JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WANAFUNZI WALIOKUWA WAHAMISHWE SHULE ZA VIPAJI MAALUMU, KUTOHAMISHWA

- Imesitisha kuwahamisha Wanafunzi 48 wa kidato cha 6 waliopata daraja la 3 kwenye mitihani ya muhula wa pili katika shule za vipaji maalumu kwenda shule za kawaida za bweni

Zaidi, soma https://jamii.app/Kidato6VipajiKotohamishwa
MOSHI: WATANO WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUIBA NONDO TANI 5

> Jeshi la polisi limewakamata watu 5 kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa tani 5 za nondo zilizokua zikitumika kwenye mradi wa ujenzi wa stendi kubwa ya mabasi ya Kimataifa

> Hatua ya kukamatwa kwa Watu hao inafuatia agizo lilitolewa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Soma - https://jamii.app/WiziNondoUjenzi
UFILIPINO: WANAFUNZI 12 WAFARIKI KWENYE AJALI
-
Wanafunzi 12 wa shule ya msingi, wenye umri kati ya miaka 10 na 12, wamefariki baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuanguka kwenye mwamba leo mjini Cebu
-
Taarifa inasema wanafunzi hao walikuwa wakisafiri kwenda kuhudhuria tukio ambalo lilikuwa linafanyika katika mji wa Boljoon, karibu na mahali ambapo ajali hiyo ilitokea
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Algeria maarufu ‘LesFennecs’ ndio mabingwa wapya wa #AFCON2019 baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Senegal maarufu ‘Teranga Lions’ goli 1-0 kwenye fainali

- Algeria inachukua ubingwa huo ikiwa mara ya mwisho ilikuwa bingwa wa AFCON miaka 29 iliyopita
MHANDISI WA MAJI WILAYA YA SAME ASIMAMISHWA KAZI

- Waziri Mkuu, Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi Mussa Msangi kwa kushindwa kusimamia mradi wa maji Hedaru

- Pia, amezivunja Jumuiya 3 za maji za Hedaru na kuagiza viongozi wake wahojiwe

Zaidi, soma https://jamii.app/MhandisiMajiSame
MAHAKAMA YAPENDEKEZA MAKOSA YOTE KUWA NA DHAMANA

- Mahakama ya Tanzania imependekeza makosa yote kuwa na dhamana na masharti ya dhamana hizo kulegezwa kwani itasaidia kuondoa msongamano wa Mahabusu kwenye Magereza mbalimbali nchini

Zaidi, soma https://jamii.app/PendekezoMakosaYoteDhamana
UZINDUZI WA TRENI KUTOKA DAR - TANGA - KILIMANJARO WAFANYIKA LEO

> Uzinduzi wa safari mpya ya treni ya mizigo umefanyika leo baada ya safari za treni hiyo kusimama zaidi ya miaka 12 iliyopita

> Uzinduzi huo umefanywa na Waziri Mkuu ambaye ameipokea treni iliyotokea Tanga ikiwa na mabehewa 20. Mpaka sasa Serikali imeshatumia Tsh. Bilioni 5.7 ili kuirudisha njia hiyo

Soma - https://jamii.app/UzinduziTreniDarKLM
LUSINDE: NAPE NNAUYE NA ABDULRAHMAN KINANA WAHOJIWE POLISI

- Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde ametaka wahojiwe kwa madai kuwa wamemtukana Rais Magufuli

- Alikuwa akizungumzia sauti zilizosambaa mtandaoni zikidaiwa kuwa ni za Nape

Zaidi, soma https://jamii.app/Lusinde-KinanaNape
BANGI YASABABISHA MJUKUU AUWE BIBI YAKE KWA KUMCHINJA

> Athuman Khamis ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Usongwa Mkoani Tabora anatuhumiwa kumuua kwa kumchinja bibi yake, Rahel Daud (67) huku sababu ikielezwa ni uvutaji wa bangi kwa kijana huyo

> Taarifa inasema alimvizia bibi yake akiwa ndani na kumchinja kwa kumtenganisha kiwiliwili na Kichwa

Soma - https://jamii.app/MjukuuAuaBibi
ARUSHA: MHASIBU WA JIJI ATUHUMIWA KUTAFUNA MILIONI 85 KILA MWEZI

- Charles Jacob ametakiwa kujisalimisha Polisi akidaiwa kula fedha ktk mzani wa mazao ya chakula

