JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TANGA: MKUU WA MKOA ANYANG'ANYA SHAMBA LA MWEKEZAJI NA KUWAGAWIA WANANCHI

- RC Shigela amerudisha kwa wananchi shamba la ekari 900 lililokuwa linamilikiwa na mwekezaji (Kampuni ya Hengya) ambaye ameshindwa kuliendeleza kwa miaka 3

Zaidi, soma https://jamii.app/RCTangaShamba
SERIKALI YAKIRI KUDAIWA BILIONI 95 NA WAKULIMA WA KOROSHO

- Imesema Wakulima na wadau wengine kama Wasafirishaji wanadai jumla ya Tsh. Bilioni 105

- Aidha, imebainisha kuwa hadi sasa ina korosho tani 200,000 kwa ajili ya kuziuza nje ya nchi

Zaidi, soma https://jamii.app/Serikali-WakulimaKorosho
MTOTO WA KOCHA LUIS ENRIQUE AFARIKI KWA SARATANI

- Xana (9), mtoto wa Kocha huyo wa zamani wa Barcelona, amefariki jana kutokana na Saratani ya mifupa

- Enrique (49) aliyewahi pia kuinoa timu ya Taifa ya Uhispania alijiuzulu kuifundisha kwasababu zilizotajwa ni binafsi
KISUTU: KESI YA KABENDERA YAPIGWA KALENDA TENA. AFYA YAKE YATAJWA KUZOROTA

- Kesi ya Mwandishi Erick Kabendera imeahirishwa tena hadi Septemba 12, 2019

- Kabendera ametajwa kupata shida ya upumuaji hasa usiku na kusababisha afya yake kuzorota

Zaidi, soma https://jamii.app/AfyaKabenderaKuzorota
KILIMANJARO: AJINYONGA BAADA YA NDUGU KUKATAA KUMCHANGIA HELA YA KUMZIKA MKEWE

- Mkazi wa Rombo, Ambros Marandu(54) amekutwa amejiua kwa kujinyonga kwenye mwembe

- Aliomba mchango kwani hakuwa na fedha baada ya kumuuguza mkewe kwa muda mrefu

Zaidi, soma https://jamii.app/AjinyongaMchangoMazishiMke
UGANDA: MTOTO WA MIAKA 9 ALIYEKUTWA NA UGONJWA WA EBOLA, AFARIKI

- Mtoto huyo alikutwa na Ebola baada ya kupimwa katika mpaka uliopo Wilayani Kasese akiwa anatokea Congo

- Mama yake aliyewasili naye, ametengwa akisubiri kurudishwa Congo

Zaidi, soma https://jamii.app/MgonjwaEbolaAfarikiUG
SOLSKJAER: CHRIS SMALLING YUPO MBIONI KUJIUNGA NA AS ROMA

- Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema beki huyo ameenda Italia kumalizia kuijunga kwa mkopo na AS Roma

- Desemba 2018, Smalling(29) aliongeza mkataba wa kubaki Old Trafford hadi mwaka 2022
EDEN HAZARD ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA EUROPA

- Hazard anayechezea Real Madrid ya kwa sasa, ameshinda tuzo hiyo kwa msimu wa mwaka 2018/19

- Msimu wa mwaka 2018/19 alikuwa anacheza Chelsea ambapo aliisaidia timu hiyo kuchukua Kombe la Europa kwa msimu huo
MICHEZO: MAKUNDI YA LIGI YA EUROPA 2019/20 YATANGAZWA

- Makundi ya Ligi ya Europa kwa msimu wa mwaka 2019/20 yametangazwa leo na UEFA huko Monaco

- Aidha, michezo ya kwanza ya Ligi hiyo inatarajiwa kuchezwa Septemba 19, 2019 huku fainali ikitarajiwa kuchezwa Mei 27, 2020
AFRIKA KUSINI: MAOMBI YA KUPINGA KUSHIKILIWA KWA NDEGE YA ATCL KUSIKILIZWA LEO

> Wakili Mkuu wa Serikali Msaidizi, Dkt. Ally Possi amesema kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wanasimamia suala hilo ili kuhakikisha ndege inaachiwa

