JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Mkurugenzi wa Klabu ya Barcelona, Eric Abidal amesafiri kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Klabu ya Paris Saint-Germain ili kumrudisha Camp Nou Mbrazil, Neymar

> Mchezaji huyo aliondoka Barcelona kwenda PSG kwa usajili uliyoweka rekodi wa Euro milioni 200 mwaka 2017

#JFMichezo
KISUTU, DAR: ANAYETUHUMIWA KWA KUMUUA MKEWE NA KISHA KUMTEKETEZA KWA MOTO AWATISHA WANAHABARI

> Mfanyabiashara Khamis Luwonga amesema ataishangaza Mahakama endapo Waandishi wa Habari wataendelea na utaratibu wao wa kumpiga picha

Zaidi, soma => https://jamii.app/MtuhumiwaVsWanahabari
PROF. KABUDI AWA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAWAZIRI SADC, ASISITIZA KASI YA SOKO HURU

> Profesa Palamagamba Kabudi amesema juhudi za haraka zinahitajika kuongeza kasi ya utekelezaji wa itifaki ya biashara na soko huru la Jumuiya hiyo

> Amekabidhiwa uenyekiti huo na mtangulizi wake, Netumbo Nandi-Ndaitwah ambaye ni Waziri wa mambo ya nje wa Namibia

Soma - https://jamii.app/KabudiMKitiSADC
ZAMBIA: WATU 30 WALIOKUWA WAKIANDAMANA NA KUFANYA FUJO WAKAMATWA NA KUSHIKILIWA NA POLISI

- Ghasia zilizuka baada ya Askari wa Polisi kumnusuru Mwanamke waliyekuwa wakimpiga baada ya kumkamata kwa tuhuma za ushirikina

Zaidi, soma => https://jamii.app/GhasiaChamboli
DORIA YA ULINZI KWA MKUTANO WA SADC KUANZA KESHO, PIKIPIKI KUENDELEA KUKAMATWA

> Polisi Kanda Maalum Dar imesema kuanzia kesho itaimarisha ulinzi kwa kutumia vikosi vyote vya doria ikiwemo Mbwa, Farasi na helikopta ili kuhakikisha mkutano wa 39 Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), unamalizika salama

> Pia wanaendelea kukamata pikipiki zote na magari yanayovunja sheria na katazo la kuingia mjini ambapo jumla ya magari na pikipiki 126 zimeshakamatwa

Soma - https://jamii.app/DoriaUlinziSADC
TANZANIA YAPANGA MIKAKATI ILI LUGHA YA KISWAHILI ITUMIKE SADC

> Waziri Profesa Palamagamba Kabudi amesema katika Mkutano wa 39 na kwenye mwaka mmoja ujao, Tanzania itafanya jitihada kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

> SADC pia itaendeleza harakati za kuitaka Jumuiya ya kimataifa ishinikize Zimbabwe iondolewe vikwazo vya kiuchumi

Soma - https://jamii.app/UseSwahiliSADC
SIMIYU: MASHINE YA 'ULTRA SOUND' YAIBWA KATIKA HOSPITALI YA SOMANDA, BARIADI

> Mashine hiyo pamoja printer vimeibwa katika mazingira ya kutatanisha kwenye Wodi ya wajawazito

> Watu 17 wakiwemo wauguzi wanashikiliwa kwa mahojiano

Zaidi, soma => https://jamii.app/UltraSound-Somanda

#JFLeo
MAREKANI YAIHIMIZA UINGEREZA IJITOE UMOJA WA ULAYA BILA YA MAKUBALIANO

- Mshauri wa masuala ya usalama wa Rais Trump, John Bolton amesema wataiunga mkono

- Asema wanategemea kuiona ikijitenga na Umoja huo kikamilifu ifikapo Oktoba 31, 2019

Soma https://jamii.app/Marekani-UingerezaBrexit
#JFLeo
KENYA: DIWANI AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA DAWA ZA KULEVYA

> Jeshi la Polisi nchini Kenya linamshikilia Diwani Ahmed Salama kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya Dawa za kulevya

> Msako dhidi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya umeanza siku ya Jumapili na jumla ya watu 18 wameshakamatwa

Soma - https://jamii.app/MpArrestedDrugsKE
#JFLeo
SHAURI LA LISSU MAHAKAMA KUU KUSIKILIZWA AGOSTI 15, 2019

