JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAOMBI YA DHAMANA YA KABENDERA KUSIKILIZWA AGOSTI 5

- Maombi ya dhamana ya Mwandishi Erick Kabendera kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

- Alikamatwa Julai 29, 2019 na Idara ya Uhamiaji na amekuwa akihojiwa juu ya uraia wake

Zaidi, soma https://jamii.app/MaombiDhamanaKabendera
MADAGASCAR: MWANAFUNZI AJIUA KWA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE NDEGE

> Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge, Alana Cutland (19) amefariki baada ya kujirusha kutoka kwenye ndege umbali wa futi 5,000 angani

> Inadaiwa alilazimisha kufungua mlango wa ndege hiyo kisha kujirusha katika eneo la Anjajavy

Soma - https://jamii.app/MwnfAjiuaNdegeAngani
NICOLAS PEPE ASAJILIWA RASMI, ARSENAL

- Mchezaji huyo raia wa Ivory Coast (24) amesaini kandarasi ya miaka mitano kwa dau la Paundi Milioni 72 akitokea Lille

- Anakuwa mchezaji ghali kusajiliwa Arsenal katika historia ya klabu hiyo
DAR: Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano

- Anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti 05, 2019 kusikiliza shauri lake la kuomba dhamana lililofunguliwa na Mawakili wake
MSIMAMIZI UMEME MITAMBO YA KINYEREZI ASHUSHWA CHEO

- Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kalemani amemshusha cheo Msimamizi huyo wa nguzo kubwa kutokana na kutoridhishwa na taarifa ya hitilafu ya umeme iliyotokea leo asubuhi, Agosti 01

Zaidi, soma https://jamii.app/MsimamiziKinyereziAshushwaCheo
YEMEN: ZAIDI YA WATU 50 WAMEUAWA KWA BOMU KATIKA GWARIDE LA KIJESHI

- Waasi wa Kihouthi jana wameangusha makombora katika gwaride la Kijeshi katika mji wa Aden

- Mashambulizi mengine yaliyokuwa yamepangwa yalilenga Kituo cha Polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/WaasiWauaWanajeshi-YMN
MKURUGENZI HOTELI YA IMPALA ADAIWA KUKAMATWA KWA KUSHINDWA KULIPA WAFANYAKAZI

> Randy Mrema na Msaidizi wake wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Arusha kwa kosa la kuwanyanyasa na kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wapatao 180 katika kipindi cha miezi 3 mfululizo

> Pia, wafanyakazi 2 raia wa Kenya wamekamatwa wakidaiwa kufanya kazi kinyume na taratibu za nchi

Soma - https://jamii.app/MkrgMadeniMishahara
BALOZI WA ZIMBABWE NCHINI AWEKEWA VIKWAZO NA MAREKANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

> Balozi Anselem Sanyatwe anatuhumiwa kuamuru mauaji ya waandamanaji sita waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Zimbabwe mwaka 2018

> Aliwahi kuwa kiongozi mkuu wa kikosi cha ulizi cha Rais Robert Mugabe kipindi akiwa madarakani

Soma - https://jamii.app/USVikwazoBaloziZimb
SERIKALI: WAAJIRI WANAONYIMA LIKIZO ZA UZAZI KUCHUKULIWA HATUA

- Ni Waajiri wote wanaovunja Sheria kwa kukandamiza haki ya kupata likizo ya uzazi kwa Wanawake wanapojifungua

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ni haki ya Mwanamke kuzaa na kupata likizo ya uzazi

Zaidi, soma https://jamii.app/WaajiriLikizoUzazi
SAUDI ARABIA: WANAWAKE WAPEWA UHURU WA KUSAFIRI WENYEWE

- Wanawake katika nchi hiyo sasa wanaweza kusafiri nje ya nchi bila kusindikizwa na Wanaume

- Pia, Mwanamke wa miaka zaidi ya 21 anaweza kuomba ‘Passport’ bila idhini ya mlezi wa kiume

Zaidi, soma https://jamii.app/WanawakeKusafiriSaudiArabia
POLISI: BAADHI YA MIKOA MARUFUKU MABASI KUSAFIRI SAA 24

- Mabasi yanayotoka Dar kuelekea Kagera, Kigoma na Katavi yatalazimika kulala Wilayani Kahama kutokana na sababu za kiusalama

- Aidha, mabasi yanayotoka Kagera, Katavi na Kigoma kwenda Dar yataruhusiwa kutembea saa 24 kwani maeneo kati ya Morogoro na Dar ni salama

Zaidi, soma https://jamii.app/MabasiMarufukuSaa24
AFISA WA TRA MBARONI KWA KUOMBA RUSHWA ILI KUKWEPA KODI

> Elias Yunus (38), anashikiliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, Mkoa wa Ilala kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Tsh. milioni 50 na kupokea Dola 1,000 kwa ahadi ya kumsaidia mfanyabiashara aliyetaka kukwepa kodi na kujaza taarifa za uongo

Soma - https://jamii.app/AfisaTRARushwaKodi
RAIS KENYATTA APOKEA ZAWADI YAKE YA TAUSI

- Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amepokea Tausi wanne alioahidiwa na Rais Magufuli alipozuru Chato

- Wakati anapokea alikuwepo Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu
MWAKYEMBE: VYOMBO VYA HABARI VIONDOE HOFU KATIKA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

> Serikali imewataka wamiliki wa vyombo vya habari kujenga daraja baina yao na Serikali na kuacha kushirikiana na balozi za nje au taasisi za nje katika kujadili maslahi ya nchi

> Imesema hata gazeti likifungiwa au kupewa adhabu, wamiliki wanapaswa kuonana na Waziri husika kwanza kuliko kukimbilia kwa mabalozi au taasisi za nje

Soma - https://jamii.app/MediaUshirikianoSerikali
SKYSPORTS: MAN. UNITED YAFIKIA DAU LA KUMSAJILI MAGUIRE

- Imekubaliana na Leicester City kumsajili beki wake, raia wa England, Harry Maguire kwa dau la £80m

- Maguire atakayekuwa beki ghali zaidi duniani anatarajiwa kufanya vipimo vya afya Man. Utd muda wowote
MECHI YA SUPER CUP KUCHEZESHWA NA REFA MWANAMKE

- Stephanie Frappart (35) ataweka historia kwa kuwa Mwanamke wa kwanza kuchezesha mechi kubwa ya Wanaume uliyo chini ya UEFA

- Mchezo huo unaozikutanisha Chelsea na Liverpool utachezwa Agosti 14, 2019 huko Istanbul, Uturuki
WAFANYAKAZI WATATU WA TIGO KIZIMBANI KWA KUIBA FEDHA ZA WATEJA TIGOPESA

> Wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita likiwemo la kutakatisha fedha Tsh. Milioni 20.3

> Mashtaka mengine ni kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kuingilia mifumo ya kifedha ya Tigopesa bila kibali

Soma - https://jamii.app/WiziFedhaTigopesa
SIKUKUU YA EID KUSHEREHEKEWA AGOSTI 12
-
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kwamba Sikukuu ya Idd El-Adh’haa itakuwa siku ya Jumatatu ya Agosti 12, 2019
-
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Nuhu Mruma, Katibu Mkuu BAKWATA, inaeleza kwamba swala ya Eid itaswaliwa katika Viwanja vya Masjid Kibadeni, Chanika Zogowali Jijini Dar es Salaam na Baraza la Eid litafanyika viwanjani hapo mara baada ya swala ya Eid