Zaidi, soma > https://jamii.app/KesiNdegeSA
KINONDONI, DAR: KIJANA WA MIAKA 22 APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KULAWITI

> Abubakari Bakari, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kumlawiti Mtoto wa miaka 12

> Amekana mashtaka na kuachiwa kwa dhamana

Soma > https://jamii.app/KijanaTuhumaKulawitiDAR
AFYA: DAKTARI BINGWA ASHAURI VIJANA KUPIMA VINASABA (DNA) KABLA YA KUOANA

- Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu ktk Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Elineema Meda ametoa ushauri huo ili waepuke kupata Watoto wenye ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell)

Soma > https://jamii.app/UgonjwaSelimundu
WAZIRI LUGOLA AVIONYA VYAMA VITAKAVYOANZA KAMPENI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KABLA YA WAKATI

- Ametoa onyo kwa vyama vya siasa vilivyotangaza kufanya mikutano ya hadhara kabla ya muda uliopangwa

- Asema Jeshi lake litavishughulikia

Soma > https://jamii.app/LugolaVsVyamaSiasa
SONGWE: VIONGOZI WA CCM WAPIGWA MARUFUKU KUWATISHA WATUMISHI WA UMMA

- Mwenyekiti wa CCM Songwe, Eliniko Mkola asema Taasisi zote zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo ni vema wana CCM wakajua mipaka ya kiutendaji

Zaidi, soma > https://jamii.app/CCMVsWatumishiUmma
GUINEA-BISSAU: RAIS JOSE MARIO VAZ ALIYEMALIZA MUDA WAKE, ATANGAZA KUWANIA URAIS TENA

- Atagombea kama mgombea binafsi baada ya kutengwa na chama chake cha PAIGC na atakiungwa mkono na vyama vidogo ambavyo havina uwakilishi Bungeni

Zaidi, soma > https://jamii.app/JoseVaziKuwaniaTena
HANDENI, TANGA: ZAIDI YA WATUMISHI WA UMMA 45 WAFUKUZWA KAZI

- Watumishi waliofukuzwa ni watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo ya matumizi mabaya ya Fedha za Umma

- Afisa Utumishi wa Wilaya hiyo amesema kila idara imeguswa

Zaidi, soma https://jamii.app/WatumishiWafukuzwaHandeni
ARUSHA: MKUU WA MKOA AAGIZA KUSIMAMISHWA AFISA UGAVI NA MHANDISI UJENZI WA HALMASHAURI YA KARATU

- RC Mrisho Gambo ameagiza kusimamishwa kazi, Modestus Kastila na Venance Malamla kwa kushindwa kusimamia mradi wa soko na Hospitali ya Wilaya

Soma > https://jamii.app/Gambo-Karatu
KOREA KASKAZINI: KATIBA YAFANYIWA MAREKEBISHO NA KUMFANYA KIM JONG UN KUWA KIONGOZI WA JUU

- Bunge limepitisha mabadiliko ya Katiba na kumuongezea nguvu zaidi Kiongozi wao Kim Jong Un kuwa Kiongozi wa juu kama alivyokuwa Babu yake

Zaidi, soma > https://jamii.app/KimKatibaKorea
RUFIJI, PWANI: WATU WATANO WAFARIKI KWENYE AJALI YA GARI

- Watu watano wamefariki na mmoja kujeruhiwa baada ya lori la Dangote na gari dogo kugongana

- Lori liliteketea kwa moto papo hapo baada ya kugonga nguzo ya Umeme na kuangukiwa na nyaya

Zaidi, soma https://jamii.app/5WafarikiAjaliRufiji
LONDON: MAELFU KUANDAMANA KUPINGA UAHIRISHWAJI WA BUNGE

- Maandamano yameitishwa na wapinzani wa Brexit waitwao "Another Europe is Possible"

- Inadaiwa kuahirishwa kwa Bunge ni hila ya Serikali kuwanyima Wabunge kuzuia Uingereza kujiondoa EU

Zaidi, soma https://jamii.app/WaandamanaKupingaBunge-UK