JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UPDATE: Watu 3 wanaodaiwa kuwa viongozi wa maandamano ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania yaliyofanyika nje ya Ubalozi wa Afrika Kusini wanashikiliwa na Polisi

- Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa amesema wao hawaruhusu maandamano wala mtu kufanya atakavyo

Zaidi, soma https://jamii.app/WatanzaniaWatakaNdege-UbaloziSA
DODOMA: JAFO ATAKA WATUMISHI WA IDARA YA ARDHI WACHAPWE VIBOKO

- Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Chamwino 'kuwachapa viboko' watumishi wa idara ya ardhi ili wapime viwanja kwa kasi kulingana na mahitaji

Zaidi, soma https://jamii.app/JafoWatumishiViboko
KINONDONI, DAR: RAIA WA MALAWI APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUMNAJISI MTOTO

- Paul John (30) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kumuingiza vidole sehemu za siri Mtoto wa miaka 7

Zaidi, soma => https://jamii.app/RaiaMalawaliKunajisi
BASHIRU ALLY APIGA MARUFUKU UWEPO WA SHIRIKISHO LA WALIMU WA CCM

- Amesema hawatambuani kwa taaluma na Katiba yao haisemi mwanachama awe mwalimu bali mwanachama ni mwanachama

- Asisitiza shughuli zote za chama ziendeshwe kwa mujibu wa Katiba

Zaidi, soma https://jamii.app/BashiruAkemeaShirikishoWalimuCCM
CHUO KIKUU UDSM CHAKANUSHA MATOKEO MABAYA KWA WANAFUNZI WAKE

- Taarifa zilienea kuwa takriban Wanafunzi 1,000 wamevurunda katika mitihani ya kumaliza muhula wa masomo

- UDSM wasema Baraza la Seneti linaloidhinisha matokeo bado halijakaa

Soma => https://jamii.app/KanushoUDSM
TETESI: UHAMISHO WA NEYMAR KWENDA BARCELONA MBIONI KUKAMILIKA

- Inadaiwa atajiunga na Barcelona kabla ya dirisha la usajili kufungwa kama Ousmane Dembele atakubali kujiunga PSG

- Inadaiwa PSG imeshusha thamani ya Neymar kutoka Tsh. Bilioni 566.7 hadi Tsh. Bilioni 434.8
GEITA: WASHTAKIWA WA MAUAJI YA ALPONCE MAWAZO, KIZIMBANI

- Washtakiwa watano wa mauaji ya aliyekuwa kada wa CHADEMA wamefikishwa Mahakama Kuu

- Mawazo, aliyekuwa pia Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita, alifariki kutokana na kupigwa

Zaidi, soma https://jamii.app/WauajiMawazoKizimbani-GIT
KENYA: KIONGOZI WA KANISA NA MKEWE WAKAMATWA KWA KUMFUKUZA AFISA WA SENSA

> Akhi Shilton na Bi. Akol Emmah wamesema hawawezi kuhesabiwa Duniani bali watahesabiwa mbinguni

> Majirani wasema wawili hao waliwahi kugoma Watoto wao wasipewe chanjo

Zaidi, soma https://jamii.app/WagomeaSensaNaivasha
TABORA: MTOTO AFARIKI AKICHEZA NA WENZAKE KWENYE MABOMBA YA MAJI

- Paul Moses (9) amefariki dunia alipokuwa na wenzake wakichezea mabomba makubwa ya kusafirishia maji

- Paul na wenzake walikuwa wayakisukuma na kuingia ndani ya mabomba hayo

Zaidi, soma https://jamii.app/MtotoAfarikiBombaMaji-TBR
DAR: YANGA YAPOTEZA MCHEZO WA KWANZA WA LIGI KUU BARA 2019/20

- Klabu ya Yanga imeanza vibaya michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufungwa goli 1-0 na klabu ya Ruvu Shooting

- Bao pekee la Ruvu Shooting katika mchezo huo limefungwa na Sadat Mohamed kunako dakika ya 21
ARUSHA: MZEE WA MIAKA 98 KULIPWA MILIONI 519.30 KAMA FIDIA YA KUPORWA ARDHI

- Malipo hayo yatatoka kwa Kaya 109 za wakazi wa Sinoni kwa kosa la kupora ardhi ya Bi. Nasi Muruo

- Kikongwe huyo, alinyang’anywa ardhi yake mwaka 1977

Zaidi, soma https://jamii.app/BibiArdhiFidia
UCHAGUZI WA PILI KIDATO CHA NNE: 1674 WACHAGULIWA, 187 WAKOSA NAFASI

- Uchaguzi ni baada ya baadhi ya wanafunzi kujiunga shule binafsi na baadhi ya shule kuongeza majengo

- Pia, Waliokosa nafasi ni kutokana na kutokamilika kwa tahasusi zao

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziKidato5-2019
MANYARA: KIJANA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA KUBAKA

- Pascal Mananga (22), amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kosa la kumbaka Mwanafunzi wa Kidato cha 3 katika Shule ya Sekondari Chief Dodo

Zaidi, soma https://jamii.app/JelaKubakaBabati
BASHIRU ALLY: NILITAMANI KUJIUZULU UKATIBU MKUU WA CCM

- Katibu Mkuu wa CCM amesema wadhifa alionao ulikuwa mzigo kwake na ilifikia wakati alitaka kujiuzulu

- Amesema Mwenyekiti wa Chama hicho, John Magufuli ndiye aliyemtia moyo na sasa amekomaa

Zaidi, soma https://jamii.app/BashiruUkatibuCCM
KOMBE LA CARABAO: RATIBA YA MZUNGUKO WA TATU YATANGAZWA

- Bingwa Mtetezi, Manchester City itakutana na Preston

- Liverpool, Arsenal, Chelsea na Manchester Utd nazo zimepangiwa wapinzani wao

- Michezo hii itachezwa kuanzia wiki inayoanza Septemba 23, 2019
NIGERIA: SERIKALI YAFUNGA MPAKA WAKE NA NCHI YA BENIN ILI KUDHIBITI MAGENDO

- Rais Buhari amesema kutakuwa na mkutano wa pamoja na nchi jirani za upande wa Kaskazini (Benin na Niger) ili kujadili kudhibiti biashara ya magendo

Zaidi, soma => https://jamii.app/NigeriaYafungaMpaka
WAZIRI MKUU UINGEREZA ADAIWA KUSITISHA BUNGE ILI ‘ASIBUGHUDHIWE KATIKA MAAMUZI’

> Wadau wadai uamuzi huu ulioafikiwa na Malkia utazuia Bunge kujadili Mpango wa #Brexit

> Wanaopinga Brexit wadai ni dalili za awali za udikteta

Zaidi, soma https://jamii.app/WaziriMkuuBungeUK
MBEYA: MSAFARA WA MKUU WA WILAYA WAPIGWA MAWE

- Ni msafara wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ukiongozwa na DC wa Kyela, Claudia Kitta

- Watu wawili wamejeruhiwa na Magari kuharibiwa baada ya msafara huo kushambuliwa katika kijiji cha Mpunguti

Zaidi, soma https://jamii.app/MsafaraDCKyelaMawe
UGANDA YAACHANA NA MRADI WA KUFUA UMEME KATIKA MAPOROMOKO YA MARCHISON

- Kusitishwa kwa mradi huo ambao ungezalisha Megawatt 360 kunaashiria Serikali ya Uganda imejihakikishia kuwa mradi huo ungechafua mandhari na kuvuruga mfumo wa ikolojia

Zaidi, soma https://jamii.app/UgandaVsMarchison