JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAXENCE MELO AANZA KUJITETEA KWENYE MOJA YA KESI ZINAZOMKABILI

- Maxence na Micke William wanatuhumiwa kutotoa ushirikiano kwa Polisi

- Asema Katiba ya nchi inalinda faragha na sheria za Kimataifa za mitandao zinataka Wamiliki kuwa na Sera ya faragha

Zaidi, soma https://jamii.app/KesiMaxenceAjitetea
KIJANA ALIYECHUKUA GARI LA MKUU WA MKOA NA KUPATA AJALI, AFARIKI

- Kasobi Shida (26), mtoto wa dereva wa RC wa Mara, aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Mkoa huo baada ya kupata ajali wakati akiendesha gari la RC Adam Malima, amefariki

Zaidi, soma https://jamii.app/MtotoDerevaRCAfariki
MAREKANI: SERIKALI YATANGAZA KUZISHIKILIA MALI ZA NCHI YA VENEZUELA NA KUSITISHA MAHUSIANO YA KIBIASHARA

> Venezuela inakuwa nchi ya 5 kuwekewa vikwazo vya biashara na Marekani baada ya mataifa ya Cuba, Syria, Iran na Korea Kaskazini

Zaidi, soma =>https://jamii.app/US-MaliVenezuela
DAR: KIJANA WA MIAKA 23 AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 17

> Kijana Musa Jumanne (23) amesomewa hukumu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kumuweka kinyumba na kumbaka binti mmoja Julai Mosi, 2018 hadi Julai 21, 2018

Zaidi, soma >https://jamii.app/KijanaJelaKubaka
JE, KIFUNGUA KINYWA CHAKO HUWA KINAJUMUISHA NINI?

- Mdau kutoka JamiiForums anadai anza kunywa uji wa dona au mtama au ngano ambayo haikukobolewa sana kisha kula chakula cha wanga kama magimbi, viazi au muhogo

- Anadai achana na maandazi, chapati au vitumbua vilivyojaa mafuta kwani sio vyakula asilia vyenye mlomakapi (fibre)

Kujadili, tembelea https://jamii.app/KifunguaKinywaBora
WAKAMATWA KWA KOSA LA KUCHANGANYA JUISI YA TENDE NA VIAGRA

> Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar, imewakamata watu wawili kwa tuhuma za kuuza juisi ya tende iliyochanganywa na dawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa jina la ‘4G’ – viagra

> Juisi hiyo ya tende inadaiwa kuchanganywa na viagra pamoja na mchanganyiko wa dawa nyingine mbalimbali

Soma - https://jamii.app/TuhumaViagraTende
NDEGE YAANGUKA, ABIRIA WAJERUHIWA NA BAADHI HAWAJULIKANI WALIPO

- Inadaiwa watu 5 wamejeruhiwa na watatu hawajulikani walipo, baada ya ndege ndogo kuanguka na kuwaka moto kisiwani Mafia

- Ilikuwa ikielekea Dar ikitokea Zanzibar kupitia Mafia

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeYaangukaMafia
AKAMATWA NA STIKA FEKI ZAIDI YA 2,000 ZA VISA

> Idara ya Uhamiaji nchini, imemkamata Jasmin Ngongolo, mkazi wa Dar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na stika za Visa 2,546 za Tanzania za kughushi wakati akitokea Afrika Kusini

> Mtuhumiwa alifunga mizigo ikiwa na utambulisho juu ya kila boksi kuwa ni stika zinazobandikwa katika vioo vya magari

Soma - https://jamii.app/KughushiStikaVisa
MUIGIZAJI ALIYEJITAMBULISHA KAMA YESU AFARIKI

> Michael Job amefariki akiwa katika Hospitali ya Heyn, Marekani ambako alikuwa akipatiwa matibabu kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu

> Siku chache zilizopita Michael alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya na kudanganya watu kuwa yeye ni Yesu amerudi kama alivyoahidi

Soma - https://jamii.app/YesuFekiAfariki
MWENDELEZO: Mganga Mkuu kisiwani Mafia, Zuberi Ally Nzige amethibitisha kupokea majeruhi saba baada ya ndege kuanguka na kuwaka moto katika uwanja wa Ndege wa Mafia

- Amesema katika hao majeruhi saba, mmoja alikuwa ni muokoaji sio abiria na katika hao abiria sita Mwanamke ni moja. Wote wanaendelea vizuri, hakuna aliyepoteza fahamu bali wana maumivu madogo madogo
KOREA KASKAZINI YAANZA TENA MAJARIBIO YA MAKOMBORA

- Imefyatua makombora mawili ambayo hayajaeleweka aina yake kwenda kwenye bahari ya Japan huku Waziri wa Mambo ya Nje akiponda mazoezi ya pamoja yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini

