JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Klabu ya Simba imetolewa hatua ya awali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya UD Songo ya Msumbiji

> Mchezo huu umechezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar
KIGOMA: TANZANIA KUWAREJESHA BURUNDI WAKIMBIZI 2000 KILA WIKI

- Tanzania na Burundi zimesaini makubaliano ya kuwarejesha Wakimbizi waliopo katika Kambi ya Nduta na Mtendeli kuanzia Oktoba Mosi, 2019 kutokana na amani iliyopo katika nchi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/WakimbiziBNDKurejeshwa-TZ
KENYA: WATU 8 WAUAWA KATIKA MASHAMBULIO YA RISASI

- Wengine 9 walijeruhiwa baada ya kushambuliwa hapo jana katika maeneo ya Forole na Sabareh kwenye Kaunti ya Marsabit

- Wavamizi hao wanaodhaniwa wametoka Ethiopia waliondoka na mifugo

Zaidi, soma https://jamii.app/8DeadMarsabitAttacks
WAMILIKI WA 'VIBANDA' VYA KUONESHA MPIRA WA MIGUU WAITWA TFF

- TFF imewaita watu wote wanaoonesha mpira katika 'vibanda' Mkoani Dar kwa ajili ya majadiliano ya ushirikiano

- Majadiliano hayo yatafanyika kesho Agosti 27, katika ofisi za TFF

Zaidi, soma https://jamii.app/WamilikiVibandaMpiraTFF
UGANDA: MWANAMKE AJIFUNGUA WATOTO 5

- Sofiat Mutesi(37) amejifungua Mtoto mmoja katika kituo cha afya cha Ivukula na kuhamishiwa katika Hospitali ya Iganga-Nakavule alikojifungua wanne

- Aliwahi kujifungua mapacha katika uzao wa kwanza na watoto 3 katika uzao wa pili

Zaidi, soma https://jamii.app/Watoto5UG
SERIKALI: SHERIA ZA BARABARANI KUONGEZEWA MAKALI

- Imesema ipo kwenye mchakato wa kuangalia upya sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuziongezea makali

- Imesema lengo ni kukabiliana na madereva wanaovunja sheria mara kwa mara

Zaidi, soma https://jamii.app/SheriaBarabaraniMakali
DC KIGAMBONI: WEZI NA VIBAKA WATAPIGWA NA KUVUNJWA MIGUU KABLA YA KUPELEKWA MAHAKAMANI

> Sarah Msafiri amesema wezi na vibaka watapigwa na kuvunjwa miguu ili wasiendelee na kazi hiyo kwasababu wakipelekwa Mahakamani wanatoka kwa dhamana

Zaidi, soma https://jamii.app/DCKingamboniVsWezi
BASATA, COSOTA NA BODI YA FILAMU KUUNGANISHWA

- Serikali yataka kuunda Mamlaka moja ya kusimamia Sekta ya Sanaa na Ubunifu ili kuiboresha

- Wasanii, Watunzi, Waandishi na Wabunifu wote wa Sanaa wamekaribishwa katika mkutano wa kujadili mchakato huo

Zaidi, soma https://jamii.app/KuundwaMmamlaka1Sanaa
KENYA: MCHUNGAJI ATUHUMIWA KUPORA MKE WA MUUMINI

- John Kanyua amesema haamini imekuwaje Mchungaji aliyewafungisha ndoa amgeuke

- Mchungaji huyo wa Kanisa la Joy Springs alianza kwa kumteua mkewe, Leah Wambui(26) kuwa mchungaji msaidizi

Zaidi, soma > https://jamii.app/MchungajiMkeMuumini
KAJIADO, KENYA: MTOTO WA MIAKA 9 AOKOLEWA KUOLEWA NA MWANAUME WA MIAKA 30

> Chifu Ilmarba Felix Maitei, aliwaongoza machifu wenzake hadi katika nyumba ambayo Mtoto huyo mwanafunzi wa darasa la 3 alikuwa akiozwa

Zaidi, soma => https://jamii.app/MtotoKuozwaKajiado
UPDATE: IDADI YA VIFO VYA AJALI YA LORI LA MAFUTA MROGORO YAFIKIA 102

- Idadi hiyo imeongezeka baada ya majeruhi mwingine kufariki leo

- Majeruhi mwingine alifariki siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita na kuifanya idadi hiyo kuwa 101
UHISPANIA: WATU 7 WAFARIKI BAADA YA HELIKOPTA NA NDEGE KUGONGANA

- Ajali imetokea jana katika kisiwa cha Mallorca baada ya ndege ndogo na helikopta kugongana angani

- Watu watano wakiwemo watoto wawili walikuwemo kwenye helikopta na watu wawili kwenye ndege

Zaidi, soma https://jamii.app/7DeadPlaneHelicptrCollide
MWANAFUNZI AHUKUMIWA KWA KUCHAPISHA MAUDHUI MTANDAONI BILA LESENI YA TCRA

- Mwanafunzi wa mwaka wa pili, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Julius Warioba (23) amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 5 au kwenda jela mwaka mmoja, ikiwa ni baada ya kukiri kosa

Zaidi, soma https://jamii.app/MwanafunziNITAhukumiwa-LeseniTCRA
KIBAHA, PWANI: AKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 3

- Aliyekamatwa ni Dismas Silyvester(35) baada ya kukutwa akiwa na Mtoto huyo ktk mashamba ya mboga mboga

- Mtuhumiwa alimuiba Mtoto huyo na kwenda kichakani kumbaka

Soma > https://jamii.app/MbaroniKubakaKibaha
NGARA, KAGERA: WAKAMATWA KWA KUIBA MAFUTA BAADA YA LORI KUANGUKA

- Watu 8 mbaroni kwa tuhuma za wizi wa mafuta kwenye gari lililopata ajali Kijiji cha Mshikamano maarufu Machinjioni

- Pia, lita 300 za mafuta zilizoibwa katika tukio hilo zimekamatwa

Zaidi, soma https://jamii.app/WalioibaMafutaLoriBKMbaroni
ARUSHA: ZAIDI YA WATU 5 WAFARIKI KATIKA AJALI

- Wanadaiwa kufariki katika ajali iliyohusisha Fuso na Noah kugongana katika maeneo ya Mirombo, usiku wa kuamkia leo

- Bado haijafahamika chanzo cha ajali hiyo ambapo watu kadhaa wamejeruhiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/AjaliArushaMirombo
KENYA YAANZA KUUZA MAFUTA GHAFI KWENDA NJE YA NCHI

- Rais Uhuru Kenyatta amezindua safari ya kwanza ya usafirishaji wa mafuta hayo

- Ameshuhudia meli yenye mapipa 200,000 ya mafuta ya thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 26.6 ikielekea Uingereza

Zaidi, soma https://jamii.app/KEKuuzaMafutaGhafi
MWANZA: WADAU WA USAFIRISHAJI WASUSIA KIKAO CHA LATRA

- Kikao kilihusu uchukuaji maoni ya kuboresha rasimu za kanuni zitakazotumika katika sheria ya LATRA

- Ni baada ya kuambiwa baadhi ya marekebisho yao hayawezekani kwani ni sheria tayari

Zaidi, soma https://jamii.app/LATRAvsWadauUsafirishaji