JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
COSAFA: TIMU YA WANAWAKE YA TANZANIA U20 YAIBUKA KIDEDEA

- Timu hiyo imefanikiwa kuchukua ubingwa baada ya kuifunga Zambia goli 2-1 kwenye mchezo wa fainali

- Imekuwa timu ya kwanza kuchukua ubingwa wa COSAFA ikiwa kama Taifa alikwa

Soma https://jamii.app/COSAFATzU20Bingwa
#JFLeo
KIGOMA: DIWANI WA KATA YA GWARAMA ADAIWA KUKAMATWA NA JESHI LA POLISI

- Taarifa zinadai Diwani Elia F. Michael amekamatwa akiwa katika eneo la wazi kwenye Kata yake

- Imeelezwa alikuwa amepanga kuzungumza na Wananchi

Soma => https://jamii.app/DiwaniGwarama-Akamatwa
TANGA: WATU KUMI WANUSURIKA KIFO BAADA YA BOTI KUPINDUKA

> Boti inayomilikiwa na mtu binafsi jijini Tanga, imepinduka baharini jana jioni ikiwa na watu 11, huku wengi wakiwa ni wafanyakazi wa NMB Korogwe

> Kati yao, 10 wameokolewa na mmoja bado hajapatikana

Soma - https://jamii.app/AjaliBotiKupinduka
INDIA: WATU 154 WAFARIKI KUTOKANA NA MAFURIKO

> Idadi ya vifo vinavyotokana na mafuriko yaliyoambatana na dhoruba kali nchini India imefikia watu 154 huku zaidi ya watu milioni moja wakihamishiwa katika kambi za muda

> Vifo vingi vimeripotiwa katika Wilaya za Kerala, Wayanad na Malappuram

Soma - https://jamii.app/VifoMafurikoIndia
RUVUMA: LORI YA KAMPUNI YA NJOMBE FILLING STATION LATEKETEA KWA MOTO

> Lori hilo limeteketea kwa moto baada ya kupata ajali katika Kijiji cha Ngadinda, Madaba Wilayani Songea

> Aidha, dereva wa Lori hilo mpaka sasa hajulikani alipo

Soma > https://jamii.app/LoriMoto-Songea

#JFLeo
GUATEMALA: ALEJANDRO GIAMMATTEI ASHINDA UCHAGUZI WA URAIS

> Mgombea wa uchaguzi kutoka chama cha mrengo wa kulia cha Vamos nchini Guatemala ameshinda uchaguzi wa urais uliofanyika jana, Agosti 11

> Alejandro ameshinda kwa 58% ya kura, dhidi ya Sandra Torres ambaye amepata 42% ya kura huku hii ikiwa ni mara ya nne mfululizo kwa Alejandro kuwania kinyang'anyiro hicho

Soma - https://jamii.app/GuatemalaPresidElection
UPDATE: Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili umetoa taarifa ya kufariki kwa majeruhi 4 kati ya 43 wa ajali ya moto iliyotokea Agosti 10 eneo la Msamvu Itigi, Morogoro

> Vifo hivyo vinafanya mpaka sasa jumla ya idadi ya waliofariki kutokana na ajali hiyo kufikia 76

#JFLeo
WAZIRI AITAKA NEMC KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA CHUMA CHAKAVU NJE YA NCHI

> Waziri George Simbachawene amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kudhibiti usafirishwaji wa chuma chakavu maeneo yote yenye mipaka

>Aidha, Waziri ametoa muda kwa mamlaka husika kutoa maelezo ya makontena 18 ya chuma chakavu yaliyosafirishwa nje ya nchi licha ya kuwepo kwa zuio la kusafirishwa

Soma - https://jamii.app/UdhibitiChumaChakavu
MAANDAMANO HONG KONG: SAFARI ZA NDEGE ZASITISHWA

> Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong, China umesitisha safari zote nchini humo kutokana na maandamano yanayoendelea

> Sitisho hilo lililotangazwa leo, litazihusisha ndege zote zinazoingia na kutoka katika mji huo baada ya waandamanaji kupiga kambi katika uwanja huo kwa siku 4 sasa

Soma - https://jamii.app/HongKongFlightCancel
TAKWIMU: KIWANGO CHA AJIRA SEKTA BINAFSI NA SERIKALINI CHAPUNGUA

> Ripoti hiyo iliyopewa jina la “Tanzania in Figures 2018 inaeleza ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018

> Ajira zilizotengenezwa na Serikali zilipungua kutoka 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na anguko la asilimia 78.1 katika kipindi hicho

