JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: MWANAHABARI BOLLEN NGETTI ADAIWA KUKAMATWA

- Inadaiwa Mwandishi huyo anayeandika habari za Kiuchunguzi amekamatwa jana, Agosti 8 na kupelekwa kituo cha Polisi Stakishari

- Sababu za kukamatwa kwa Mwandishi huyo bado hazijafahamika

Zaidi, soma https://jamii.app/BollenNgetiMbaroni
RASMI: DAVID LUIZ ASAJILIWA ARSENAL AKITOKEA CHELSEA

- David Luiz (32) amesajiliwa kwa ada ya Paundi Milioni 8 na amesaini kandarasi ya miaka miwili

- Arsenal ilikuwa na shauku ya kusajili beki wa kati ili kuziba pengo la Laurent Koscielny aliyetimkia Bordeaux
KENYA: AMUUA MUME WAKE AKIMSHUTUMU KUMUIBIA KSH. 1,000

- Polisi katika Kaunti ya Bungoma imemkamata Mwanamke huyo anayedai mumewe alimuibia fedha hizo na kugoma kurudisha

- Inadaiwa alimpiga na kitu kizito kichwani na kumkata mguuni kwa panga

Zaidi, soma https://jamii.app/WomanKillsHusband-Bungoma
MAREKANI, UINGEREZA WAUNGANA KUKEMEA KINACHOENDELEA NCHINI

> Mabalozi wa nchi hizo hapa nchini wasikitishwa na kinachoendelea nchini na mfumo wa utoaji haki

> Waisihi Serikali kuhakikisha utoaji haki kwa Raia kwa mujibu wa Mikataba ya Kimataifa

Zaidi, soma https://jamii.app/USA-UingerezaVsHakiTanzania
MWANZA: PIKIPIKI YASABABISHA BASI LA ABOOD KUPATA AJALI

- Basi la Abood linalofanya safari zake kati ya Dar na Mwanza limepata ajali leo asubuhi maeneo ya Mkolani

- Inadaiwa chanzo cha ajali ni mwendesha pikipiki kuingia barabarani ghafla

Zaidi, soma https://jamii.app/AboodBodabodaZapataAjali-MWZ
MCHUNGUZI MWANDAMIZI WA TAKUKURU KIZIMBANI

- Cosmas Revelian Batanyita amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar

- Anakabiliwa na mashtaka 7 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuomba rushwa ya Tsh. Milioni 200

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaTAKUKURUKizimbaniRushwa
TANZANIA YANG’ARA AFRIKA KATIKA MAPAMBANO YA RUSHWA

- Taasisi ya ‘Global Corruption Barrometter Africa 2019’, imesema Tanzania imekuwa ya kwanza kati ya nchi 35 za Afrika katika ‘Juhudi za Serikali Katika Mapambano dhidi ya Rushwa Mwaka 2019’

Zaidi, soma https://jamii.app/TZYaongozaMapambanoRushwa
HOUSTON, MAREKANI: WATANZANIA 9 WAHUKUMIWA KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

- Jumla ya Watu 11 kutoka Nchi za Tanzania, Pakistani na Iran wamehukumiwa kifungo kwa kushiriki katika kusafirisha #DawaZaKulevya aina ya heroin nchini humo

Zaidi, soma https://jamii.app/WatanzaniaKifungoMarekani
MOROGORO: LORI LATEKETEA KWA MOTO, WATU 100 WASADIKIKA KUUNGUA KATIKA MOTO HUO

> Ajali imetokea eneo la Mzambarauni (Nje kidogo ya Mji wa Morogoro)

> Yadaiwa waendesha Bodaboda waliojaribu kuchota mafuta wameteketea ktk moto huo

Zaidi, soma => https://jamii.app/LoriMoto-Moro
AJALI, MOROGORO: WALIOFARIKI WAFIKIA 62 NA MAJERUHI 68

- Katika waliofariki, Wanaume ni 58, Wanawake ni 3 na mtoto mmoja

- Majeruhi wa Kiume ni 58 huku majeruhi wa Kike ni 10 akiwemo Mtoto mmoja

- Majeruhi 39 wamekimbizwa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar
MANCHESTER CITY YAANZA KUTETEA UBINGWA KWA KISHINDO

- Klabu ya Manchester City chini ya Kocha Pep Guardiola imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-0 dhidi ya West Ham United

- Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu hizo katika msimu huu mpya wa Ligi Kuu England 2019/20