JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKEBISHO YA SHERIA: KUTOSAJILI LAINI YA SIMU FAINI MILIONI 5 AU JELA MWAKA 1

- Bunge lililoanza leo linatarajiwa kufanya marekebisho ya Sheria hiyo

- Atakayesababisha kutumika kwa laini isiyosajiliwa, faini Tsh. Milioni 10 au jela miaka 2

Soma https://jamii.app/AdhabuKutosajiliLaini
JARIBIO LA MAPINDUZI BURKINA FASO: WATUHUMIWA WAHUKUMIWA KWENDA JELA

> Aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Upelelezi, Jenerali Gilbert Diendere amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kupatikana na hatia ya kufanya mauaji na kutishia Usalama wa Taifa

> Pamoja naye, Waziri wa Mambo ya Nje amehukumiwa kifungo cha miaka 10 kwa kuwa Mratibu Mkuu wa jaribio hilo

Soma - https://jamii.app/HukumuWatuhumiwaMapinduzi
MMOJA WA MAPACHA WALIOTENGANISHWA, AFARIKI

- Ni Anisia Bernatus, mmoja wa mapacha waliorejea nchini siku chache zilizopita wakitoka Saudi Arabia kutenganishwa

- Amefariki katika hospitali ya Taifa Muhimbili, alipokuwa akipatiwa matibabu

Soma https://jamii.app/MtotoAliyekuwaAmeunganaAfariki
MICHEZO: Klabu ya Manchester United imewatumia wawakilishi wake kusaka mrithi wa kipa wao, David de Gea ambaye yupo mbioni kutimka Old Trafford
-
De Gea amebakiza mkataba wa mwaka 1 ambao utamalizika mwishoni mwa msimu huu na taarifa zilizopo zinadai kwamba amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea na Man. United
-
Klabu ya PSG inamnyatia kipa huyo endapo Man. United itamwachia katika dirisha dogo la usajili Januari 2020
BUNGE KUTOGAWA KARATASI ZA SHUGHULI ZA BUNGE. BARUA PEPE NA WHATSAPP KUTUMIKA

- Spika Ndugai amesema hiyo ni moja ya hatua ya kuondokana na matumizi ya karatasi

- Karatasi hizo hugawiwa kwa Wabunge zikiwa na ratiba ya siku ya shughuli Bungeni

Soma https://jamii.app/KaratasiBungeniMarufuku
MWANANCHI AFUNGUA KESI KUHOJI UKOMO WA MUDA WA URAIS KATIKA KATIBA

> Patrick Dezydelius Mgoya, Dar amefungua kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mahakama Kuu, akihoji Ibara ya 40 (2) ya Katiba ambayo inaweka ukomo wa mihula 2 tuu ya miaka mitano mitano ya uongozi katika nafasi ya Urais na anaiomba Mahakama hiyo itoe tamko na tafsiri ya maana sahihi na athari za Ibara hiyo

Fahamu zaidi - https://jamii.app/KesiUkomoMudaUrais
WAANDISHI WA HABARI WATATU WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MWANZA

> Lilian Kidahya, Ezila Peter na Godfrey Kalabi wanatuhumiwa kuiba vifaa vya magari ya Kampuni ya Utangazaji ya Sahara Media group

> Walikuwa wakilala kwenye eneo la ofisi hizo wakishinikiza kulipwa stahiki zao baada ya kuachishwa kazi

Soma - https://jamii.app/WaandishiMbaroniStahiki
IRAN: RAIS HASSAN ROUHANI ASEMA NCHI YAKE HAITOZUNGUMZA NA MAREKANI

- Ameondoa uwezekano wa kufanya mazungumzo yoyote ya moja kwa moja na Marekani

- Aidha, ametishia kuchukua hatua zaidi ya kupunguza ushirikiano katika makubaliano ya nyuklia

Soma https://jamii.app/Mkutano-RohaniVsTrump
WANAFUNZI 4, MLINZI WA SHULE NA MWALIMU KIZIMBANI KWA KUUA MWANAFUNZI

> Wanafunzi hao, Mwalimu pamoja na Mlinzi wa Shule ya Sekondari Katoro Islamic, wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba wakikabiliwa na tuhuma za kumuua Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, Mood Muswadiku Aprili 14, 2019

Soma - https://jamii.app/WanafnMwalmMauaji
TETESI, MICHEZO: Mtanzania Hasheem Thabeet yupo mbioni kurudi kucheza ligi kuu ya kikapu nchini Marekani (NBA) akihusishwa kujiunga na Timu ya kikapu ya New York Knicks
-
Taarifa za Hasheem kurejea NBA zitatimia endapo New York Knicks wakifanikiwa kumshawishi na kukubaliana kurejea NBA kuendeleza kipaji chake
-
Hasheem amecheza NBA katika Timu za Memphis Grizzlies, Houston Rockets, Portland Trail Blazers, Oklahoma City Thunder na Grand Rapids Drive ambapo mara ya mwisho kucheza NBA ni katika msimu wa 2013-2014
AJALI YA MOTO, MOROGORO: TCRA KUVIADHIBU VITUO VYA HABARI VILIVYOONESHA PICHA ZA MIILI YA MAREHEMU