Soma - https://jamii.app/TakwimuAngukoAjira
KENYA: AJUZA WA MIAKA 80 ABAKWA NA KUUAWA

> Jedidah Wanjiru mkazi wa Kijiji cha Kanyange, Kata ya Kirinyaga amekutwa akiwa amefariki huku amewekwa vipande vya nguo ndani ya mdomo wake

> Shingo yake yakutwa na alama za michubuko

Zaidi, soma => https://jamii.app/AjuzaAbakwa-KE
MICHEZO: Mchezo wa Ngao wa Jamii kati ya Simba na Azam sasa utafanyika Jumamosi ktk Uwanja wa Taifa jijini Dar kuanzia saa 1 usiku

> Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika Uwanja wa Samora Iringa lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko ya uwanja

#JFMichezo
RAIS RAMAPHOSA KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI TANZANIA

> Rais huyo wa Afrika Kusini, anatarajiwa kuwasili Nchini kesho Agosti 14 kwa Mwaliko wa Ziara ya kitaifa na atapokelewa na Mwenyeji wake, Rais John Magufuli

> Baada ya kumaliza ziara yake atakuwepo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

Soma - https://jamii.app/RamaphosaVisitsTZ
#JFLeo
MUFTI TANZANIA: BAKWATA HAITAVUMILIA KUNYANYASWA NA KUVUNJIWA HESHIMA

> Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakary Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu halitaacha Uislamu uchezewe na amewaomba Mashehe, Maimamu na Maustaadhi waheshimu mamlaka na wawe watiifu kwa viongozi

> Ameomba Serikali ielewe kwamba, kwenye masuala ya Waislamu nchini wa kusikilizwa ni BAKWATA

Soma - https://jamii.app/MuftiDharauBaraza
UN: VYAKULA VYA MIMEA NI MUHIMU KATIKA KUPAMBANA NA JOTO DUNIANI

> Ripoti ya wataalamu wa tabia ya nchi wa Umoja wa Mataifa wameeleza kubadili aina ya chakula kutoka nyama na kuingia kwenye vyakula vitokanavyo na mimea kunasaidia kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi

> Ripoti imesema matumizi makubwa ya nyama na maziwa katika nchi za Magharibi yanachochea ongezeko la joto duniani

Soma - https://jamii.app/NyamaOngezekoJoto
KAMBI RASMI YA UPINZANI KUPINGA ONGEZEKO LA ASILIMIA 6 KWA WANUFAIKA WA MIKOPO ELIMU YA JUU

> Kambi ya Upinzani Bungeni pia imepanga kupinga makato ya 1% yanayokatwa na HESLB dhidi ya wanufaika wa mikopo hiyo kama ada ya uendeshaji

Zaidi, soma => https://jamii.app/Upinzani-HESLB
ACACIA YARUHUSIWA KUENDELEA KUSAFIRISHA DHAHABU

> Kampuni ya Acacia imeruhusiwa kuendelea na utaratibu wa kusafirisha dhahabu baada ya kuzuiliwa kwa takribani mwezi mmoja na Tume ya Madini Tanzania

> Hata hivyo, Tume ya Madini imesema inaamini baadhi ya vipengele vya kanuni ya madini ya mwaka 2010 vilikiukwa

Soma - https://jamii.app/AcaciaResumeExports
MICHEZO: Kiungo Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Wesley Sneidjer (35) ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka baada ya miaka 17 ya uchezaji

> Aliwahi kushinda medali ya mshindi wa pili wa Kombe la Dunia akiwa na timu ya Taifa huko Afrika Kusini mwaka 2010

#JFMichezo
TANZIA: Ange Di Huon maarufu kama DJ Arafat, msanii maarufu kutoka Ivory Coast amefariki baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki

> Wimbo wa mwisho alioutoa ni ‘Moto moto’ ambao hadi sasa umetazamwa zaidi ya mara milioni 4.4 kwenye YouTube ndani ya miezi mitatu

Soma - https://jamii.app/DjArafatDead
#JFLeo
KAPSERET, KENYA: MWANAUME AFARIKI WAKATI AKIFANYA MAPENZI NDANI YA SHAMBA LA MAHINDI

- Julius Bor(35) amefariki dunia katika shamba la mahindi lililopo Kaunti ya Uasin Gishu baada ya kuanguka wakati akifanya mapenzi na Janet Cheruto(40)

Soma > https://jamii.app/AfarikiShambaniKE