JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ALIYEMUUA MKEWE AHUKUMIWA KUSAFISHA HOSPITALI

- Mkazi wa Lindi, Atanasi Kijombo amehukumiwa kusafisha mazingira ya Hospitali ya Kilwa kwa miezi 12

- Alimuua Mkewe, Hadija Mambo bila kukusudia kwa kumkuta akifanya mapenzi na Mwanaume mwingine

Zaidi, soma https://jamii.app/AuaAhukumiwaKusafishaHosp-MTW
DAR: WATU WAFURIKA UWANJA WA TAIFA IKIDAIWA KUNA MIKOPO ITATOLEWA

- Wamedai wamejiandikisha watokako ikidaiwa kuna shirika linagawa mikopo kwa familia masikini na wajane

- Hata hivyo, imeelezwa uwanjani hapo kuna kongamano la ndoa na familia

Zaidi, soma https://jamii.app/MikopoUwanjaTaifa-DAR
LIGI KUU ENGLAND: Mchezo wa kwanza wa Ligi hiyo umemalizika kwa timu ya Manchester United kutoka sare ya goli 1-1 na timu ya Southampton

- Manchester United inafikisha alama 5 ikiwa imecheza michezo minne huku Southampton yenyewe ikifikisha alama 4 baada ya michezo minne
ARUSHA: GHALA LA KIWANDA SUNFLAG LATEKETEA KWA MOTO

- Ghala la kiwanda la kuhifadhia Pamba limeteketea kwa moto na baadhi ya marobota ya pamba inayotumika kutengeneza nguo kuteketezwa

- Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana

Zaidi, soma https://jamii.app/MotoKiwandaSunflag
SERIKALI: WATAKAO TUHUJUMU KUHUSU KUZUIWA NDEGE YA ATCL, KUSHTAKIWA

- Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema watakaobainika kuihujumu Serikali kuhusu kuzuiwa kwa ndege ya ATCL nchini Afrika Kusini watafunguliwa kesi ya kuihujumu nchi

Zaidi, soma https://jamii.app/AtayehujumuKushikwaATCLKushtakiwa
MATOKEO: Baadhi ya mechi za mzunguko wa nne za Ligi Kuu nchini England zimemalizika

- Manchester City imefanikiwa kupata ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Brighton huku Chelsea ikitoka sare na Sheffield United ya goli 2-2
BASHIR AFUNGULIWA RASMI MASHTAKA YA RUSHWA. AKIRI KUPOKEA PESA HARAMU

- Amefunguliwa rasmi mashtaka ya rushwa na kupokea fedha kinyume na sheria kutoka nje ya Nchi

- Amekiri kuzipata fedha hizo kutoka Familia ya Kifalme ya Saudi Arabia

Zaidi, soma https://jamii.app/BashirAkiriKupokeaPesaKiharamu
MICHEZO: Klabu ya Liverpool imeibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya klabu ya Burnley katika mchezo wa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu Soka nchini England

- Liverpool inafikisha alama 12 ikiendelea kuwa kinara wa Ligi huku Manchester City ikiwa nafasi ya pili na alama 10
TANZIA: WAZIRI WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE AFARIKI DUNIA

- Ibrahim Kaduma (82), aliyekuwa Waziri katika Serikali ya awamu ya kwanza, amefariki akiwa India usiku wa kuamkia leo

- Alienda India kwa uchunguzi wa afya baada ya kujisikia vibaya

Zaidi, soma https://jamii.app/KadumaAfariki-Agosti31
ODESSA, TEXAS: WATU 5 WAUAWA NA WENGINE 21 KUJERUHIWA KWA RISASI

> Muuaji alianza kurusha risasi baada ya kusimamishwa na Polisi

> Muuaji huyo pia ameuawa na Polisi

> Ni tukio la pili ndani ya mwezi mmoja baada ya tukio la awali ambapo watu 22 waliuawa na 24 kujeruhiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/OdessaShooting5Killed
BAHAMAS: SERIKALI YAWATAHADHARISHA WANANCHI DHIDI YA KIMBUNGA DORIAN

