JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UNHCR YAPINGANA NA TANZANIA. YASEMA BURUNDI SI SALAMA KWA WAKIMBIZI KURUDI

- Yasema hali hairuhusu kushinikiza Wakimbizi kurudi katika nchi hiyo

- Limezitaka Tanzania na Burundi kuhakikisha kuwa hakuna Mkimbizi anayerudishwa kwa kushurutishwa

Zaidi, soma https://jamii.app/UNHCRvsTZ-WakimbiziBRND
PWANI: POLISI YAMKAMATA KIJANA AKISAFIRISHA MAGUNIA 9 YA BANGI

> Francis Deogratias(30) mkazi wa Mwananyamala, Jijini Dar anayefanya kazi ya udereva, amekamatwa na magunia hayo ambapo kila moja lina uzito wa kilo 50

Zaidi, soma https://jamii.app/BangiYakamatwaPwani
KAHAMA, SHINYANGA: AMUUA MKEWE NA KISHA KUJIUA KWA SUMU

- Paschal Mahona(32) amejiua baada ya kumuua mkewe, Ashura Paschal(30) kwa kumnyonga

- Chanzo cha tukio hilo la Agosti 28 ni wivu wa mapenzi kwani kabla wawili hao walikuwa wakigombana

Zaidi, soma https://jamii.app/AuaMkeAjiua-Mapenzi
SERIKALI: TUTAWACHUKULIA HATUA WANAOSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU DAWA

> Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Ndugulile amesema kuna taarifa zinazoenezwa kuhusu madhara anayoweza kuyapata mtu iwapo atatumia aina fulani ya dawa

Zaidi, soma https://jamii.app/GvtVsWapotoshaji
UPDATE: Polisi imethibitisha msafara wa DC wa Kyela, Claudia Kitta kushambuliwa kwa mawe walipofika kumuokoa Mama aliyetaka kuuawa na Wananchi akidaiwa kumuua mwanaye

- Wananchi walikuwa wanataka mama huyo anayedaiwa kumuua mwanaye kwa imani za kishirikina, amfufue

Zaidi, soma https://jamii.app/MsafaraDCKyelaMawe
MAKUNDI YA UEFA KUPANGWA LEO. MCHEZAJI BORA KUTANGAZWA

- Droo ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya-2019/20 itachezeshwa leo saa 2:00 usiku

- Aidha, mchezaji bora wa msimu wa 2018/19 anatarajiwa kutangazwa ambapo Messi, C. Ronaldo na Van Dijk wanawania tuzo hiyo

Zaidi, fuatilia https://jamii.app/DrooUEFA2019-20
RAIS WA ITALIA AMUAGIZA WAZIRI MKUU ALIYEJIUZULU KUUNDA SERIKALI YA MSETO

- Rais wa Italia, Sergio Mattarella amemuagiza Giuseppe Conte kuunda Serikali mpya ili kuepuka kufanya uchaguzi mwingine

Zaidi, soma https://jamii.app/ConteSerikaliMpya
SIMBA YAANZA KUTETEA KOMBE LA LIGI KWA USHINDI

- Klabu ya Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya klabu ya JKT Tanzania

- Magoli ya Simba yamefungwa na M. Kagere (2’, 59’) na M. Athuman (74’) huku goli la JKT likifungwa na E. Songo (87’)
WAZIRI WA SERIKALI YA AWAMU YA TATU ATAJWA KWENYE KESI YA UHUJUMU UCHUMI

- Maokola Majogo, atajwa katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Mohamed Yusufali na wenzake wawili

- Adaiwa kumdhamini Alhaji Kilahama wakati akikopa dola laki 5

Zaidi, soma https://jamii.app/MajogoTuhuma
WAHUKUMIWA MIEZI 6 JELA KWA UZURURAJI NA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA NGONO

- Mahakama ya Mwanzo ya Nunge ya Manispaa ya Morogoro imewahukumu watu 22 kwa makosa hayo

- Washtakiwa hao ambao wengi ni Wanawake walikamatwa usiku wa Agosti 16, 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/JelaMiezi6Uzururaji
MICHEZO: Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) limetangaza Wachezaji bora wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita 2018/19 katika kila nafasi

- Kipa Bora ni Alison Becker (Liverpool), Beki Bora ni Virgil van Dijk (Liverpool), Kiungo Bora ni Frankie De Jong (Ajax) na Mshambuliaji Bora ni Lionel Messi (Barcelona)
MICHEZO: Shirikisho la Soka Barani Ulaya leo limepanga makundi ya timu zinazoshiriki Klabu Bingwa Ulaya msimu wa 2019/20

- Mechi za kwanza kwa msimu wa 2019/20 zinatarajiwa kuchezwa tarehe 17 na 18 Septemba, 2019 huku fainali ikitarajiwa kuchezwa Mei 30, 2020
VAN DIJK ATANGAZWA KUWA MCHEZAJI BORA WA KIUME WA UEFA

- Beki mahiri wa Liverpool ambaye ni raia wa Uholanzi, Virgil van Dijk ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa Kiume wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya kwa msimu wa mwaka 2018/19

- Van Dijk amefanikiwa kuwabwaga Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo na Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi
JamiiForums pinned a photo
KILIMANJARO: MAGARI 20 YALIYOIBWA NCHINI KENYA YAKAMATWA TANZANIA

- Magari hayo yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.7 yaliibwa kati ya mwaka 2018 na 2019

- Miongoni mwa magari hayo ni Landcruiser, Marcedes Benz, Prado, Probox, axio na Allion

Zaidi, soma https://jamii.app/MagariKenyaYakamatwaTZ