Zaidi, soma https://jamii.app/NKoreaFires2Missiles
MTOTO ALIWA NA SIMBA AKIWA AMELALA NA MAMA YAKE

> Kangwa Manuga (6) alinyakuliwa na Simba, wakati akiwa amelala na mama yake katika Kijiji cha Sitalike Wilayani Mpanda

> Walikuwa wamelala kwenye nyumba ambayo haikuwa na mlango imara na udhaifu huo wa mlango ulichangia mnyama huyo kuingia ndani kirahisi

Soma - https://jamii.app/MtotoKuliwaSimba
MAONI YA WATAALAMU KUHUSU KUPELEKA WATOTO CHINI YA MIAKA 10 SHULE YA BWENI

> Kuanzia umri wa miaka 2 hadi 4, mtoto huwa na ufahamu usiyojitosheleza katika kujua mabaya na mema. Ni muhimu mzazi kutoa muongozo na uangalizi kwa mtoto

> Mtoto wa miaka 5 hadi 6 anaweza kufuata maelekezo ya mzazi vyema zaidi na huamini kila anachosema mzazi wake

> Mtoto wa miaka 7 mpaka 8, mfumo binafsi wa kung’amua jema na baya unaimarika. Anaanza kujua mifumo ya maisha ya jamii husika na kuelewa madhara ya kutenda mabaya

> Katika miaka 9 na kuendelea, mtoto anaanza kuelewa maumivu ya kutenda kosa na faraja ya kutenda mema. Kwahiyo ni vyema mzazi/mlezi kuwa mfano mwema kwa mtoto

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/BweniMtotoChini10
#JFMalezi
KENYA: WATUHUMIWA 3 WAKAMATWA WAKIDAIWA KUSHAMBULIA WATU HOVYO BARABARANI

- Watuhumiwa hao na wengine wanaoendelea kutafutwa na Polisi walijeruhi wapita njia kwa mapanga jana usiku huko Bamburi

- Watu 13 wamejuruhiwa huku 4 wakiwa mahututi

Zaidi, soma https://jamii.app/ArrestedOverBamburiGangAttack
UGANDA: BOBI WINE ASHTAKIWA AKIDAIWA KUWA NA NIA YA KUMKERA RAIS MUSEVENI

- Ameshtakiwa akidaiwa kuwa na nia ya kumkera, kumshtua au kumkejeli Rais Museveni

- Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki tayari anakabiliwa na shtaka jingine la uhaini

Zaidi, soma https://jamii.app/BobiWineAshtakiwaKumkeraMuseveni
KOREA KASKAZINI YADAI MAREKANI INACHOCHEA MIVUTANO YA KIJESHI. YADHAMIRIA KUJIHAMI

- Imedai hivyo kutokana na Marekani kufanya mazoezi ya Kijeshi na Korea Kusini

- Marekani yasema imedhamiria kuondoa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini

Zaidi, soma https://jamii.app/NKoreaUchocheziMarekani
SHAMBULIO DR CONGO: WATU 2 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 24 HAWAJULIKANI WALIPO

> Watu hao wamefariki baada ya kutokea kwa shambulio katika eneo la Mashariki la Nchi hiyo. Shambulio hilo limetekelezwa na kikundi cha Waasi cha ADF

Zaidi, soma => https://jamii.app/ADFEsternDRC
KENYA: WATU WANNE WAFARIKI KWENYE AJALI WAKITOKA MSIBANI

> Watu 4 wamepoteza maisha na 2 kujeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyotokea jana, katika eneo la Ithe Ruui kwenye Barabara ya Kenol-Murang’a

> Dereva alipoteza mwelekeo wa gari na kuyumba nje ya barabara kabla ya kugonga miti na kuingia kwenye bonde

Soma - https://jamii.app/Vifo4AjaliMsibani
KOREA KASKAZINI YADAIWA KUIBA FEDHA KUFADHILI MPANGO WAKE WA SILAHA

- Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja, inadai nchi hiyo imeiba Dola Bilioni 2 kimtandao

- Ililenga benki na ubadilishanaji wa Sarafu ya Kidijitali (Crypto-Currency)

Zaidi, soma https://jamii.app/NKoreaWiziFedha
AJALI: DALADALA YAGONGANA NA LORI, WATU WAJERUHIWA

> Abiria kadhaa wali wamejeruhiwa baada ya Daladala inayofanya safari katiki ya Gongo la Mboto na Ubungo 2000 kugongana na Lori

> Ajali hiyo imetokea katika eneo la Gereza la Ukonga

Soma > https://jamii.app/Ajali-Ukonga