JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TMDA YATOA UFAFANUZI KUHUSU UVUMI WA DAWA AINA YA P-500 (PARACETAMOL)

> Mamlaka ya Dawa na Vifaa imesema dawa hiyo haijasajiliwa na hakuna uthibitisho wa kuwepo kwenye soko la Tanzania na pia kiwanda husika hakitambuliki nchini

> Inawaomba wananchi kutosambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa na kupatiwa ufafanuzi na Mamlaka husika

Soma - https://jamii.app/NoP500ParacetamolTz
#JFLeo
RIPOTI: UHALIFU WAPUNGUA NCHINI KATIKA KIPINDI CHA NUSU YA MWAKA

> Serikali imesema katika kipindi cha Januari hadi Juni 2019 uhalifu umepungua kwa 2.2% kwa makosa makubwa ya jinai ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2018

> Makosa makubwa ya jinai ni Makosa dhidi ya binadamu, dhidi ya Maadili ya Jamii, Makosa ya kuwania mali na Uhalifu wa Kifedha

Soma - https://jamii.app/RipotiPunguoUhalifu
#JFLeo
MICHEZO: Kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda, Farouk Miya (21), amepiga hatua kisoka baada ya kufanikiwa kujiunga na Klabu ya Konyaspor ya Ligi Kuu ya Uturuki akitokea timu ya Gorica ya nchini Croatia

> Miya amesaini mkataba wa miaka mitatu na alikuwa sehemu ya kikosi cha Uganda The Cranes katika michuano ya AFCON 2019 nchini Misri

#JFMichezo
IFAHAMU SHERIA KATIKA HAKI YA KUDAI FIDIA AHADI YA KUOA AU KUOLEWA INAPOVUNJWA

> Kifungu cha 69 cha Sheria ya ndoa 1971 kinatoa haki kwa wapenzi kupeleka shauri Mahakamani na kudai fidia kutokana na kuvunjwa kwa ahadi ya ndoa

> Pia, Kifungu cha 70 kinaweka ukomo wa muda wa kupeleka shauri Mahakamani kudai fidia kufanyika kwa kipindi cha mwaka 1 tangu ahadi hiyo ilipovunjwa

> Aidha, kifungu cha 71 kinatoa haki ya kurudishiwa zawadi zilizotolewa na mmoja kati ya wachumba hao kwa matarajio ya kufunga ndoa

Fahamu zaidi hapa - https://jamii.app/SheriaAhadiNdoa
#JFLeo
CAMEROON: MWANAHARAKATI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA

- Ni Kiongozi wa 'Vuguvugu la eneo wanapozungumza Kiingereza', Sisiku Julius Ayuk Tabe na wafuasi wake 9

- Wamekutwa na hatia katika makosa ya Ugaidi na Kutangaza kujitenga nchi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/MwanaharakatiJelaMaisha-CRM
AUSTRALIA: MAHAKAMA YAKATAA RUFAA YA HUKUMU YA KARDINALI

> Mahakama Kuu imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu ya miaka sita kwa Kardinali wa Kanisa Katoliki, George Pell (78) aliyehukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kuwalawiti watoto wawili wa kiume

> Mpaka sasa, ameshatumikia kifungo hicho kwa miaka mitatu na miezi nane

Soma - https://jamii.app/RufaaKardinaliPell
MUHIMBILI: VIFO VYA MAJERUHI WA MOTO VINATOKANA NA KUUNGUA KWA 80% - 90%

> Daktari bingwa wa upasuaji amesema majeruhi wa ajali ya lori, Morogoro wanapoteza maisha kutokana na wengi wao kuungua zaidi sehemu za ndani kama vile mfumo wa hewa na figo

> Pia, kutokana na ngozi zao kuungua kwa asilimia kubwa hali hiyo imesababisha mwili kukosa kinga na kupoteza maji mengi

Soma - https://jamii.app/ChanzoVifoMajeruhiMoto
#JFLeo
KENYA: BAA ZAAGIZWA KUFUNGWA KWA SIKU MBILI KUPISHA ZOEZI LA SENSA

- Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang’i ameagiza kufungwa kwa baa zote kwa siku za Jumamosi na Jumapili hadi saa 11:00 jioni ili kurahisisha zoezi la kuhesabu Watu

Zaidi, soma https://jamii.app/BaaKufungwaHadiJioni-KE
KENYA: AMUUA NDUGUYE WAKIGOMBANA KUHUSU NANI APIKE

- Mtuhumiwa Patrick Simwa(45) alikasirishwa na mdogo wake, Evans Alumasa(30) kuleta chakula na kumtaka apike

- Inadaiwa baada ya kukataa, Evans alimpiga kibao na yeye kumpiga na kitu kichwani