- Inadaiwa mzani unaingiza Tsh. Milioni 3.3 kwa mwezi badala ya Tsh. Milioni 88

Zaidi, soma https://jamii.app/MhasibuArushwaAtakiwaPolisi
WATU 152 WAFARIKI KUTOKANA NA MAFURIKO KUSINI MWA BARA LA ASIA

> Takribani watu 90 wamefariki nchini Nepal, watu 50 kutoka katika Jimbo la Assam nchini India na wengine kutoka nchini Bangladesh tangu kuanza kwa mafuriko yaliyotokana na msimu wa mvua za masika

> Katika jimbo la Assam watu milioni 4.8 katika vijiji 3,700 wameathiriwa na mafuriko na Faru 10 wenye pembe moja wamekufa baada ya kingo za mto kupasuka na mafuriko kuingia kwenye Mbugani

#JFLeo
UJERUMANI NA UFARANSA ZAITAKA IRAN KUIACHIA MELI YA UINGEREZA

- Ujerumani na Ufaransa zimelaani hatua ya Iran ya kuikamata meli yenye bendera ya Uingereza katika mlango bahari wa Hormuz na kuitaka nchi hiyo kuiachia huru meli hiyo mara moja

Zaidi, soma https://jamii.app/UjerumaniUfaransa-Iran
RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA WAZIRI JANUARI MAKAMBA, SIMBACHAWENE ACHUKUA NAFASI YAKE

> Januari Makamba January Makamba ametenguliwa, nafasi yake inachukuliwa na George Simbachawene

> Ndg. Hussein Bashe anakuwa Naibu Waziri wa Kilimo

Soma > https://jamii.app/JanuariMakambaOut
JamiiForums
Photo
JANUARY MAKAMBA: NIMEYAPOKEA MABADILIKO KWA MOYO MWEUPE

> Asema ataongea zaidi siku zijazo

> Ni muda mchache baada ya kutangazwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri
DERA ISMAIL KHAN, PAKISTAN: MASHAMBULIO DHIDI YA POLISI YAUA WATU 8

> Kati ya waliofariki, askari polisi ni wanne

> Imethibitika kuwa shambulio la pili lilikuwa la kujitoa mhanga lililofanywa na mwanamke katika lango la kuingilia hospitali

Soma https://jamii.app/PoliceAttackPakistan
HYDERABAD, INDIA: MTANZANIA MBARONI KWA KUENDESHA DANGURO

- Ramadhani Usanga Sabia Bayoni akishirikiana rafiki yake, huweka picha za wanaowauza kwenye tovuti za ngono ili kuwavutia wateja

- Wateja hao hulipa Rs 10,000(Sawa na Tsh. 334,162.72)

Soma https://jamii.app/TanzanianArrestedInIndia
KAGERA: KATIBU MWENEZI CHADEMA ADAIWA KUJINYONGA

- Ni Nurunet Bakaishumba(35) Katibu Mwenezi wa CHADEMA katika Kata ya Igurwa, Wilayani Karagwe

- Ameacha ujumbe kwamba familia yake haihusiki na kifo chake na wazo kujinyonga alikuwa nalo kwa muda wa mwezi mmoja sasa

Soma https://jamii.app/KatibuMweneziCHADEMAAjinyonga
#JFLeo
KENYA: MLINZI WA SPIKA AULIWA KWA KUPIGWA RISASI

> Mlinzi wa Spika wa Bunge la Kaunti ya Embu ameuliwa kwa kupigwa risasi mapema jana eneo la Kamiti Corner jijini Nairobi

> Aidha dereva wake amekamatwa baada ya uchunguzi wa mwanzo kubaini kuwa huenda alihusika

Soma - https://jamii.app/SpeakerGuardShortDead
TATHMINI YA CHAKULA: HALMASHAURI 46 ZAWEZA KUPATA UPUNGUFU WA CHAKULA

> Wizara ya Kilimo imebaini Halmashauri 46 katika Mikoa 13 zina dalili ya kukumbwa na upungufu wa chakula kutokana na changamoto zilizoathiri uzalishaji wa chakula kwa msimu wa 2018/19, ikiwa ni pamoja na upungufu wa mvua

> Tathmini hiyo huangalia baadhi ya mazao muhimu yanayohitajika zaidi ikiwamo Mahindi, Mtama, Ulezi, Mchele, Kunde, Ngano, Ndizi, Mihogo na Viazi

Soma - https://jamii.app/Halmshr46UpungufuChakula