JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DR CONGO KUWA NA SERIKALI YA PAMOJA

- Rais wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila wameafikiani juu ya suala hilo

- Baraza la Mawaziri litakuwa na viongozi 42 kutoka mrengo wa Kabila na 23 kutoka mrengo wa Tshisekedi

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliPamojaDRC
DAR: ASKARI FEKI AKAMATWA AKIWA NA VIFAA VYA JESHI

- Daudi Iddy (23) aliyewahi kwenda mafunzo JKT anashikiliwa kwa kujifanya Afisa wa Polisi

- Amekutwa na vifaa mbalimbali vya Jeshi ikiwemo sare ya Polisi, vyeo tofauti, pingu, buti na viatu

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariFekiJKTMbaroni
UTEUZI: MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI TRA

- Rais Magufuli amemteua Dkt. Suleiman Magesa Missango kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA

- Dkt. Missango ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Sera za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Zaidi, soma https://jamii.app/MissangoM-KitiBodiTRA
ALIYEMUUA MKEWE NA KUMCHOMA MOTO, ASOMEWA MASHTAKA YA KUUA KWA KUKUSUDIA

- Mkazi wa Gezaulole, Kigamboni jijini Dar, Hamisi Saidi (38) ‘Meshack’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kumuua mke wake, Naomi Marijani

Zaidi, soma https://jamii.app/AshtakiwaKuuaKukusudia
SUDAN: MAZUNGUMZO KATI YA JESHI NA WAANDAMANAJI YAFUTWA

- Viongozi wa Maandamano wamefuta mazungumzo yaliyopangwa kufanyika jana baada ya Wanafunzi kuuawa

- Wakati huo huo, Mamia ya Wanafunzi wameandamana kupinga mauaji ya wenzao wanne

Zaidi, soma https://jamii.app/WanafunziWauawaSudan
TETESI ZA SOKA: JE, MANCHESTER UNITED KUMSAJILI DYBALA?

- Manchester United inadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na Juventus kuweza kumsajili Mshambuliaji wake, Paulo Dybala(25)

- Inadaiwa Juventus ipo tayari kumuachia Mchezaji huyo raia wa Argentina kwani inamuwania Romelu Lukaku wa United
MAHAKAMA YAAMURU ERICK KABENDERA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

- Wanasheria wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Kisutu kutaka Kabendera afikishwe Mahakamani

- Mahakama imeridhia na kuitaka Polisi kufanya hivyo kesho asubuhi kama watakuwa naye bado

Zaidi, soma https://jamii.app/KabenderaKufikishwaMahakamani
ZANZIBAR: MAALIM SEIF AKAMATWA NA POLISI

- Chama Cha ACT-Wazalendo kimesema Mshauri Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif amekamatwa

- Kimesema Polisi wamevamia na kuvunja kongamano la Miaka 10 ya Maridhiano ya Wazanzibari na kumchukua Seif

Zaidi, soma https://jamii.app/MaalimSeifAkamatwaZNZ
LISSU: MAANDALIZI YA KUFUNGUA KESI JUU YA UBUNGE WANGU YAMEKAMILIKA

- Tundu Lissu amebainisha kuwa yeye na timu yake ya Mawakili wako tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania

- Amesema kesi za Ubunge zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandaliziKupingaUbungeLissu
TARIME: Inadaiwa Watu takribani 9 wamefariki kwenye ajali ya Hiace mchana wa leo, iliyotokea Mlima Nyamwaga Wilayani Tarime na abiria wengine wametoka wakiwa mahututi

> Gari hilo linafanya safari kati ya Tarime na Mugumu wilayani Serengeti.

> Mashuhuda wanadai gari limefeli break na kulikuwa na abiria zaidi ya 20 ndani

Soma https://jamii.app/AjaliMbayaTarime
SERIKALI: MARUFUKU MWALIMU KUINGIA DARASANI NA VIBOKO

- Imepiga marufuku Walimu wanaofundisha kuanzia elimu ya awali hadi darasa la tatu kuingia na viboko darasani

- Imesema vitendo hivyo vinasababisha Wanafunzi kuogopa na kutokuwa wasikivu

Zaidi, soma https://jamii.app/MarufukuVibokoDarasani
KONTENA LILILOTAKIWA KUWA NA MIZIGO ILIYOAHIDIWA NA CHINA KWA KENYA LAKUTWA TUPU

- China iliahidi kulipatia Bunge la Kenya vifaa vya Ofisini kama sehemu ya kuboresha urafiki wao

- Lakini kontena lilipofika Bungeni na kufunguliwa lilikutwa tupu

Zaidi, soma https://jamii.app/KontenaChina-KenyaTupu
WAANDAMANAJI 44 WA HONG KONG WAFIKISHWA MAHAKAMANI

- Waandamanaji hao wanaopigania demokrasia wamefikishwa Mahakamani jana wakishtakiwa kwa kufanya vurugu

- Iwapo watakutwa na hatia wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 10 jela

Zaidi, soma https://jamii.app/WaandamanajiMahakamaniHongKong
DED HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO AENGULIWA

- Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kayombe Lyoba kutokana na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo

- Meneja wa TARURA wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Godfrey Mlowe atakaimu nafasi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/DEDMorogoroAenguliwa-Agt2019
MAREKANI YADAI KUMUUA MTOTO WA OSAMA BIN LADEN

- Imedai kumuua Hamza Bin Laden, lakini haijaweka wazi kuhusu mahala au tarehe ya kifo

- Awali, Marekani iliahidi kutoa Dola Milioni 1 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kujua alipo

Zaidi, soma https://jamii.app/MtotoOsamaAuawa
KIGOMA: BABA LEVO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 5 JELA

- Msanii na Diwani wa Kata ya Mwanga Kakazini (ACT-Wazalendo), Revocatus Kipando 'Baba Levo' amehukumiwa kwenda jela

- Mahakama ya Mwanzo ya Mwandiga imemtia hatiani kwa kosa la kumshambulia Trafiki

Zaidi, soma https://jamii.app/BabaLevoJelaMiezi5