JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIA WA KENYA ALIYEJIFANYA MCHUNGAJI AKAMATWA MKOANI RUVUMA

- Adinikas Kyuvu amekamatwa Mjini Songea kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za utapeli

- Anatuhumiwa kujifanya Mchungaji na kuendesha ibada zilizojaa udanganyifu

Soma > https://jamii.app/MkenyaAkamatwaSongea
AFRIKA KUSINI: MADUKA YA RAIA WA KIGENI YAVAMIWA NA KUPORWA

- Raia wa Afrika Kusini wanadai wageni wanachukua fursa zao za ajira na uchumi

- Maeneo yaliyoathiriwa na uvamizi ni Moroka, Dlamini, Protea Glen, Dobsonville, Rockville na Zola

Soma > https://jamii.app/WageniVsWazawaSA
GHANA: MWANAMKE AFUNGUA AKAUNTI FEKI ILI AMCHUNGUZE MPENZI WAKE, APEWA JIBU LA KUSHANGAZA

> Baada ya kufungua akaunti hiyo feki, Mwanamke huyo alianza kuwasiliana na mpenzi wake na kumhoji maswali mbali mbali kuhusu maisha yake ya mahusiano

> Katika hali iliyomshangaza Akosuah May ambaye ni muuguzi, Mwanaume huyo alimjibu kuwa mpenzi wake alifariki miezi miwili iliyopita

Zaidi, soma => https://jamii.app/MahusianoUaminifu
BARIADI, SIMIYU: RAS AKATAA WATUMISHI WA HOSPITALI KUNUNUA KIFAA CHA 'ULTRA SOUND' KILICHOIBWA

- Atengua uamuzi wa DC kuwataka Watumishi hao kuchanga fedha ili kukinunua

- Asema haliwezi likawa jambo la kila mtu, muhusika lazima apatikane

Soma https://jamii.app/RASvsDC-UltraSound
FAHAMU KUHUSU HISTORIA YA BIBI TITI

>Bibi Titi Mohammed alizaliwa Juni, 1926 na aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge, Uongozi wa Wilaya ya Rufiji na Mufindi, Rais wa Umoja wa wanawake Tanganyika(UWT) na baadae Waziri

> Akiwa na miaka 16 tu alikuwa mmoja kati ya wanawake wachache walioaminiwa katika kuongoza mapambano dhidi ya udhalimu waliokuwa wakifanyiwa Watanganyika

> Mwaka 1968 ,yeye pamoja na aliyekuwa Waziri wa ulinzi, walihusishwa na matukio ya uhaini na kuhukumiwa kifungo cha maisha lakini mwaka 1972 waliachiwa kwa msamaha wa Rais

> Alifariki Novemba, 2000 baada ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo

Soma zaidi - https://jamii.app/HistoriaBibiTiti
#JFHistoria
MOROGORO: BASI LA ABIRIA LAGONGANA NA LORI, WATANO WAFARIKI NA 26 WAJERUHIWA

- Ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo imelihusisha basi la Safari Njema lililogongana na Lori aina ya Tata, mali ya kiwanda cha Tumbaku cha Alliance One

Soma => https://jamii.app/AjaliBasiLoriMoro
MIFUKO YA PLASTIKI YABAINIKA KUENDELEA KUTUMIKA SOKO LA KARIAKOO

> Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene baada ya kufanya ziara katika soko hilo amebaini uwepo wa mifuko hiyo inayotumika kama vifungashio kinyume cha utaratibu

> Atoa siku 14 iondolewe sokoni

Soma - https://jamii.app/MifukoPlastikiKkoo
LINDI: MUME NA MKE WANUSURIKA KIFO BAADA YA KULIPUKIWA NA MAFUTA YA PETROLI

- Walionusurika ni Shafii Selemani na Liuza Shafii wakazi wa Mtumbya

- Shafii Selemani ni dereva bodaboda na alikuwa amehifadhi dumu la lita 5 ndani ya nyumba yake

Soma >https://jamii.app/MotoNyumbaLindi
RWANDA: MWAKILISHI WA UPINZANI ATOWEKA TANGU JULAI 15

> Eugène Ndereyimana, Mwakilishi wa Chama cha Upinzani Mashariki mwa Rwanda hajulikani alipo kwa siku 30 sasa, tangu alipotoweka Julai 15, wakati akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano

> Pia, Mwandishi wa habari wa TV1 Rwanda, Constantin Tuyishimire naye hajulikani alipo kwa siku 29 sasa, tangu alipotoweka Julai 16

Soma - https://jamii.app/OppositionLeaderMissing
#JFLeo
MAREKANI YAMUWEKEA VIKWAZO ALIYEKUWA MKUU WA IDARA YA UJASUSI SUDAN

> Salah Gosh, ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Ujasusi wakati wa utawala wa Omar al-Bashir anatuhumiwa kuhusika katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Sudan hasa mauaji ya wapinzani na wakosoaji wa Omar al-Bashir