Zaidi, soma https://jamii.app/AuawaMgogoroKupika-KE
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
PAUL KAGAME AONGELEA SAKATA LA RWANDA KUDAIWA 'KUPIKA' TAKWIMU ZA UCHUMI

- Amesema iwapo 'walipika' takwimu basi walikuwa hawamdanganyi mtu bali walijidanganya wenyewe

- Ameongeza kuwa hadhani kama wanataka kuwaridhisha wanaoandika hayo, ila wanataka kujiridhisha wenyewe
DAR: WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUENDESHA BIASHARA YA UPATU

- Magdai Gothard na Halima Nsubuga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 21 wakikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kuendesha biashara ya upatu

Zaidi, soma https://jamii.app/KisutuKosaUpatu
CHINA YASEMA HAITARUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA

> China imetangaza kuwa haitaruhusu ndoa za watu wa jinsia moja, licha ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati kuitaka Beijing kufuata nyayo za Taiwan

> Msimamo wa kisheria unabaki wa kutambua kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke

Soma - https://jamii.app/ChinaBansHomosexuality
#JFLeo
BENKI YA DUNIA KUIKOPESHA TANZANIA ZAIDI YA TSH. TRILIONI 3.9

- Imesema ipo tayari kutoa mkopo wa masharti nafuu wa zaidi ya Tsh. Trilioni 3.9 ikiwa ni fedha zilizobaki katika fungu la awamu ya 18 ya mgao wa Chama cha Kimataifa cha Maendeleo

Zaidi, soma https://jamii.app/MkopoBenkiDunia-TZ
KAMATI YA PAC KUKAGUA MIKATABA YA ZABUNI BENKI YA POSTA

> Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali imeiagiza Benki ya Posta Tanzania kupeleka mikataba 2 ya zabuni ya utengenezaji wa nembo ya benki hiyo kwa ajili ya kuipitia baada ya kubaini upungufu

> Pia imeitaka kuhakikisha Novemba, 2019 inapeleka majibu kuhusu maeneo yaliyoibua mkanganyiko

Soma - https://jamii.app/UkaguziZabuniTPB
BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA MAZIWA YAVUNJWA

- Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameivunja Bodi hiyo kwa kutoridhishwa na utendaji

- Ameivunja chini ya kifungu cha sheria ya Bodi ya Maziwa namba 8 ya mwaka 2004 kifungu cha 8 na 9(1)

Zaidi, soma https://jamii.app/BodiWakurugenziBodiMaziwa
MBEYA: WATU WANNE WAKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI

> Zungu Paulo Tinya [45] na Baraka Lazaro Timotheo [40], wote wakazi wa Kijiji na Kata ya Lupa wamekamatwa na vipande vitatu vya Meno ya Tembo bila kibali

> Aidha, wengine 2, wote wakazi wa Kijiji cha Isangawana wamekamatwa na vipande kumi vya meno ya Tembo bila kibali

Soma - https://jamii.app/MbaroniNyaraSerikali
#JFLeo
DRC: WATU 18 WAFARIKI KWENYE AJALI

> Watu wengine 21 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ya gari iliyotokea nje kidogo na mji wa Kinshasa

> Chanzo ni uzembe wa dereva, ambaye baada ya kuona amechoka na safari alimruhusu msaidizi wake ambaye hana uzoefu wa kuendesha gari hilo

Soma - https://jamii.app/18DeadRoadAccident
MAHAKAMA YAKATAA MATOKEO YA UCHUNGUZI WA RUSHWA DHIDI YA JACOB ZUMA

> Mahakama nchini Afrika Kusini imetupilia mbali matokeo ya uchunguzi uliowasafisha maafisa wa Serikali kwa tuhuma za rushwa kuhusu manunuzi ya zana za kijeshi ambapo Rais wa zamani, Jacob Zuma alikuwa mtuhumiwa

> Uchunguzi ulihitimisha kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu makosa ya rushwa na udanganyifu

Soma - https://jamii.app/CourtAnnulsFindings
HARMONIZE AOMBA KUJITENGA NA KUNDI LA WASAFI

- Uongozi wa kundi umesema ametuma barua ya maombi kuvunja mkataba wake kwa kufuata sheria

- Aidha, umesema umefurahia hatua hiyo kwani labda kuna vitu Harmonize ameona akivifanya atafika mbali

Zaidi, soma https://jamii.app/HarmonizeKuondokaWCB
KENYA YACHAGULIWA KUWA MJUMBE BARAZA LA USALAMA UN

> Kenya imepata kura 37 dhidi ya 13 za Djibouti wakati wa uchaguzi ulioandaliwa na Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi ya Umoja wa Afrika

> Anakuwa mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Soma - https://jamii.app/KEMjumbeBarazaUN