- Watu katika visiwa hivyo hususani Grand Bahamas na Abaco wametakiwa kujikinga

- Kimbunga hicho chenye mwendokasi wa Kilometa 240 kwa saa, kinatarajiwa kutua Bahamas leo

Zaidi, soma https://jamii.app/HurricaneDorianBahamas
INDIA: SERIKALI KUJIONDOA KWENYE UENDESHAJI WA SHIRIKA LA NDEGE

- Inataka kujiondoka kabisa katika uendeshaji wa shughuli za Shirika la ndege la India (Air India) linaloendelea kupata hasara

- Hili ni jaribio lingine baada ya awali kushindwa

Zaidi, soma https://jamii.app/GovtSellingAirIndia
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO MOROGORO YAFIKIA 104

- Ni baada ya majeruhi wawili kati ya 13 waliokuwa wamelazwa ktk Hospitali ya Taifa Muhimbili kufariki

- Kati ya majeruhi 11 waliobaki, sita wapo wodi namba 22 ya Sewahaji na watano wapo Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU)
MICHEZO: ARSENAL YATOKA SULUHU NA TOTTENHAM

- Arsenal imeilazimisha Tottenham sare ya goli 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Nchini England

- Arsenal inafikisha alama 7 na kushika nafasi ya 5 katika msimamo huku Tottenham ikiwa na alama 5 na kushika nafasi ya 9
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: BASI LA MWENDOKASI LAUNGUA MOTO

- Limewaka moto likiwa maeneo ya Kimara Mwisho huku chanzo cha moto huo ikidaiwa ni hitilafu kwenye injini

- Hakuna taarifa yoyote ya kifo wala mtu yeyote aliyepata majeraha kutokana na moto huo

Zaidi, soma https://jamii.app/BasiMwendokasiMotoKimara
MIAKA 80 YATIMIA TANGU KUTOKEA KWA VITA YA II YA DUNIA(1939)

> Rais wa Ujerumani na Poland wamefungua maadhimisho ya siku nzima ya kumbukumbu za miaka 80 tangu ilipoanza Vita ya Pili ya Dunia

> Maadhimisho hayo yamefanyika katika mji wa Wielun, ulioko katikati mwa Poland ambao ulikuwa ni wa kwanza kushambuliwa na vikosi vya utawala wa Wanazi wa Ujerumani

Soma - https://jamii.app/80YrsWorldWarII
#JFLeo
MCHEKESHAJI KEVIN HART APATA AJALI YA GARI

- Mchekeshaji huyo, raia wa Marekani amepata ajali mapema Jumapili akiwa na wenzake wawili huko Calabasas, California

- Hart na dereva Jared Black wameripotiwa kupata majeraha makubwa mgongoni

Soma https://jamii.app/HartAccidentCalifornia
#JFLeo
RAIS MUSEVENI KUFUNGUA MKUTANO WA WAFANYABIASHARA TANZANIA NA UGANDA

> Rais wa Uganda anatarajiwa kufungua mkutano wa Wafanyabiashara kati ya Uganda na Tanzania ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 1000 katika kujadili namna ya kuongeza biashara mpya baina ya nchi hizi

> Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Septemba 6, 2019 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dsm

Soma - https://jamii.app/MuseveniMkutanoBiashara
#JFLeo
MKUTANO JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA KUANZA LEO ZANZIBAR

> Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA) unatarajiwa kuanza leo ambapo utawaweka pamoja Viongozi zaidi ya 400 kutoka Afrika

> Baadhi ya nchi zitakazoshiriki ni Zambia, Ghana, Malawi, Nigeria, Cameroon, Afrika Kusini, Uganda pamoja na Tanzania

Zaidi, soma https://jamii.app/MkutanoJumuiyaMadola
MICHEZO: Klabu ya Sporting Lisbon ya Ligi Kuu Ureno, imeripotiwa kuanza mazungumzo na KRC Genk kwa ajili ya kupata saini ya nahodha wa Timu ya Taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta (27)

> Sporting Lisbon ndiyo klabu iliyomkuza staa wa Juventus, Christiano Ronaldo

#JFMichezo