JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI YAWAONYA WANAOWAPA SIMU WATOTO CHINI YA MIAKA 18

- Imewaonya wazazi au walezi wanaowaruhusu watoto kumiliki simu na laini

- Imesema watoto hawawezi kusajiliwa kutumia simu na wakipata matatizo waliosajili kwa niaba yao ndio watakamatwa

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliVsWazaziWatotoSimu
ZANZIBAR: MTOTO ANUSURIKA KUFA KWA KUBWIA DAWA ZA KULEVYA

- Mtoto huyo mwenye mwaka na miezi 6 alifikishwa hospitalini Agosti 18 baada ya kudaiwa kubwia ‘cocaine’

- Mama wa mtoto alieleza kuwa mtoto wake alikula dawa hizo baada ya kuziokota

Zaidi, soma https://jamii.app/MtotoAbwiaCocaine
MWANAFUNZI AMSHTAKI MUSEVENI KWA KUMZUIA(BLOCK) TWITTER

- Hillary Seguya anayesoma Harvard(Marekani) pia amewashtaki Msemaji wa Serikali na Mkuu wa Siasa wa Polisi

- Awasilisha ushahidi wa Tweets 27 za kiutendaji ambazo hazikumfikia

Zaidi, soma > https://jamii.app/SeguyaVsMuseveni
DAR: ANAYETUHUMIWA KUBAKA WAKE ZA WATU AFUNGULIWA KESI

- Ahmed Mohamed amefunguliwaa mashtaka yakiwamo ya uhujumu uchumi Mahakamani Kisutu

- DPP Mganga amedai Mohamed amekuwa akiwabaka, kuwaingilia kinyume cha maumbile na kuwaibia wanawake

Zaidi, soma https://jamii.app/MdhalilishajiWanawakeAshtakiwa
DAR: MFANYABIASHARA ALIYEMUUA MKEWE NA KUMCHOMA MOTO, AIOMBA MAHAKAMA IMPATIE FEDHA ZAKE

- Hamis Said(38), aomba apatiwe fedha zake zaidi ya Tsh. Milioni 5 zilizopo kwenye laini 2 za simu

- Asema anazihitaji kwa matumizi yake na karo ya Mtoto

Zaidi, soma > https://jamii.app/MtuhumiwaFezaSimu
KENYA: NYIMBO ZA 'TETEMA' NA 'WAMLAMBEZ' ZAPIGWA MARUFUKU NJE YA KLABU

- Wimbo wa Rayvanny na Diamond (Tetema) na wa Sailors (Wamlambez) kuchezwa klabuni na baa tu

- Inaelezwa maneno ktk nyimbo hizo ni uchafu na hayafai kusikilizwa hadharani

Zaidi, soma https://jamii.app/TetemaWamlambezMarufukuHadharani-KE
MKAKATI KUWASAJILI WACHEZA MICHEZO YA KUBAHATISHA WAJA

- Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kuweka mfumo utakaowasajili wacheza michezo hiyo ili kuwadhibiti

- Mkurugenzi Mkuu wa bodi, amesema michezo hiyo ina madhara ya kiuchumi na kisaikolojia

Zaidi, soma https://jamii.app/MkakatiKusajiliWachezaKamari
UBELGIJI: WATUHUMIWA WA MAUAJI YA KIMBARI NCHINI RWANDA KUSHTAKIWA

- Watuhumiwa hao ni Fabien Neretse, Emmanuel Nkunduwimye na Ernest Gakwaya

- Wote wanatuhumiwa kujihusisha na kikundi cha Interahamwe kilichofanya ubakaji na mauaji 1994

Soma > https://jamii.app/MauajiRwandaBrussels
BRAZIL YAKATAA MSAADA WA G7 HUKU MOTO UKIZIDI KUTEKETEZA MSITU WA AMAZON

- Imeukataa msaada uliokusudiwa kusaidia kudhibiti moto ulioharibu hekari milioni 2.3 za msitu

- Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro ametilia shaka msaada huo na kuhoji dhamira yake

Zaidi, soma https://jamii.app/BrazilYakataaMsaadaG7
KATIBU MKUU WA CCM AMPONGEZA ASKARI ALIYEKATAA KUTOA SALAMU YA CCM

- Dkt. Bashiru Ally amempongeza Askari wa Mkoani Pwani aliyegoma kutumia salamu za chama