> Yeye na familia yake wamepigwa marufuku kuingia Marekani

Soma - https://jamii.app/USBanSalahGosh
#JFLeo
KAMPUNI YA HUAWEI YATUHUMIWA KUZISAIDIA SERIKALI ZA AFRIKA KUWADUKUA WAPINZANI

- Kampuni hiyo ya China inatuhumiwa kwa kuisaidia Zambia, Uganda na baadhi ya Serikali nyingine za Kiafrika katika kudukua taarifa za wapinzani

Soma => https://jamii.app/HuaweiVsAfricanGvt
POLISI WAZUIA MKUTANO WA ZITTO KABWE, ADO SHAIBU ACHUKULIWA NA POLISI

> Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika leo saa 5 asubuhi na mpaka sasa Polisi hawajatoa sababu za kuuzuia

> Aidha, Polisi wamemchukua Katibu wa Itikadi ACT Wazalendo, Ado Shaibu kwa ajili ya mahojiano baada ya kumkosa Zitto

Soma - https://jamii.app/ZuioMkutanoZitto
MICHEZO: Kesho timu za mpira za Simba na Azam wanatarajiwa kuvaana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2019-2020

> Timu hizo zitaumana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam saa 1 usiku

#JFMichezo
TETESI ZA SOKA: ALEXIS SANCHEZ KWENDA KUCHEZA SOKA ITALIA

- Inadaiwa yupo tayari kwenda kucheza katika ligi ya Serie A anapowaniwa na Juventus, Napoli, AC Milan na Inter Milan

- Inaelezwa hapewi kipaumbele katika kikosi cha kwanza cha Man. Utd chini ya Kocha Solskjaer

#JFLeo
KENYA: MUME AMKATA MIKONO MKE WAKE KWA MADAI YA KUTOKUZAA

> Jackline Mwende Mkazi wa Kijiji cha Kathama, amekatwa mikono yote na Stephen Ngira Thenge kwa kutumia kisu akidai ameshindwa kumzalia watoto kwa miaka 7 ya ndoa

> Jackline amesema kutokana na vipimo walivyofanya hospitali mumewe ndiye alionekana kuwa na tatizo kwenye uzazi

Soma - https://jamii.app/AkatwaMikonoKutokuzaa
SERIKALI YAAGIZA UCHUNGUZI DHIDI YA WIZI WA 'ULTRA SOUND' YA HOSPITALI SIMIYU

- Waziri wa TAMISEMI, ametengua agizo la Mkuu wa Wilaya ya Bariadi aliyewataka watumishi 137 wa Hospitali ya Somanga wachange fedha za kulipa mashine hiyo

Zaidi, soma => https://jamii.app/RASvsDC-UltraSound
BODI YA MIKOPO YA ELIMU YAONGEZA MUDA KWA WAOMBAJI MIKOPO

> Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imeongeza muda wa kuomba mkopo kwa njia ya mtandao hadi Agosti 23, mwaka huu ili kuwapa fursa waombaji ambao hawajakamilisha maombi yao kufanya hivyo

> Mpaka sasa bodi imeshapokea maombi zaidi ya 74,821 yaliyokamilika kwa njia ya mtandao

Soma - https://jamii.app/EducnLoansDeadline
#JFLeo
TETESI ZA SOKA: ALEXIS SANCHEZ KWENDA KUSAKATA KABUMBU NCHINI ITALIA
-
Inadaiwa Mchezaji huyo raia wa Chile anayekipiga katika klabu ya Manchester United yupo mbioni kwenda kujiunga na klabu moja kwenye ligi ya Serie A
-
Mchezaji huyo (30) aliyewahi kuchezea klabu ya Udinese ya nchini Italia miaka 8 iliyopita, anadaiwa kuwa tayari kurudi Serie A anapowaniwa na vilabu vya Juventus, Napoli, AC Milan na Inter Milan
-
Inaelezwa Sanchez kwa sasa hapewi kipaumbele na Kocha Ole Gunnar Solskjaer anayetajwa kuwapa kipaumbele Wachezaji Marcus Rashford, Anthony Martial, Daniel James na Mason Greenwood
CHUNYA: SERIKALI YABAINI UTOROSHAJI WA DHAHABU

> Zaidi ya nusu ya madini ya dhahabu yanayonunuliwa na wanunuzi wa kati kutoka kwa wachimbaji wadogo hutoroshwa badala ya kupelekwa soko kuu

> Imebainika kiasi kikubwa cha dhahabu inayouzwa sokoni hapo inatoka viwanda vya uchenjuaji

Soma - https://jamii.app/UtoroshajiMadiniChunya
KENYA: RAIA WAWILI WA CHINA WAKAMATWA WAKIENDESHA KIWANDA BUBU CHA GONGO

- Kwa mujibu wa Kamanda wa Athi River, Samuel Mkuusi, raia hao wanashikiliwa kwa mahojiano

- Kiwanda bubu kilikuwa kwenye nyumba za kupanga za 'Green Park'

Soma => https://jamii.app/GongoWachinaAthiRiver