JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SUDAN: MAZUNGUMZO KATI YA JESHI NA WAANDAMANAJI YAFUTWA

- Viongozi wa Maandamano wamefuta mazungumzo yaliyopangwa kufanyika jana baada ya Wanafunzi kuuawa

- Wakati huo huo, Mamia ya Wanafunzi wameandamana kupinga mauaji ya wenzao wanne

Zaidi, soma https://jamii.app/WanafunziWauawaSudan
TETESI ZA SOKA: JE, MANCHESTER UNITED KUMSAJILI DYBALA?

- Manchester United inadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na Juventus kuweza kumsajili Mshambuliaji wake, Paulo Dybala(25)

- Inadaiwa Juventus ipo tayari kumuachia Mchezaji huyo raia wa Argentina kwani inamuwania Romelu Lukaku wa United
MAHAKAMA YAAMURU ERICK KABENDERA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

- Wanasheria wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Kisutu kutaka Kabendera afikishwe Mahakamani

- Mahakama imeridhia na kuitaka Polisi kufanya hivyo kesho asubuhi kama watakuwa naye bado

Zaidi, soma https://jamii.app/KabenderaKufikishwaMahakamani
ZANZIBAR: MAALIM SEIF AKAMATWA NA POLISI

- Chama Cha ACT-Wazalendo kimesema Mshauri Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif amekamatwa

- Kimesema Polisi wamevamia na kuvunja kongamano la Miaka 10 ya Maridhiano ya Wazanzibari na kumchukua Seif

Zaidi, soma https://jamii.app/MaalimSeifAkamatwaZNZ
LISSU: MAANDALIZI YA KUFUNGUA KESI JUU YA UBUNGE WANGU YAMEKAMILIKA

- Tundu Lissu amebainisha kuwa yeye na timu yake ya Mawakili wako tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania

- Amesema kesi za Ubunge zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandaliziKupingaUbungeLissu
TARIME: Inadaiwa Watu takribani 9 wamefariki kwenye ajali ya Hiace mchana wa leo, iliyotokea Mlima Nyamwaga Wilayani Tarime na abiria wengine wametoka wakiwa mahututi

> Gari hilo linafanya safari kati ya Tarime na Mugumu wilayani Serengeti.

> Mashuhuda wanadai gari limefeli break na kulikuwa na abiria zaidi ya 20 ndani

Soma https://jamii.app/AjaliMbayaTarime
SERIKALI: MARUFUKU MWALIMU KUINGIA DARASANI NA VIBOKO

- Imepiga marufuku Walimu wanaofundisha kuanzia elimu ya awali hadi darasa la tatu kuingia na viboko darasani

- Imesema vitendo hivyo vinasababisha Wanafunzi kuogopa na kutokuwa wasikivu

Zaidi, soma https://jamii.app/MarufukuVibokoDarasani
KONTENA LILILOTAKIWA KUWA NA MIZIGO ILIYOAHIDIWA NA CHINA KWA KENYA LAKUTWA TUPU

- China iliahidi kulipatia Bunge la Kenya vifaa vya Ofisini kama sehemu ya kuboresha urafiki wao

- Lakini kontena lilipofika Bungeni na kufunguliwa lilikutwa tupu

Zaidi, soma https://jamii.app/KontenaChina-KenyaTupu
WAANDAMANAJI 44 WA HONG KONG WAFIKISHWA MAHAKAMANI

- Waandamanaji hao wanaopigania demokrasia wamefikishwa Mahakamani jana wakishtakiwa kwa kufanya vurugu

- Iwapo watakutwa na hatia wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 10 jela

Zaidi, soma https://jamii.app/WaandamanajiMahakamaniHongKong
DED HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO AENGULIWA

- Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kayombe Lyoba kutokana na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo

- Meneja wa TARURA wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Godfrey Mlowe atakaimu nafasi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/DEDMorogoroAenguliwa-Agt2019
MAREKANI YADAI KUMUUA MTOTO WA OSAMA BIN LADEN

- Imedai kumuua Hamza Bin Laden, lakini haijaweka wazi kuhusu mahala au tarehe ya kifo

- Awali, Marekani iliahidi kutoa Dola Milioni 1 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kujua alipo

Zaidi, soma https://jamii.app/MtotoOsamaAuawa
KIGOMA: BABA LEVO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 5 JELA

- Msanii na Diwani wa Kata ya Mwanga Kakazini (ACT-Wazalendo), Revocatus Kipando 'Baba Levo' amehukumiwa kwenda jela

- Mahakama ya Mwanzo ya Mwandiga imemtia hatiani kwa kosa la kumshambulia Trafiki

Zaidi, soma https://jamii.app/BabaLevoJelaMiezi5
MAOMBI YA DHAMANA YA KABENDERA KUSIKILIZWA AGOSTI 5

- Maombi ya dhamana ya Mwandishi Erick Kabendera kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

- Alikamatwa Julai 29, 2019 na Idara ya Uhamiaji na amekuwa akihojiwa juu ya uraia wake

Zaidi, soma https://jamii.app/MaombiDhamanaKabendera
MADAGASCAR: MWANAFUNZI AJIUA KWA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE NDEGE

> Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge, Alana Cutland (19) amefariki baada ya kujirusha kutoka kwenye ndege umbali wa futi 5,000 angani

> Inadaiwa alilazimisha kufungua mlango wa ndege hiyo kisha kujirusha katika eneo la Anjajavy

Soma - https://jamii.app/MwnfAjiuaNdegeAngani
NICOLAS PEPE ASAJILIWA RASMI, ARSENAL

- Mchezaji huyo raia wa Ivory Coast (24) amesaini kandarasi ya miaka mitano kwa dau la Paundi Milioni 72 akitokea Lille

- Anakuwa mchezaji ghali kusajiliwa Arsenal katika historia ya klabu hiyo
DAR: Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano

- Anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti 05, 2019 kusikiliza shauri lake la kuomba dhamana lililofunguliwa na Mawakili wake