza ya ATM Oktoba 7, 2014 na kabla ya hapo hakukuwa na ATM yoyote nchini humo

Kufahamu zaidi - https://jamii.app/FctsAboutAfrica
#JFIntelligence
UINGEREZA: MARUBANI WAANZISHA MGOMO, SHIRIKA LAFUTA SAFARI ZOTE ZA NDEGE

> Shirika la ndege la Uingereza limetangaza kufuta takribani safari zote za ndani na nje ya London baada ya Marubani kuanza mgomo wa saa 48 wakidai maboresho kwenye mishahara yao

> Mpaka sasa wasafiri wapatao 145,000 wameathiriwa na mgomo huo

Soma - https://jamii.app/BritishAirwaysFlightscancelled
#JFLeo
MAHAKAMA KUU, DAR: Mahakama Kuu imekataa maombi ya Tundu Lissu(CHADEMA) ya kutengua maamuzi ya Spika kumvua Ubunge

- Jaji Matupa amesema hawezi kufuta uamuzi wa Spika Ndugai kwa sababu ataingia kwenye mgogoro wa kikatiba na Bunge.

Zaidi, soma > https://jamii.app/KesiLissuUbunge
MCHUNGAJI WA KANISA LA PENTECOSTAL POWER MINISTRY AKAMATWA KWA AMRI YA WAZIRI

> Waziri Lugola amefika katika kanisa hilo na kuamuru kukamatwa kwa Mchungaji wake, Eliya Mahela

> Anatuhumiwa kuendesha Kanisa bila kibali na kuwapigia kelele majirani

Soma > https://jamii.app/LugolaVsNabiiEliya
MOTO UNAOWAKA MSITU WA AMAZON WATEKETEZA HEKTA 1700

> Moto unaoendelea kuwaka katika msitu wa Amazon nchini Brazil umevuka mpaka na kuteketeza hekta 1700 za msitu nchini Bolivia

> Serikali ya Bolivia imetakiwa kutangaza moto huo kuwa ni janga la Taifa kwa kuwa umeangamiza sehemu kubwa ya misitu ambayo ina vyanzo muhimu vya maji

Soma - https://jamii.app/AmazonFireInBolivia