TARIME: FISI AUA MTOTO NA KUJERUHI WATU WATATU
> Fisi anayedhaniwa kuwa na kichaa amemuua mtoto wa miaka mitatu na kujeruhi watu wengine watatu akiwemo baba wa mtoto huyo, Osango Nyawino
> Fisi huyo alivamia mji wa Osango na kumjeruhi mtoto huyo tumboni hali iliyosababisha kifo chake na kisha kwenda kuvamia miji mingine ukiwamo wa Adikus Akwanyo na kujeruhi ng’ombe 2
#JFLeo

UTEUZI: RAIS MAGUFULI AMTEUA EDWARD MPOGOLO KUWA MKUU WA WILAYA YA IKUNGI, SINGIDA
> Anakwenda kuchukua nafasi ya Miraji Mtaturu aliyechaguliwa kuwa Mbunge wa Singida Mashariki
> Kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma
Soma > https://jamii.app/MpogoloDCIkungi

NIGERIA YAINGIA MAKUBALIANO NA SIEMENS KWA AJILI YA KUTATUA TATIZO LA NISHATI YA UMEME
> Serikali ya Nigeria imeingia makubaliano hayo ili kuhakikisha nchi hiyo inapata umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2025
> Miundombinu itakayojengwa na kampuni hiyo itazalisha Megawati 25,000 za umeme ifikapo mwaka 2025
Zaidi, soma => https://jamii.app/NigeriaVsSiemens

WAVUVI 8 WALIOPOTEA BAHARINI: WATATU WAPATIKANA KENYA WAKIWA HAI
> Wavuvi 3 kati ya 8 wa kijiji cha Shumba Wilaya ya Micheweni Pemba, waliokuwa wamepotea kwenye boti 2 wamepatikana wakiwa hai eneo la Watamu nchini Kenya huku mwenzao 1 akihofiwa kufariki
> Ambao hawajaonekana na wala hakuna taarifa zao ni pamoja na Kombo Fakih Mwalimu (55), Mwalimu Bosi Faki (32), Said Ali Omar (50) na Omar Kombo Fakih (25), waliokuwa chombo kimoja
Soma - https://jamii.app/KupoteaBotiUpepo

AHUKUMIWA MIAKA 2 JELA KWA KUMUUA MKE WAKE BILA KUKUSUDIA
> Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Mhandisi Novat Kaberwa baada ya kukiri kumuua Clara Munisi bila kukusudia
> Anadaiwa kumpiga mke wake baada ya kurudi nyumbani usiku na kukuta watoto wameshinda njaa huku marehemu akiwa ameenda kulewa kwa kutumia hela ya matumizi aliyomuachia
Soma - https://jamii.app/JelaKuuaBilaKusudio

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO KWENYE KATA 13 TANZANIA BARA
> Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza uchaguzi mdogo wa Kata 13 ambao utafanyika Agosti 17, 2019 na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya Julai 29 Julai mpaka Agosti 03
> Baadhi ya kata ni pamoja na Laroi, Lemanyata na Likiding’a (Arusha), Kimokouwa (Longido), Kwembe (Ubungo), Izigo (Muleba), Mahida (Rombo)
Soma - https://jamii.app/UchaguziKata13

RAIS MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UMEME RUFIJI
> Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kesho Rais John Magufuli ataweka jiwe la msingi katika Mradi wa kufua umeme wa megawati 2115 wa Rufiji ‘Stiegler's Gorge’ uliopo Mikoa ya Pwani na Morogoro
> Mradi huo utakapokamilika unatarajiwa kutumia kiasi cha Tsh. Trilioni 6.5
Soma - https://jamii.app/MsingiUmemeRufiji

OLE SABAYA KUCHUNGUZWA KUHUSU TUHUMA ZA RUSHWA. MWENYEWE AKANUSHA
> Mkuu wa Wilaya ya Hai anachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutokana na malalamiko yaliyotolewa na Mfanyabiashara wa Kampuni ya Asante Tours, akitumhumu Sabaya kumpa vitisho na kudai fedha kwa nguvu ikiwa ni pamoja na kuwakamata wafanyakazi wake na kuwaweka mahabusu
Soma - https://jamii.app/SabayaTuhumaRushwa

AFYA: Tatizo la mtu mzima kukojoa kitandani limekuwa likileta usumbufu na aibu kubwa katika jamii
- Takwimu zinaonesha kuwa tatizo hili huwakumba zaidi Wanawake na watu wenye umri mkubwa
> Baadhi ya sababu zinazotajwa kusababisha tatizo hili ni umri, uzito uliopitiliza, uvutaji wa sigara na magonjwa ya figo na kisukari
Kwa tiba na jinsi ya kuepuka tatizo hili, bofya => https://jamii.app/WatuWazimaKukojoa

