JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KOMBE LA DUNIA 2022: Ratiba ya kufuzu michuano hiyo imetolewa ambapo timu 28 kati ya 54 za Afrika zilizo chini kwenye viwango vya FIFA zitacheza mechi za awali

- Zitachuana Septemba 2 na 10, 2019 na mshindi atajiunga na timu nyingine 26 katika makundi ili kuchuana kufuzu
HOJA: Wahitimu wengi wa elimu ya juu hukosa ajira na huamua kujiajiri katika sekta mbalimbali ambapo wengi hujiajiri katika shughuli ambazo si zile walizosomea vyuoni

- Mdau wa JamiiForums anasema kusoma mpaka Chuo Kikuu kisha kujiajiri ni kupoteza muda, elimu ya kidato cha nne inatosha kupata maarifa ya kujiajiri

Fuatilia mjadala hapa => https://jamii.app/Hoja-Wahitimu
SINGIDA: ALIYEJIFANYA LUTENI WA JESHI LA WANANCHI AKAMATWA

> Amieli Stephano(29) mkazi wa Arusha amekamatwa mkoani humo kwa tuhuma ya kujifanya Ofisa wa JWTZ

> Baada ya kuhojiwa alikiri yeye ni mkulima na hajaajiriwa mahali popote

Zaidi, soma > https://jamii.app/AfisaFeki-JWTZ
BRAZIL: TAKRIBANI WAFUNGWA 52 WAMEFARIKI KATIKA GHASIA GEREZANI

> Taarifa kutoka katika mamlaka za Brazil zinaeleza kuwa wafungwa hao wameuawa katika ghasia hizo zilizozuka katika gereza la Altamira

> Wafungwa 16 wamejeruhiwa

Zaidi, soma > https://jamii.app/VifoAltimaraPrison
MWANAHABARI ERICK KABENDERA ACHUKULIWA NA JESHI LA POLISI

> Askari Polisi walifika nyumbani kwake Mbweni jijini Dar wakiwa wamevalia kiraia

> Waliondoka na Mwanahabari huyo na kwa sasa wanaendelea kumhoji

Soma > https://jamii.app/KabenderaVsPolisiTz
MKURUGENZI SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) ABADILISHWA

- Rais Magufuli amemteua Dkt. Elirehema Joshua Doriye kuchukua nafasi hiyo kuanzia leo Julai 29, 2019

- Dkt. Elirehema anachukua nafasi ya Sam Kamanga ambaye Uteuzi wake umetenguliwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MkurugenziNICAbadilishwa
BABA NA MWANAYE MBARONI KWA KUMHONGA DC WA DODOMA

- TAKUKURU inawashikilia kwa kumhonga DC Patrobas Katambi Tsh. Milioni 1.2 ili asitekeleze majukumu yake

- Walitaka asifuatilie mapungufu katika Baraza la Ardhi kuhusu hukumu ya kesi yao

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniKumhongaDC-DOM
BERNARD MEMBE AKIRI SAUTI ILIYOSAMBAA AKIONGEA NA SIMU NI YAKE

- Amesema sauti ya hivi karibuni ni yake na anajua ilipotoka ila kutokana na miiko yake hatoeleza

- Amezitahadharisha kampuni za simu kuwa wateja wao kudukuliwa kunaweza kuwapatia hasara

Zaidi, soma https://jamii.app/MembeAkiriKudukuliwa
SERENGETI, MARA: AUA NA KUJERUHI BAADA YA KUNYIMWA BIA

- Kijana mmoja (jina halijajulikana) ametuhumiwa kuua mtu mmoja na kujeruhi wawili kwa mishale

- Inadaiwa walinunua kreti ya bia na Mtuhumiwa alipewa chupa 2 alipotaka tena wakamnyima

Zaidi, soma https://jamii.app/AnyimwaBiaAua-Mara
POLISI KUZUNGUMZIA SUALA LA KABENDERA LEO MCHANA

- Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar, Lazaro Mambosasa amesema atatoa taarifa rasmi juu ya Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera ifikapo saa 7:00 mchana

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiKumzungumziaKabendera
NDEGE YA JESHI YA PAKISTAN YAANGUKA NA KUUA RAIA

- Ndege hiyo iliyokuwa katika safari ya mafunzo imeanguka katika eneo la Makazi karibu na mji wa Rawalpindi leo saa 8 usiku

- Wanajeshi watano na raia 13 wamefariki huku Watu wengine 12 wakijeruhiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeJeshiPakistaniYaua
SUDAN: WANAFUNZI WAUAWA KATIKA MAANDAMANO

- Wanafunzi wanne ni miongoni mwa Waandamanaji watano waliouawa kwa kupigwa risasi jana katika mji wa Al-Obeid huko Kordofan ya Kaskazini wakati wa maandamano ya kulalamikia uhaba wa mkate na mafuta

Zaidi, soma https://jamii.app/WanafunziWauawaSudan
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametolea ufafanuzi kukamatwa kwa Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera

- Aidha, ameeleza kuwa Mwandishi huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi kilichopo Posta jijini Dar (Central Police Station) kwa mahojiano
DR CONGO KUWA NA SERIKALI YA PAMOJA

- Rais wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila wameafikiani juu ya suala hilo

- Baraza la Mawaziri litakuwa na viongozi 42 kutoka mrengo wa Kabila na 23 kutoka mrengo wa Tshisekedi

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliPamojaDRC
DAR: ASKARI FEKI AKAMATWA AKIWA NA VIFAA VYA JESHI

- Daudi Iddy (23) aliyewahi kwenda mafunzo JKT anashikiliwa kwa kujifanya Afisa wa Polisi

- Amekutwa na vifaa mbalimbali vya Jeshi ikiwemo sare ya Polisi, vyeo tofauti, pingu, buti na viatu

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariFekiJKTMbaroni
UTEUZI: MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI TRA

- Rais Magufuli amemteua Dkt. Suleiman Magesa Missango kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA

- Dkt. Missango ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Sera za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Zaidi, soma https://jamii.app/MissangoM-KitiBodiTRA
ALIYEMUUA MKEWE NA KUMCHOMA MOTO, ASOMEWA MASHTAKA YA KUUA KWA KUKUSUDIA

- Mkazi wa Gezaulole, Kigamboni jijini Dar, Hamisi Saidi (38) ‘Meshack’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kumuua mke wake, Naomi Marijani

Zaidi, soma https://jamii.app/AshtakiwaKuuaKukusudia