- TCRA imesema katika hali ya kusikitisha na kustaajabisha, baadhi ya vyombo vya habari vilisambaza picha hizo hususani 'Online TV' zaidi ya 15

Soma https://jamii.app/TCRA-TV-MiiliAjaliMoro
#JFLeo
RUVUMA: JIKO LA MKAA LASABABISHA WATOTO WAWILI KUFARIKI

- Wamefariki kwa kukosa hewa kutokana na jiko la mkaa lililowashwa katika chumba walimokuwemo

- Mama yao, aliyekuwa amebandika mihogo jikoni amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa

Soma https://jamii.app/WafarikiKukosaHewa-RVM
#JFLeo
MWAMUZI ALIYEKATAA GOLI LA RUVU SHOOTING DHIDI YA YANGA, AFUNGIWA

- Janeth Balama aliyekataa goli la Ruvu Shooting afungiwa miezi 3 kwa kukataa goli halali

- Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungiwa kuiongoza Yanga katika mechi 3 za Ligi Kuu

Zaidi, soma https://jamii.app/Mwamuzi-Zahera-Wafungiwa
BEI YA MAFUTA YA PETROLI NA DIZELI YAPANDA. KUANZA KUTUMIKA KESHO

> Bei za rejareja zimeongezeka kwa Petroli Tsh.83 kwa lita, Dizeli Tsh.61 kwa lita na Mafuta ya taa Tsh.46 kwa lita

> Kwa Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara bei zimeongezeka kwa Tsh.108 Petroli na Tsh.72 Dizeli

Soma - https://jamii.app/PriceRisePetrolDiesel
#JFLeo
RAIS RAMAPHOSA AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI KUKOMESHA UKATILI UNAOENDELEA DHIDI YA WAGENI

> Rais wa Afrika Kusini amezitaka Wizara zinazohusika na ulinzi na usalama kuhakikisha wanaangazia matukio ya kikatili yaliyowalenga wageni nchini humo na kuyakomesha kabisa

> Raia wanaoathirika sana ni wa kutoka Nigeria, Somalia na Ethiopia

Soma - https://jamii.app/RamaphosaAddressViolence
MTWARA: WANANCHI WADAI KUPATA MAJI MACHAFU

- Wananchi hususani wa maeneo ya Mangowela wanadai maji yanayotoka Mamlaka ya Maji(MTUWASA) si salama

- Inadaiwa Mamlaka hiyo haina chujio la maji hivyo maji yanayofika kwa wananchi ni machafu

Soma https://jamii.app/MajiMachafuMtwara
#JFLeo
TUNDU LISSU KUTORUDI SEPTEMBA 7. ASEMA NI MPAKA DAKTARI AMPE RUHUSA

> Mwanasiasa huyo amesema sio bayana kwamba atarudi Tanzania Septemba 7 kwa kuwa bado anasubiri kupata ridhaa ya madaktari wake iwapo anaweza kurudi nyumbani

> Aidha, amesema iwapo chama chake pamoja na vyama rafiki vitampa wito, atashiriki kugombea Urais mwakani

Soma - https://jamii.app/LissuSuspendsReturn
MAKONDA AWASILISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MIRATHI

> Muswada huo umezitaja sheria kandamizi za kufanyiwa marekebisho kuwa ni pamoja na Sheria ya kiserikali ya mirathi, Sheria ya Mirathi ya Kimila pamoja na Sheria ya Mirathi ya Kidini kwa madai ya kuwa zimepitwa na wakati na zimekuwa zikileta mateso kwa wajane

Soma - https://jamii.app/MuswadaSheriaMirathi
> Moto unawaka katika Magorofa ya Mwenge, yanayoitwa Magorofa ya Jeshi karibu na ofisi za TRA na chanzo bado hakijafahamika

> Mpaka sasa bado Zimamoto hawajafika kuudhibiti moto huo na taarifa za awali zinadai moto unaendelea kusambaa

> Tutaendelea kukujuza zaidi....

#JFLeo
MKUTANO WA MASHAURIANO WA WADAU WA SEKTA YA UJENZI

- Rais Magufuli anaongoza Mkutano huo unaoendela katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar

- Mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Ujenzi, Isack Kamwelwe

Soma https://jamii.app/MkutanoSektaUjenzi-Magufuli
#JFLeo