JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KAGERA: WANAKIJIJI WACHOMA SHAMBA LA MWENZAO WAKIDAI ANAMILIKI ARDHI KUBWA

- Wanakijiji wa Kishanda B, Kyerwa wanadaiwa kuvamia shamba la Tryphone Jeremiah na kuchoma moto nyumba yake, kukata migomba na kuua mifugo yake wakiwemo mbuzi

Zaidi, soma https://jamii.app/WenzakeWamchomeaShamba
TETESI ZA SOKA: TOTTENHAM NA JUVENTUS ZAKUBALIANA DAU LA DYBALA

Kwa mujibu wa SkySports, Klabu ya Juventus imekubali kumuuza mchezaji wake, Paulo Dybala kwa ada ya Paundi Milioni 64.4 ila masuala binafsi kati ya Dybala na Klabu ya Tottenham bado hayajaafikiwa
ZANZIBAR: WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUWABAKA NA KUWADHALILISHA WATOTO WA MIAKA 12

> Wanaume wawili wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kubaka na kudhalilisha Watoto wa Kike wenye miaka 12

> Watuhumiwa wote wako nje kwa dhamana ya Mahakama

Soma > https://jamii.app/KesiKubakaZNZ
ALIYETAKA KUTOROKA KWA KUVAA KAMA MWANAYE, AFARIKI

- Mamlaka nchini Brazil zimesema zimekuta Mfungwa, Clauvino da Silva amefariki gerezani akiwa amejinyonga

- Ni siku kadhaa tangu ajaribu kutoroka gerezani hapo akiwa amevaa kama mwanaye wa kike

Zaidi, soma https://jamii.app/InmateDressedDaughterDead
KENYA: MBUNGE ALIYEINGIA NA MTOTO BUNGENI ATOLEWA

- Spika wa muda, amemtoa Bungeni Mbunge Zulekha Hassan aliyekuwa na mtoto wa chini ya miezi 5

- Spika amesema kanuni za Bunge haziruhusu na kumshauri kutumia majengo maalumu ya kunyonyeshea

Zaidi, soma https://jamii.app/MbungeMtotoBungeni-KE
TETESI ZA SOKA: DAVID LUIZ ANATAKA KUJIUNGA NA ARSENAL

- SkySports imedai mchezaji wa Chelsea, David Luiz leo amefanya mazoezi peke yake tofauti na Wachezaji wengine

- Inadaiwa Luiz anataka kujiunga na Arsenal, na ni mmoja kati ya mabeki wa kati wanaofuatiliwa na Arsenal
WATUMISHI 183 WASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI

- Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amewasimamisha kazi watumishi 183 wa Wizara yake kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuingilia mfumo wa kukadiria na kukusanya kodi ya pango la ardhi

Zaidi, soma https://jamii.app/LukuviAsimamishaWatumishi183
TANGA: MBARONI KWA KUBADILI FEDHA ZA KIGENI BILA LESENI

- Wafanyabiashara 12 wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kufanya biashara hiyo bila leseni ya BoT

- Ni baada ya Polisi kufanya msako kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Dola

Zaidi, soma https://jamii.app/WabadiliFedhaWakamatwaTA
TETESI ZA SOKA: DAVID LUIZ AKARIBIA KUTUA ARSENAL AKITOKEA CHELSEA

- SkySports imedai David Luiz anafanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Arsenal

- Imeripoti kuwa beki huyo mwenye miaka 32 atajiunga Arsenal kwa ada ya £8m na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili
MMILIKI WA KITALU CHA LAKE NATRON EAST AKANA KUFUTIWA UMILIKI WA KITALU HICHO

- Kampuni ya Green Mile Safari imesema haijapata taarifa ya aina yoyote kutoka Serikalini

- Imesema inazichukulia taarifa hizo kama mkakati wa kuichafua kampuni hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/KitaluNatronUmiliki
KATAVI: MWILI WA MTOTO ALIYETOWEKA WAKUTWA MAKABURINI UKIWA UMEHARIBIKA

> Mwili wa Mtoto Kelvin Stephano (12), umeokotwa katika makaburi ya Nsemulwa kwa Mkumbo

> Umetambuliwa kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa siku alipotoweka nyumbani

Soma > https://jamii.app/MwiliMtoto-Kaburini
DAR: MWALIMU MBARONI KWA KUOMBA RUSHWA YA LAKI MOJA

- TAKUKURU imemkamata Mwalimu Mkuu wa Shule ya awali na msingi, Real Hope ya Mbagala Majimatitu, Ayubu Mtondo

- Anadaiwa kupokea fedha hizo za mtego ili kusaidia kumrudisha kazini Mtumishi

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuRealHopeMbaroniRushwa
PAKISTAN YASITISHA UHUSIANO NA INDIA

- Imetangaza kumuondosha Mwanadiplomasia wa juu wa India na kusitisha biashara kati yake na India kufuatia mzozo wa eneo la Kashmir

- India na Pakistani, kila moja inadai eneo la Kashmir ni lake

Zaidi, soma https://jamii.app/PakistanYasitishaUhisianoIndia
RASMI: ROMELU LUKAKU AJIUNGA INTER MILAN

- Inter Milan imethibitisha kumsajili Lukaku akitokea Manchester United kwa ada ya Paundi Milioni 73

- Mshambuliaji huyo, raia wa Ubelgiji mwenye miaka 26 alikuwa akitakiwa kwa muda mrefu na Kocha wa sasa wa Inter, Antonio Conte
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
IKULU, DAR: Amiri Jeshi na Rais wa Tanzania, John Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kikosi cha Wanajeshi 238 wanaoendelea na zoezi la usafi wa fukwe Jijini Dar

- Usafi huo ni sehemu ya kuimarisha usafi wa Jiji kuelekea Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za SADC
DAR: MWANAHABARI BOLLEN NGETTI ADAIWA KUKAMATWA

- Inadaiwa Mwandishi huyo anayeandika habari za Kiuchunguzi amekamatwa jana, Agosti 8 na kupelekwa kituo cha Polisi Stakishari

- Sababu za kukamatwa kwa Mwandishi huyo bado hazijafahamika

Zaidi, soma https://jamii.app/BollenNgetiMbaroni
RASMI: DAVID LUIZ ASAJILIWA ARSENAL AKITOKEA CHELSEA

- David Luiz (32) amesajiliwa kwa ada ya Paundi Milioni 8 na amesaini kandarasi ya miaka miwili

- Arsenal ilikuwa na shauku ya kusajili beki wa kati ili kuziba pengo la Laurent Koscielny aliyetimkia Bordeaux
KENYA: AMUUA MUME WAKE AKIMSHUTUMU KUMUIBIA KSH. 1,000

- Polisi katika Kaunti ya Bungoma imemkamata Mwanamke huyo anayedai mumewe alimuibia fedha hizo na kugoma kurudisha

- Inadaiwa alimpiga na kitu kizito kichwani na kumkata mguuni kwa panga

Zaidi, soma https://jamii.app/WomanKillsHusband-Bungoma
MAREKANI, UINGEREZA WAUNGANA KUKEMEA KINACHOENDELEA NCHINI

> Mabalozi wa nchi hizo hapa nchini wasikitishwa na kinachoendelea nchini na mfumo wa utoaji haki

> Waisihi Serikali kuhakikisha utoaji haki kwa Raia kwa mujibu wa Mikataba ya Kimataifa

Zaidi, soma https://jamii.app/USA-UingerezaVsHakiTanzania