JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ABIRIA 47 WANUSURIKA KIFO KWENYE AJALI YA BASI LA BUFFALO NA GARI DOGO

> Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Arusha kwenda Dar wamenusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya Kampuni ya Buffalo kugongana na gari dogo na kupinduka

> Chanzo cha ajali ni dereva Buffallo, kulazimisha 'overtake' mahali pasiporuhusiwa

Soma - https://jamii.app/AjaliBuffaloGari
#JFLeo
MHADHIRI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUOMBA RUSHWA YA NGONO

> Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samsoni Mahimbo (68), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake ili amfaulishe ktk mtihani wa marudio (Supplementary)

Soma - https://jamii.app/MhadhiriRushwaNgono
#JFLeo
OFISI YA TAKWIMU (NBS) YAKANUSHA KUPUNGUA KWA AJIRA SERIKALINI

- Imeeleza kuwa taarifa iliyosambazwa na mitandao hususan 'Jamii Forum' haina ukweli na ipuuzwe

- Aidha, imekiri kuwa ajira Serikali Kuu zimepungua lakini zimeongezeka katika miradi ya maendeleo ya Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/NBSKanushoKupunguaAjira
KAMATI YA SADC YAPITISHA KISWAHILI KUWA LUGHA RASMI YA JUMUIYA

> Kamati ya Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo wamekubaliana na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya 4 ya Jumuiya hiyo na kwa sasa wanasubiri baraka za wakuu wa nchi hizo ili kianze kutumika

Soma - https://jamii.app/KiswahiliRasmiSADC
SOMALIA: AL-SHABAAB WASHAMBULIA KAMBI YA JESHI

> Watu 10 wameuawa kwenye mapigano kufuatia shambulio la Kundi la Kigaidi la Al-Shabaab ndani ya kambi moja ya kijeshi nje kidogo ya mji mkuu, Mogadishu

> Pia, shambulio hilo limewauwa wanamgambo 7 wa Al-Shabaab

Soma - https://jamii.app/MilitaryBaseAttack
#JFLeo
RAIS RAMAPHOSA AWASILI TANZANIA, KUTEMBELEA ENEO LA MAZIMBU KESHO

> Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amewasili nchini kwa ziara ya siku mbili kabla ya kushiriki mkutano wa 39 wa SADC

> Kutembelea eneo la Mazimbu Mkoani Morogoro siku ya Ijumaa ambapo wanajeshi wa Afrika Kusini waliweka kambi wakati wa harakati za kudai uhuru dhidi ya Utawala wa Kibaguzi ‘Apartheid Policy’

Soma - https://jamii.app/RamaphosaZiaraMoro
#JFLeo
UVUNJAJI WA SHERIA WAWAWEKA KITANZINI WAKURUGENZI 40

> Waziri wa Nchi TAMISEMI amewapa siku 14 Wakurugenzi wa Halmashauri zaidi ya 40 kujieleza kwa barua kwanini wasichukuliwe hatua kwa kupeleka asilimia 10 kwa wanawake, vijana na walemavu badala ya asilimia 50 ya mapato yao

Soma - https://jamii.app/UvunjifuSheriaDED
#JFLeo
AJALI RUVU PWANI: BARABARA YA KUTOKA DAR KWENDA MOROGORO IMEFUNGWA

> Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Mlandizi, barabara haipitiki kufuatia ajali hiyo iliyotokea mapema leo. Mtoa taarifa anashauri kuwa wanaosafiri kwa kutumia barabara hiyo ni vyema watumie njia ya Dar- Bagamoyo-Chalinze

#JFLeo
ARUSHA NA DODOMA ZANG'ARA KWENYE UKUSANYAJI MAPATO

> Halmashauri ya Jiji la Arusha imeongoza katika kundi la Halmashauri za majiji kwa kukusanya 105% ya mapato ya ndani huku jiji la Dodoma likikusanya Tsh. bilioni 71.727 kama pato ghafi

Soma - https://jamii.app/UvunjifuSheriaDED
#JFLeo
BARIADI, SIMIYU: BAADA YA MASHINE YA ULTRA SOUND KUIBWA, WATUMISHI WA HOSPITALI WACHANGISHWA

- DC Festo Kiswaga ametoa siku 7 kwa Watumishi wa hospitali ya Bariadi kununua mashine mpya ya Tsh. Milioni 30

