JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BAHAMAS: WALIOFARIKI KUTOKANA NA KIMBUNGA DORIAN WAFIKIA 43

- Waziri Mkuu wa Bahamas amesema idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka maradufu

- Watu 35 wamefariki kisiwani Abacos na wengine 8 wamefariki kisiwani Grand Bahama

Zaidi, soma https://jamii.app/43WafarikiBahamas-Dorian
SEMENYA AACHANA NA RIADHA NA KUIJUNGA NA KLABU YA SOKA

> Mwanariadha Caster Semenya (28) ameanza kufanya mazoezi na klabu ya wanawake ya JVW FC kutoka mjini Gauteng baada Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) kuweka sheria zinazotaka wanawake walio na homoni za juu za ‘testosterone’ kutumia dawa kuzipunguza kabla ya kushiriki mashindano yoyote kitu ambacho amekataa kufanya

Soma - https://jamii.app/SemenyaJoinsFootball
#JFMichezo
BUNGE LAPITISHA KUHARAMISHA UMILIKI WA SILAHA PASIPO RIDHAA YA IGP

> Limepitisha marekebisho kwenye sheria ya udhibiti wa silaha na milipuko pamoja na sheria ya uhifadhi wa wanyama pori umepitishwa na kuharamisha uingizaji, utengenezaji na umiliki wa fataki bila ridhaa ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP)

Soma - https://jamii.app/SheriaUmilikiSilaha
KENYA: HAKIMU NA MAAFISA WA MAHAKAMA MBARONI WAKIDAIWA KUPOTEZA VIELELEZO

- Ni Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Mombasa, Edgar Matsigulu na Wafanyakazi wengine watatu

- Wanadaiwa kuhifadhi vibaya vielelezo vya Mahakamani na kupoteza 10Kg za Heroin na fedha

Zaidi, soma https://jamii.app/HakimuMombasaMbaroni
MAMBO MUHIMU YA KUFANYA ILI UWEZE KUIMILIKI SIKU YAKO VIZURI

> Mwandishi Aubrey Marcus anatushirikisha jinsi ya kuimiliki siku ktk kila eneo la maisha yetu

> Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya unapoamka ni kunywa maji na kiasi cha kunywa ni angalau theluthi moja ya lita ya maji

> Pata mwanga wa Jua kwa kuwa ndiyo hupeleka taarifa kwenye akili zetu na unapofika kwenye ngozi husaidia ngozi kutengeneza vitamin D

> Jitahidi kuoga maji baridi kwa kuwa huupa mwili msongo wa muda mfupi, na hivyo kuufanya utengeneze kinga na kujiweka kuwa imara zaidi

Fahamu zaidi - https://jamii.app/MuhimuKumilikiSiku
#JFMaisha
KLABU YA SIMBA YAMTAMBULISHA CEO WAKE MPYA

- Yamtambulisha Senzo Mazingiza wa Afrika Kusini kuwa Mtendaji Mkuu(CEO), akichukua nafasi ya Crescentius Magori anayemaliza muda wake

- Senzo amewahi kuwa CEO wa vilabu vya Platinum Stars na Orlando Pirates vya Afrika Kusini
MAGHEMBE AZISHUTUMU KAMPUNI ZA MAWASILIANO KWA KUIBA PESA ZA VIFURUSHI

> Mbunge wa Mwanga, Jumanne Maghembe amezilalamikia Kampuni za Mawasiliano na kuzionya kuhusu tabia ya kuwaibia wateja wao wanapojiunga na vifurushi

> Ametolea mfano Kampuni ya Vodacom kuwa wamekuwa wakimuibia sana dakika zake pindi anapojiunga vifurushi

Soma - https://jamii.app/WiziVifurushiSimu
DAR: BABU SEYA AFUNGA NDOA TAKATIFU

- Mwanamuziki Mkongwe nchini, Nguza Viking maarufu ‘Babu Seya’ amefunga ndoa takatifu leo na Katibu Tawala Wilaya ya Muheza (DAS), Esterine Haule

- Babu Seya na Mke wake wamefunga ndoa hiyo katika Kanisa Katoliki la Sinza
IRAN YATANGAZA KUTUMIA MASHINE ZA KISASA KURUTUBISHA URANIUM

- Imesema licha ya kujiondoa katika mkataba wa nyuklia bado itaruhusu Mataifa kufuatilia kazi zake