SERIKALI: WATANZANIA NI WAVIVU WA KULA NYAMA
> Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ameeleza kuwa kila Mtanzania anapaswa kula Kg50 za nyama kwa mwaka
> kwa mujibu wa FAO, kwa sasa kila Mtanzania anakula kilo 15 tu kwa mwaka
Zaidi, soma => https://jamii.app/WatanzaniaVsKulaNyama

TANZIA: RAIS WA TUNISIA AFARIKI DUNIA
> Beji Caid Essebsi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92
> Alikimbizwa katika Hospitali ya Jeshi jana baada ya afya yake kubadilika
Zaidi, soma => https://jamii.app/RIP-Essebsi

MZEE KHAMIS KILOMONI AKAMATWA NA JESHI LA POLISI
> Khamis Kilomoni, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Simba SC amekamatwa kwa kuitisha kusanyiko nyumbani kwake bila kibali
> Aliandaa mkutano na Wanahabari nyumbani kwake Kinondoni, Dar
Soma > https://jamii.app/KilomoniAkamatwa

WATUMISHI KUKATWA MISHAHARA KWASABABU YA UBADHILIFU
> Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameiagiza Halmashauri ya Wilaya Biharamulo kuhakikisha inawachukulia hatua watumishi waliohusika na ubadhilifu wa fedha za umma na kutoa siku mbili kurejeshwa kwa fedha ambazo zimetumika kinyume na malengo

TANZANIA KUIUZIA KENYA MAHINDI ILI KUSAIDIA UPUNGUFU WA CHAKULA
> Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali itaiuzia Kenya Mahindi tani milioni 1 katika kipindi cha mwaka 1, baada ya msimu wa mvua kugoma nchini humo hali inayotishia kuwepo kwa upungufu wa chakula
Soma - https://jamii.app/TZKuuzaMahindiKE

BENKI YA DUNIA YATOA TAHADHARI KUHUSU DENI LA TAIFA NA MIKOPO
> Benki ya Dunia imetahadharisha kuhusu ukopaji unaofanywa na Serikali ya Tanzania na kuongeza kuwa ingawa deni hilo bado ni himilivu, ila umakini unahitajika kabla hali haijawa ngumu kwa Serikali kushindwa kutekeleza makubaliano
Soma - https://jamii.app/OnyoWBDeniTaifa

WAKIMBIZI 150 WAFARIKI BAADA YA BOTI YAO KUZAMA PWANI YA LIBYA
> Boti hiyo ilibeba takribani watu 300 ambapo baada ya ajali hiyo watu 145 wameokolewa mpaka sasa huku 5 wakiwa hawajulikani walipo
> Zoezi la uokoaji liliendeshwa na Wavuvi
Soma > https://jamii.app/Wakimbizi150Wafariki

NSSF KUFANYA MSAKO KWA WAAJIRI WASIOSAJILI WAFANYAKAZI KWENYE MFUKO
> Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii utaanza msako maofisini na kwenye kampuni kuwasaka waajiri ambao hawajawasajili wafanyakazi katika mfuko huo na wasiopeleka makato ya michango
> Msako utaanza Agosti 1 nchi nzima ili kuhakikisha waajiriwa katika sekta binafsi wanapata haki zao
Soma - https://jamii.app/NSSFMsakoWaajiri

RUFIJI: WATU WATATU WAFARIKI KWENYE AJALI
> Askari wawili wa kanda maalum Rufiji, pamoja na "staff officer" wamefariki katika ajali ya gari baada ya kupasuka kwa gurudumu la nyuma na kupinduka na kusababisha majeruhi wawili
> Waliofariki katika ajali hiyo ni Issah Bukuku, Inspekta Esteria wa RCO Rufiji na PC Lameck wa FFU Rufiji
Soma - https://jamii.app/AjaliVifoPolisi

MAREKANI YAIDHINISHA ADHABU YA KIFO KUANZA KUTEKELEZWA TENA
> Serikali ya Marekani imeidhinisha adhabu ya kifo ianze tena baada ya kusitishwa miaka 16 iliyopita
> Mwanasheria Mkuu ameiagiza Halmashauri ya Magereza kupanga siku ya kunyongwa kwa wafungwa 5 waliopewa adhabu hiyo kwa kuhusika na mauaji na ubakaji wa watoto na watu wazima
Soma - https://jamii.app/RejeshoAdhabuKifo

KIJANA AFARIKI BAADA YA KUTUMBUKIA KISIMANI
> Ali Ibrahimu Haji (30) Mkazi wa Jambiani Kibigija amefariki dunia baada ya kutumbukia kisimani katika Bar ya Maisha Pub, Mkoa wa Kusini Unguja
> Inasadikiwa alikuwa amelewa na aliondoka katika meza na kuelekea msalani na ndipo alipoingia katika kisima
Soma - https://jamii.app/AjaliKifoKisimani