- Aagiza atakayegoma afutwe kazi

Soma https://jamii.app/WatumishiHospUltraSound
WATU 9 WAKAMATWA KWA KUHUSIKA NA WIZI WA "ILE HELA TUMA KWENYE NAMBA HII"

> Polisi mkoani Pwani wanawashikilia watu tisa kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya utapeli kwa kutumia simu za mkononi

> Wanadaiwa kukutwa na simu 13 za tochi, simu janja 4 na laini 22 za simu pamoja na orodha ya namba za simu

Soma - https://jamii.app/WeziPesaSimu
DAKTARI FEKI AKAMATWA AKIHUDUMIA WAGONJWA KATIKA ENEO LA KANISA

> Moses Lucas Masoud (34) Mkazi wa Visiga Mkoani Pwani amekamatwa kwa kujifanya Daktari bingwa wa kutibu magonjwa ya binadamu

> Alikuwa akitoa huduma kwa gharama kati ya Tsh. 600,000 hadi Tsh. Milioni 1.2 kulingana na hali ya mteja wake

Soma - https://jamii.app/DktFekiMbaroni
#JFLeo
RWANDA YATUHUMIWA KWA KUPIKA TAKWIMU ZA UCHUMI KWA MANUFAA YA KISIASA

- Jarida la Financial Times limeeleza kuwa upikaji mkubwa wa takwimu ulifanyika 2015 kabla ya kura ya maoni iliyomwongezea muda wa kukaa madarakani Rais Kagame kufanyika

Soma =>https://jamii.app/RwandaGvtEcoStat

#JFLeo
LIGI KUU BARA: VIWANJA 3 VYAFUNGWA

> Bodi ya Ligi imevifunga viwanja vya Mwadui, Manungu na Mabatini kutumika msimu huu wa Ligi Kuu Bara hadi vitakapofanyiwa marekebisho

> Ni baada ya kubainika vina uzio ambao ni hatari kwa wanasoka wenyewe

Soma - https://jamii.app/LigiViwanjaVyafungwa
#JFLeo
CANADA: WAZIRI MKUU AKUTWA NA HATIA YA KUINGILIA UCHUNGUZI WA RUSHWA

> Kamati ya Bunge inayoshughulikia maadili imemkuta na hatia Justin Trudeau ya kuingilia uchunguzi juu ya kampuni kubwa ya ujenzi ya SNC-Lavalin

> Kampuni hiyo inatuhumiwa kutoa hongo ya takribani milioni 50 kati ya 2001 na 2011 kwa familia ya Muammar Gaddafi ili kushinda zabuni za ujenzi

Soma - https://jamii.app/TrudeauEthicsViolation
#JFLeo
FAHAMU UGONJWA WA KIHARUSI NA JINSI YA KUKABILIANA NAO

> Kiharusi ni ugonjwa unaotokea pale ubongo unapokosa hewa ya Oksijeni kutokana na mishipa ya damu kupasuka ama kusinyaa

> Dalili za awali ni; Maumivu makali ya kichwa, kupata shida ya kuona, mdomo kwenda upande, kukosa nguvu ya mkono au mguu upande mmoja na kupoteza fahamu

Kufahamu zaidi tembelea - https://jamii.app/DaliliMadharaKiharusi
#JFAfya
KARDINALI PENGO ANG'ATUKA, ASKOFU MKUU RUWA'ICHI ASHIKA USUKANI KULIONGOZA JIMBO KUU DAR

- Papa Francis aridhia ombi la Kardinali Polycarp Pengo, kung’atuka na kumteua Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa’ichiwa kuwa ni Askofu Mkuu wa Jimbo hilo

Soma > https://jamii.app/PengoAstaafu
KESI YA KUPINGA TUNDU LISSU KUVULIWA UBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI KUAMULIWA AGOSTI 23, 2019

- Lissu kupitia Mawakili wake ameomba kibali cha kufungua shauri la maombi maalum ili apate amri mbalimbali kuhusiana na uamuzi wa kuvuliwa Ubunge

Soma > https://jamii.app/LissuMahakamaKuu
KIGOMA: MWALIMU KIZIMBANI KWA KUMBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI WAKE

- Ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantole, Jason Rwekaza(42)

- Anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wake wa darasa la 7 mwenye miaka 17

Soma > https://jamii.app/MwlRwekazaKizimbani