JamiiForums
52.8K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DR CONGO: WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA MADINI WATEKWA

- Wafanyakazi wa Banro Mining hawajulikani waliko baada ya kutekwa Ijumaa, Julai 26 kwenye mgodi wa Namoya

- Watu waliotambuliwa kama wanamgambo wa Mai Mai Malaika wamehusishwa na utekaji

Zaidi, soma https://jamii.app/WafanyakaziWatekwa-DRC
PAUL MAKONDA: WASIOFUA NGUO, KUNYOOSHA, KUOGA WASIONEKANE MJINI HADI MKUTANO WA SADC UMALIZIKE

> Amesema kwenda mjini bila kunyoosha nguo na kuoga ni marufuku

> Wapo wanaotembea na chawa. Kama huwezi kuwa msafi basi subiri mkutano upite

Soma > https://jamii.app/Makonda-WachafuDa
SONGWE: MFANYABIASHARA ALIYEWAUZIA WAKULIMA MBEGU FEKI ATAKIWA KUKAMATWA

- Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ametoa agizo hilo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo

- Kutokana na kitendo hicho mfanyabiashara huyo anadaiwa kuathiri mavuno

Zaidi, soma https://jamii.app/MuuzajiMbeguFekiKukamatwa
MICHEZO: ROMELU LUKAKU MBIONI KUONDOKA MAN. UNITED?

- Hajatajwa kwenye kikosi cha Wachezaji 26 wa Manchester United wanaoenda Norway katika maandalizi ya msimu ujao

- Inadaiwa Kocha wake, Ole Gunnar Solskjaer amempa siku 4 kukamilisha usajili wake wa kujiunga Inter Milan
HAI: MBOWE ATAKIWA KUSITISHA ZIARA KUTOKANA NA ZIARA ZA DC SABAYA

- Freeman Mbowe ametakiwa kusitisha ziara jimboni kwake kwani DC Ole Sabaya ana ziara Wilayani hapo

- Polisi imedai kuingiliana kwa ziara kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani

Zaidi, soma https://jamii.app/MboweAzuiwaMikutano
MKURUGENZI MSAIDIZI WA MIRADI YA EU NCHINI AKUTWA AMEFARIKI

- Leopold Lwajabe amekutwa amefariki Wilayani Mkuranga baada ya kupotea wiki iliyopita

- Wizara ya Fedha imesema imepata taarifa ya kifo wakati ikijiandaa kutoa taarifa ya kumtafuta

Zaidi, soma https://jamii.app/LeopoldKitengoEUAfariki
KOMBE LA DUNIA 2022: Ratiba ya kufuzu michuano hiyo imetolewa ambapo timu 28 kati ya 54 za Afrika zilizo chini kwenye viwango vya FIFA zitacheza mechi za awali

- Zitachuana Septemba 2 na 10, 2019 na mshindi atajiunga na timu nyingine 26 katika makundi ili kuchuana kufuzu
HOJA: Wahitimu wengi wa elimu ya juu hukosa ajira na huamua kujiajiri katika sekta mbalimbali ambapo wengi hujiajiri katika shughuli ambazo si zile walizosomea vyuoni

- Mdau wa JamiiForums anasema kusoma mpaka Chuo Kikuu kisha kujiajiri ni kupoteza muda, elimu ya kidato cha nne inatosha kupata maarifa ya kujiajiri

Fuatilia mjadala hapa => https://jamii.app/Hoja-Wahitimu
SINGIDA: ALIYEJIFANYA LUTENI WA JESHI LA WANANCHI AKAMATWA

> Amieli Stephano(29) mkazi wa Arusha amekamatwa mkoani humo kwa tuhuma ya kujifanya Ofisa wa JWTZ

> Baada ya kuhojiwa alikiri yeye ni mkulima na hajaajiriwa mahali popote

Zaidi, soma > https://jamii.app/AfisaFeki-JWTZ
BRAZIL: TAKRIBANI WAFUNGWA 52 WAMEFARIKI KATIKA GHASIA GEREZANI

> Taarifa kutoka katika mamlaka za Brazil zinaeleza kuwa wafungwa hao wameuawa katika ghasia hizo zilizozuka katika gereza la Altamira

> Wafungwa 16 wamejeruhiwa

Zaidi, soma > https://jamii.app/VifoAltimaraPrison
MWANAHABARI ERICK KABENDERA ACHUKULIWA NA JESHI LA POLISI

> Askari Polisi walifika nyumbani kwake Mbweni jijini Dar wakiwa wamevalia kiraia

> Waliondoka na Mwanahabari huyo na kwa sasa wanaendelea kumhoji

Soma > https://jamii.app/KabenderaVsPolisiTz
MKURUGENZI SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) ABADILISHWA

- Rais Magufuli amemteua Dkt. Elirehema Joshua Doriye kuchukua nafasi hiyo kuanzia leo Julai 29, 2019

- Dkt. Elirehema anachukua nafasi ya Sam Kamanga ambaye Uteuzi wake umetenguliwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MkurugenziNICAbadilishwa
BABA NA MWANAYE MBARONI KWA KUMHONGA DC WA DODOMA

- TAKUKURU inawashikilia kwa kumhonga DC Patrobas Katambi Tsh. Milioni 1.2 ili asitekeleze majukumu yake

- Walitaka asifuatilie mapungufu katika Baraza la Ardhi kuhusu hukumu ya kesi yao

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniKumhongaDC-DOM
BERNARD MEMBE AKIRI SAUTI ILIYOSAMBAA AKIONGEA NA SIMU NI YAKE

- Amesema sauti ya hivi karibuni ni yake na anajua ilipotoka ila kutokana na miiko yake hatoeleza

- Amezitahadharisha kampuni za simu kuwa wateja wao kudukuliwa kunaweza kuwapatia hasara

Zaidi, soma https://jamii.app/MembeAkiriKudukuliwa
SERENGETI, MARA: AUA NA KUJERUHI BAADA YA KUNYIMWA BIA

- Kijana mmoja (jina halijajulikana) ametuhumiwa kuua mtu mmoja na kujeruhi wawili kwa mishale

- Inadaiwa walinunua kreti ya bia na Mtuhumiwa alipewa chupa 2 alipotaka tena wakamnyima

Zaidi, soma https://jamii.app/AnyimwaBiaAua-Mara
POLISI KUZUNGUMZIA SUALA LA KABENDERA LEO MCHANA

- Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar, Lazaro Mambosasa amesema atatoa taarifa rasmi juu ya Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera ifikapo saa 7:00 mchana

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiKumzungumziaKabendera
NDEGE YA JESHI YA PAKISTAN YAANGUKA NA KUUA RAIA

- Ndege hiyo iliyokuwa katika safari ya mafunzo imeanguka katika eneo la Makazi karibu na mji wa Rawalpindi leo saa 8 usiku

- Wanajeshi watano na raia 13 wamefariki huku Watu wengine 12 wakijeruhiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeJeshiPakistaniYaua
SUDAN: WANAFUNZI WAUAWA KATIKA MAANDAMANO

- Wanafunzi wanne ni miongoni mwa Waandamanaji watano waliouawa kwa kupigwa risasi jana katika mji wa Al-Obeid huko Kordofan ya Kaskazini wakati wa maandamano ya kulalamikia uhaba wa mkate na mafuta

Zaidi, soma https://jamii.app/WanafunziWauawaSudan
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametolea ufafanuzi kukamatwa kwa Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera

- Aidha, ameeleza kuwa Mwandishi huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi kilichopo Posta jijini Dar (Central Police Station) kwa mahojiano