> Shauri hilo la maombi lililofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ni la kuiomba Mahakama itoe amri ya kumtaka Spika Ndugai ampe taarifa Lissu ya kumvua ubunge aliyoitangaza Juni 28 na kisha itengue na kutupilia mbali uamuzi huo

Soma - https://jamii.app/KesiLissuVsNdugai
MICHEZO: Kocha Mkuu wa Klabu ya Chelsea, Frank Lampard amethibitisha kuwa kiungo wake N'Golo Kanté atakosekana kwenye mchezo wa leo wa UEFA Super Cup dhidi ya Liverpool utakaochezwa saa 4 usiku
-
Aidha, Lampard amesema atandelea kuwatumia zaidi wachezaji chipukizi ambao ni Mason Mount na Tammy Abraham kwenye kikosi chake

#JFMichezo
AFRIKA KUSINI: MEYA WA MJI WA DURBAN AFUKUZWA NA CHAMA CHAKE

> Chama cha ANC kimeamua kumfukuza Zandile Gumede ambaye yuko chini ya uchunguzi wa utakatishaji fedha na rushwa katika kesi ya udanganyifu wakati wa kupata mkataba wa zabuni

> Kashfa hiyo inamhusu yeye na madiwani 62 kutoka Mkoa wa KwaZulu-Natal

Soma - https://jamii.app/DurbanMayorKickedOut
KENYA: MFANYAKAZI SAFARICOM KIZIMBANI KWA KUIBA FEDHA ZA MAREHEMU

- Peter Odhiambo Ochieng amefikishwa Mahakamani akidaiwa kuiba namba ya simu ya mteja aliyefariki

- Anadaiwa pia kuiba Ksh. 45,600 zilizokuwa kwenye akaunti ya namba hiyo

Soma https://jamii.app/MtumishiSafaricomKizimbaniWizi
UPDATE: Majeruhi 6 wa ajali ya moto iliyotokea Mkoani Morogoro waliokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefariki na kufanya idadi ya waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo kufikia 82

> Majeruhi wengine 32 bado wanaendelea na matibabu hospitalini hapo
TANGA: MWILI WA MFANYAKAZI WA NMB WAOPOLEWA BAHARINI

> Patrick Kilungulia (53) ni mmoja wa wafanyakazi 11 wa Benki ya NMB, waliokuwa ndani ya boti ambayo waliikodisha kwa ajili ya kufanya utalii

> Boti hiyo ilipinduka Jumapili jioni

Zaidi, soma - https://jamii.app/MwiliMfanyakaziNMB
#JFLeo
DAR: MOTO WATEKETEZA NYUMBA MAENEO YA TABATA, JESHI LA ZIMA MOTO LAFIKA NA KUUZIMA

> Wananchi wa eneo la TOT-Tabata kwa kushirikiana na Askari wa Kikosi cha Zimamoto wameuzima moto ulioiteketeza nyumba hiyo iliyopo mita chache kutoka kituo cha mafuta cha Mount Meru

Zaidi, soma => https://jamii.app/MotoTabataToT
UNAVIJUA VYAKULA HATARI KWA AFYA YA NGOZI?

> Mdau kutoka JamiiForums anasema kuna baadhi ya vyakula huharibu ngozi vikitumika sana

> Mojawapo ya vyakula hivi ni nyama nyekundu ambayo ina kemikali aina ya Carnitine ambayo inafanya mishipa ya damu kukakamaa na kusababisha kuzeeka kwa ngozi

> Sukari pia hudhoofisha mfumo wa kinga za mwili. Kiasi kingi cha sukari mwilini hufanya ngozi kuwa kavu na kutengeneza makunyazi

Kufahamu zaidi, soma - https://jamii.app/VyakulaMadharaNgozi
#JFAfya
KENYA: MWILI WA MAREHEMU WAFUKULIWA NA KUVULIWA NGUO

- Uongozi wa Kaunti ya Kakamega waamuru mwili wa Martin Alikoye aliyekuwa askari wa kikosi cha ulinzi cha vijana wa kaunti hiyo ufukuliwe na kuvuliwa sare za kazi alizozikwa nazo

Zaidi, soma => https://jamii.app/MwiliWafukuliwa-KE
DAR: RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA KIFO KWA CHRISTOPHER BAGENI

> Rufaa iliyokatwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kinondoni, Christopher Bageni imetupiliwa mbali

> Alikutwa na hatia ya mauaji ya Wafanyabiashara 3 wa madini kutoka Morogoro(2006)

Soma > https://jamii.app/RufaniBageni