- Marekani imesema haishangazwi kuona Iran imeanzisha mashine mpya ya nyuklia

Zaidi, soma https://jamii.app/IranMashineMpyaUranium
SUDAN YAREJESHWA NDANI YA AU BAADA YA KUUNDA SERIKALI YA MPITO

> Umoja wa Afrika umeirejeshea Sudan uanachama wake, baada ya kusimamishwa kwa miezi 3 ikisubiriwa kuunda Serikali ya kiraia

> Sudan ilisimamishwa uanachama wake kufuatia vurugu za maandamano kati ya Jeshi na raia ambapo watu kadhaa waliuawa

Zaidi, soma https://jamii.app/SudanMembershipAU
AUSTRIA: MSITU WAOTESHWA KWENYE UWANJA WA MPIRA KUPINGA UKATAJI MITI

- Mchoraji kutoka Uswizi, Klaus Littmann ameubadilisha Uwanja wa mpira wa Wörthersee kuwa msitu

- Umepandwa miti 300 na baadhi ya miti inakadiriwa kuwa na uzito wa tani 6

Zaidi, soma https://jamii.app/MsituUwanjaMpira-Austria
MJADALA: JE, NI KWELI MTU MKIMYA ANA DHARAU?

- Mdau wa JamiiForums anadai kuwa kuna dhana kuwa mtu mkimya ana dharau kutokana na kwamba wakati wewe unaongea kwa mdomo, yeye anaongea kichwani mwake

- Inadaiwa ukiongea naye mara nyingi anaweza asijibu kwa maneno bali vitendo na pia anadaiwa kutosahau haraka alichoambiwa

Una maoni gani kuhusiana na dhana hii?

Kujadili, tembelea https://jamii.app/UkimyaDharau
MICHEZO: Vikosi vya timu ya Taifa ya Tanzania🇹🇿#TaifaStars’ na timu ya Taifa ya Burundi🇧🇮 vitakavyochuana katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022

- Katika mchezo wa kwanza uliocheza nchini Burundi timu hizo zilifungana goli 1-1
RAIS BUHARI KUTEMBELEA AFRIKA KUSINI ILI KUTULIZA MGOGORO KATI YAO

> Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria atatembelea Afrika Kusini mwezi ujao kujaribu kuboresha uhusiano uliovurugika wa nchi hizo kufuatia wimbi la ghasia na mashambulizi yaliowalenga wageni

> Afrika Kusini imefunga Balozi zake nchini Nigeria baada ya Nigeria nayo kumuita nyumbani Balozi wake nchini Afrika Kusini

Soma - https://jamii.app/BuhariTalksXenophobia
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Tanzania🇹🇿#TaifaStars’ inaongoza kwa goli 1-0 dhidi ya Burundi🇧🇮 katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022

- Goli la Tanzania limefungwa na Mbwana Samatta katika dakika 29 ya mchezo
MAPUMZIKO: Timu ya soka ya Tanzania ‘#TaifaStars’ na timu ya soka ya Burundi zinaenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa kufungana goli 1-1

- Stars ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa Mbwana Samatta (29’) kabla ya Burundi kusawazisha kupitia kwa Abdul Razak (45+1’)
DAR: MAKONDA KURUHUSU MAHUBIRI YA DINI KWENYE VILABU VYA USIKU

- Amesema Mtumishi wa Mungu atakayetaka kuhubiri kwenye vilabu hivyo, aende kwa nusu saa

- Amesema katika vilabu, watu wanacheza kwa furaha ila hawaonekani kufahamu kuhusu Mungu

Zaidi, soma https://jamii.app/MakondaMahubiriVilabuni
MAISHA: FAHAMU KUHUSU URAIBU WA MITANDAO YA KIJAMII

> Mitandao ya kijamii imekuwa aina mpya ya uraibu kwa wengi. Wengi wamejikuta wanakuwa watumwa wa mitandao, wakiitumia kwa muda mrefu

> Kwa namna mitandao hii ilivyotengenezwa, ni makusudi kwa ajili ya kukufanya uitembelee mara kwa mara

> Tafiti zinaonesha uraibu wa mitandao ya kijamii kimekuwa chanzo kipya cha ugonjwa wa sonona (depression) kwa wengi na watu hujilinganisha na wale wanaowaona

Zaidi, soma - https://jamii.app/SocialMediaAddictions
#JFMaisha