- Askari huyo alipotakiwa kutumia salamu ya CCM, alikataa na kusema Askari hana chama

Soma https://jamii.app/BashiruAmpongezaAskari
LHRC WAKEMEA VIKALI KAULI YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI ILIYOTOLEWA NA DC KIGAMBONI

- LHRC waeleza kusikitishwa na kauli ya hiyo ya Sara Msafiri aliyesema wezi na vibaka watavunjwa miguu na kuachwa na ulemavu kabla ya kufikishwa Mahakamani

Zaidi, soma > https://jamii.app/LHRCVsDCKigamboni
MDAU: MUME WANGU ANANILAZIMISHA NIJITOE KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK

- Mdau wa JamiiForums kupitia Jukwaa la Mapenzi, Mapenzi na Urafiki anasema kuwa Mume wake hataki kumuona akitumia mtandao huo

- Anasema kuwa yeye anakutana na rafiki zake wengi kupitia mtandao huo na pia anafurahia kujumuika na watu na kushiriki mijadala inayoendelea huko

Kujadili, tembelea https://jamii.app/MumeHataki-FB
WATANZANIA WAWILI NA MKENYA MMOJA WASHTAKIWA KWA UTAPELI

- Titus Fedha, Haji Shariff na Suleiman Salum wanadaiwa kujipatia takribani Tsh. Milioni 44.4 kwa kudai kuwa wanaweza kulisafisha shamba la Harbans Singh dhidi ya nguvu za giza

Zaidi, soma https://jamii.app/WatanzaniaMkenyaKizimbaniUtapeli
UGANDA KUANZA KUUZA BANGI KIMATAIFA

- Wakaguzi wa Umoja wa Ulaya wameidhinisha Uganda kutuma bangi barani humo kwa matumizi ya matibabu

- Uganda ni nchi pekee Afrika Mashariki iliyohalalisha uzalishaji wa bangi japo ni kwa matumizi ya dawa

Zaidi, soma https://jamii.app/UgandaBangiKimataifa
DAR: BINTI WA MIAKA 21 AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA NOTI 20 ZA BANDIA

- Mariam Zuberi (21), alikamatwa akiwa na noti hizo Juni 27 mwaka huu(2019)

- Hata hivyo, mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na kuachiwa kwa dhamana

Zaidi, soma https://jamii.app/KizimbaniNotiFeki
SAMIA SULUHU: SINA NIA YA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

- Makamu wa Rais, Samia Suluhu amesema maneno ya kuwa anataka kugombea Urais Zanzibar ni uongo

- Amesema kwenye ngazi za uongozi za Tanzania, yeye ni namba 2 na hana nia ya kwenda kuwa namba 3

Zaidi, soma https://jamii.app/SamiaHatakiUraisZNZ
RAIS WA UGANDA, YOWERI MUSEVENI ASEMA HANA HARAKA YA KUSTAAFU

- Amesema hana mpango wa kumwandaa mrithi wa nafasi yake

- Ameeleza kuwa kwa sasa anajikita katika kuimarisha ukuaji wa Uganda na bara la zima la Afrika

Zaidi, soma https://jamii.app/MuseveniVsKustaafu
RAIS WA KWANZA WA GAMBIA, DAWDA JAWARA AFARIKI

- Alianza kujihusisha na siasa mwaka 1960 baada ya kurejea Gambia akitokea Scotland

- Mwaka 1950 alijiunga na chama cha Progressive People na baadaye kuwa Rais hadi 1994 alipopinduliwa na Yahya Jammeh

Soma https://jamii.app/RIPJawara
TETESI: MANCHESTER UNITED YAKUBALI SANCHEZ AENDE INTER MILAN KWA MKOPO

- Inter Milan imekubali kulipa takribani Tsh. Bilioni 12.6 ikiwa ni sehemu ya Tsh. Bilioni 59.2 ya Mshahara wa Alexis Sanchez kwa mwaka

- Sanchez anadaiwa kuwa atakamilisha vipimo vya afya leo
DAR: WATU WAKUSANYIKA NJE YA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI WAKIDAI NDEGE

- Watu hao wanashinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania inayoshikiliwa Afrika kusini

- Ndege inashikiliwa kutokana na kesi ya fidia ya Hermanus Steyn dhidi ya Tanzania

Zaidi, soma https://jamii.app/WatanzaniaWatakaNdege-UbaloziSA